orangutan
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 759
- 772
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa muziki huu wa kizazi kipya tangu kipindi kile cha miaka ya 98 ulipoanza kukubalika katika jamii yetu ya kibongo na kukonga nyoyo za watu wa rika lolote bila kujali wadhifa wa mtu. Na kusema kweli nikijaribu kucheki ngoma za siku hizi za hiphop ya kibongo, nimegundua kuwa hazifikii hata chembe mikwaju iliyokuwa ikigongwa na real MCs wa kipindi kile cha kina fanani na Hasheem Dogo.
Kilichonishawishi kuanzisha huu uzi ni kutokana na ukweli niliogundua kuwa baadhi ya nyimbo nyingi kali za wasanii wa hiphop wa kipindi kile hazipatikani kabisa mitandaoni hata kupata album zao kitaa ni ishu. Huwa naishia tu kuzisikia mara mojamoja kutoka kwenye zile redio kongwe zenye maDJ wanao-appreciate muziki wa kikizazi kipya old skul.
Nimejaribu kuzitafuta ngoma zifuatazo mtandaoni bila mafanikio kwa muda mrefu sasa;
1.GANGWE MOBB-Laifu la uswazi
2.KALI P-Tumbo joto
3.HITS za waturutumbwi kutoka r CHUGGA
4.Mr 2 SUGU-hii ni noma
5.Inspector Haroun-kisa cha baba mkwe
6.AY-mchanga wa macho
7. Pauline Zongo-Dunia ni ndogo sana
8.Stan boy-njoo kwangu
9.Balozi-wengi walikuwepo
10. Manyema Family-Jinsi Tulivyo
11.Wagosi wa kaya-nyeti, soka la bongo
12. Chindo Man-Mbwa mzee ndo Anabweka
13.EStam-sikiliza wimbo
Yeyote mwenye wowote kati ya hizo nyimbo naona afanye namna aweze ku-upload hiyo ngoma ili wadau wa muziki tuendelee kuenjoi haya mangoma adimu. (Link za mtandaoni pia zinakaribishwa- ila zisiwe zile zinazoruhusu kuplay online peke ake kama muziki.net au eastafricantube). Thank you in advance!!!!!!!!!!!!!!