Msaada wa kiroho, kuna jambo zito linanisumbua

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
5,497
Reaction score
5,198
Kwanza habari za kwenu,

Naomba msaada binafsi naishi,

Yale maisha ya kawaida tu kiimani yaani sio mshika dini sana na hata kanisani huwa siendi nina zaidi ya mwaka na nusu sijaenda, ila kuna hali flani nadhani Mungu au malaika wa Mungu wana waniambia kitu ( I'm not kama ni malaika kweli au wenge langu tu mwenyewe )

Kuna sauti ndani ya moyo wangu imekuwa inaniambia nifanye sana maombi hasa ya kufunga na kila jambo litakuwa sawa hii sauti imeanza tokea mwaka Jana lakini nimekuwa mgumu kuomba wala kufunga na mwaka.

Jana bila kutarajia nilinunua tu ghafla bibilia kwa ushawishi wa hiyo sauti lakini hadi Leo sijawahi hata kusoma hiyo bibilia zaidi ipo tu chumba kwangu na hata mwaka huu kuna vitabu nilinunua vya kufanya maombi lakini huwa kila nikitaka kusoma hivyo vitabu plus bibilia kuna mambo 3 huwa ama nitahisi uvivu kusoma bibilia na hivyo vitabu na nikijilazimisha basi usingizi hunipitia. 2 nikianza kusoma lazima kuna mchepuko nilio wahi kutongoza au msichana yoyote ghafula anaweza kukutext.

Yes nina kisimati cha wadada hadi nahisi UKIMWI utanipa mkataba najaribu kuzuia hii hali ya kupenda ngono kupitiliza siwezi na bahati mbaya au nzuri sijui wadada huwa nikiongea nao hata hawagomi inanikera hii hali utumwa wa ngono huu ila ndiyo kuacha siwezi ) na 3 inawezekana kupata dharula yoyote au naweza kuacha kusoma bibilia na kujikuta nipo bize nachat.

Zaidi ya wiki 2 huwa nikilala usiku bado inajirudia na sometimes nikiwa usingizi huwa naona kuna mtu ana mavazi meupe, anasisitiza sana nifunge na kufanya maombi ili milango yangu yangu ifunguliwe, kiufupi kuna history mbaya sana na mama wangu wa kambo amekuwa anasema amenifunga nyota zangu sijui kanipa nyota ya punda (nimezaliwa 11/8 na nyota ni simba) huyu mama kambo hayo mambo ya ushirikina kaanza tokea zamani, sasa nimemaliza chuo kikuu lazima mambo yangu hayapo vizuri kabisa japo nafanya sana jitihada za kutafuta pesa na sikatai tamaa.

Na huwa moyo na mwili najisikia sana raha na Amani nikisikiliza nyimbo za dini za kuabudu huwa moyo wangu na akili zangu zinakuwa na utulivu sana

Japo niwe mkweli nimekuwa mgumu kuamini ishu za uchawi.

Hebu wataalamu wa mambo ya imani kuna ujumbe gani au hiyo sauti ina maana gani au ni mawenge yangu tu ya stress zangu za ugumu wa life kipindi hiki cha Uncle Magufuli.
f48b668d33ca36329c48b101f1721811.jpg
 
Hizo sauti kama ni za mkwara kama ya Mkuu wa nchi bora umrudie Muumba wako.
 
Haaaaa haaa haaaaa.
Comment namba #3 inachekesha sana.

Yaani, hata uandishi wako unachekesha kama simulizi hivi za riwaya.

Any way pole sana.
 
Mcheki yule mtu wa pale ubongo external atayamaliza faster, anaitwa mzee wa bapa
 
Nguvu mbili MUNGU na shetani wanaligania maisha yako.ni Rahisi sana kuchukua maamuzi,amua kwenda kwa MUNGU au kwa shetani,yaani tenda mema acha dhambi au tenda dhambi acha mema.na unaweza kufanya lolote kwa akili na maamuzi yako

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
unajua kama ukimtaka dem hakatai kwa nini unawatakataka?

anza kwenda kanisani na ukiweza kakutane na padre, au paloko muelezee,.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza habari za kwenu,

Naomba msaada binafsi naishi,

Yale maisha ya kawaida tu kiimani yaani sio mshika dini sana na hata kanisani huwa siendi nina zaidi ya mwaka na nusu sijaenda, ila kuna hali flani nadhani Mungu au malaika wa Mungu wana waniambia kitu ( I'm not kama ni malaika kweli au wenge langu tu mwenyewe )

Kuna sauti ndani ya moyo wangu imekuwa inaniambia nifanye sana maombi hasa ya kufunga na kila jambo litakuwa sawa hii sauti imeanza tokea mwaka Jana lakini nimekuwa mgumu kuomba wala kufunga na mwaka.

