Msaada wa jinsi ya kuandika makala

Msaada wa jinsi ya kuandika makala

Joined
Mar 12, 2015
Posts
25
Reaction score
2
Napenda sana uandishi hasa wa makala, ningependa nijuzwe jinsi ya kuandika au kwa mtu mwenye summary naomba tuwasiliane ili aweze kunisaidia katika hilo.

Nawasilisha wanajamvi
 
Makala za nini unapenda kuandika, naweza kuwa msaada!
 
Makala za masuala ya afya kwa mfano!!

Afya ni technical sana, inabidi uwe mweledi wa mambo hayo. Wanapendekeza wataalamu wa Afya ndio wawe waandishi wa hayo mambo!

Wewe unaweza kuandika mambo ya afya kwa mtazamo wa kijamii na siasa zake, lakini sio kuhusu magonjwa. Mwandishi asiye na uzoefu na mambo ya afya akilazimisha kuandika ni kutafuta kuchanganya watu tu!
 
Napenda sana uandishi hasa wa makala, ningependa nijuzwe jinsi ya kuandika au kwa mtu mwenye ummary naomba tuwasiliane ili aweze kunisaidia katika hilo.

Nawasilisha wanajamvi

Kwanza fikiria unataka kufikisha ujumbe gani kwa msomaji. Pili fikiria hadhira/wasomaji unaotaka kuwalenga. Huwezi kumwandikia kila mtu. Kisha brainstorm namna ya kuufikisha ujumbe wako kwa kutumia sifa za unaotaka kuwafikia.

Hatua inayofuata ni kuandika dondoo kadri zinavyokuja kichwani. Fikiria kwa mtindo wa point fupi fupi zinazokamilisha ujumbe wako. Hizi zitakuwa kama sub-headings za makala yako.

Mpangilio wa sub-headings zako uwe kwenye mtiririko unaoeleweka kwa unaowalenga lakini muhimu anza na utangulizi...onesha tatizo liko wapi na kwa nini tunahitaji kusoma makala yako. Kisha onesha kinachofahamika kwa wengi then tupe unayodhani tunahitaji kuyajua ili kutatua tatizo uliloliainisha hapo juu.

Baada ya kuridhika na dondoo zako...anza kutiririka chini ya kila subheading bila kujali makosa ya kiuandishi nk. Andika as you think. Flow.

Then anza kuhariri...jazia hoja...penye kuhitaji matokeo ya tafiti soma eneo hilo...jazia....punguza unavyohisi vinahitaji kupunguzwa etc.

Inashariwa kama makala ni ndefu weka sub-headings kumrahisishia msomaji mvivu na hakikisha sentensi ya kwanza kwenye aya inabeba ujumbe. Sentensi zinazofuata zifafanue tu.

Kumbuka unachoanza na kumaliza nacho ni muhimu kuliko aya za katikati. Weka msisitizo hapo. Pia epuka lugha technical sana kama huwaandikii wataalam wenzako.

Kila la heri 🙂
 
Kwanza fikiria unataka kufikisha ujumbe gani kwa msomaji. Pili fikiria hadhira/wasomaji unaotaka kuwalenga. Huwezi kumwandikia kila mtu. Kisha brainstorm namna ya kuufikisha ujumbe wako kwa kutumia sifa za unaotaka kuwafikia...

Umeelezea vizuri sana kaka na ninakupongeza
 
Back
Top Bottom