Jana bila kutarajia nilinunua tu ghafla bibilia kwa ushawishi wa hiyo sauti lakini hadi Leo sijawahi hata kusoma hiyo bibilia zaidi ipo tu chumba kwangu na hata mwaka huu kuna vitabu nilinunua vya kufanya maombi lakini huwa kila nikitaka kusoma hivyo vitabu plus bibilia kuna mambo 3 huwa ama nitahisi uvivu kusoma bibilia na hivyo vitabu na nikijilazimisha basi usingizi hunipitia. 2 nikianza kusoma lazima kuna mchepuko nilio wahi kutongoza au msichana yoyote ghafula anaweza kukutext.

Yes nina kisimati cha wadada hadi nahisi UKIMWI utanipa mkataba najaribu kuzuia hii hali ya kupenda ngono kupitiliza siwezi na bahati mbaya au nzuri sijui wadada huwa nikiongea nao hata hawagomi inanikera hii hali utumwa wa ngono huu ila ndiyo kuacha siwezi ) na 3 inawezekana kupata dharula yoyote au naweza kuacha kusoma bibilia na kujikuta nipo bize nachat.

Zaidi ya wiki 2 huwa nikilala usiku bado inajirudia na sometimes nikiwa usingizi huwa naona kuna mtu ana mavazi meupe, anasisitiza sana nifunge na kufanya maombi ili milango yangu yangu ifunguliwe, kiufupi kuna history mbaya sana na mama wangu wa kambo amekuwa anasema amenifunga nyota zangu sijui kanipa nyota ya punda (nimezaliwa 11/8 na nyota ni simba) huyu mama kambo hayo mambo ya ushirikina kaanza tokea zamani, sasa nimemaliza chuo kikuu lazima mambo yangu hayapo vizuri kabisa japo nafanya sana jitihada za kutafuta pesa na sikatai tamaa.

Japo niwe mkweli nimekuwa mgumu kuamini ishu za uchawi.

Hebu wataalamu wa mambo ya imani kuna ujumbe gani au hiyo sauti ina maana gani au ni mawenge yangu tu ya stress zangu za ugumu wa life kipindi hiki cha Uncle Magufuli.
Wewe umebarikiwa na wachawi wanakuogopa ww ni mtu wa mafanikio ila una maadui wengi ila ukirudi kwa mungu wako utafanikiwa sana kwa maana umechaguliwa na wanga wanajua the chosen one ila acha pombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko serious au zile riwaya zako?! hahahahahha. namtaka ndugu yangu "Romeo" hahahahahaha
 
Note: Ushauri wowote utakaopewa usiohusisha wewe kutakiwa kumcha Mungu hautaweza kutatua tatizo permanent.
Nenda makanisa yanayoamini Injili na kuombewa watu wajawe Roho mtakatifu.
Pole, Mungu anampango nawewe.
 
Ukipewa huo mkataba ndio utajua kuanzia mwanzo mpk ufunuo
 
Au nenda mwanza nasikia kuna dini wanaombea kwa jina la zamaridi kama umenunua bible na hutaki kusoma n kanisani huendi tukusaidieje?
 
Fanya hii for experiment,mtafute mchungaji akuongoze bure sala ya toba,kaza sana kusoma hiyo biblia japo paragraph moja kila siku,hudhuria ibada ingawa mwanzo hutajisikia amani katika nyumba ya sala utapata maumivu yasiyoeleweka usikate tamaa,unaweza hata kupitiwa na usingizi lakini usiache kaza tu,baada ya hapo uwe na mazowea ya kuomba japo kwa dk 30 peke yako,utahisi msisimko wa ajabu usiache.
Mungu ana neno na wewe lakini shetani anakuzuia.
Ukikwama nitafute pm. Utashinda na zaidi ya kushinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom