Msaada wa hili, miguu inakufa ganzi

Tempest

Senior Member
Apr 26, 2022
192
296
Habarini wadau,

Kama wiki sasa nimepata hili tatizo la miguu kufa ganzi, wa kushoto ndio sana mpaka sasa nakuwa siu feel kwa kiasi kikubwa, nikajua itaenda ikipungua ila naona ipo same au kama inapungu basi taratibu sanaaa kiasi chja kwamba siwezi jua,

Kama kuna yoyote mwenye ujuzi au alishawahi kukumbana na hili akapona msaada wako unahitajika

Hospital nimeenda mara mbili mara ya mwisho leo, mara ya kwanza niliambiwa inaweza kuwa ni upungufu wa Vitamin b12 maana dalili pia zinaambatana na ngozi kuwa kavu sana uchovu n.k nikachoma sindano kadhaa za vitamin b12 pamoja na vidonge ila mpaka leo maendeleo ni hafifu tu, leo nikaenda kucheki sukari pamoja na syphilis kwa mujibu wa dokta maana niliambiwa asilimia kubwa itakuwa ni sukari ila majibu yote hayo yamekuwa negative

Msaada kwenye hili tafadhali maana nahisi ni nerve damage somewhere ila sijui cause ndio inaniogopesha nahofia isije ikawa permanent hii feeling which is bad sana kwa upande wangu.
 
Una umri gani...

Una shida/ugonjwa wowote chronic?

Umeenda hospitali gani?

Kama upo mkoa wenye hospitali kubwa(kanda/taifa) nenda kaonane na neurosurgeon na ufanye definitive investigations, tatizo litaisha tuu.
 
Mama yangu anatatizo kama lako yeye ni upande wa kushoto. Alienda hospitali mbili tofauti zote wakamwambia anatatizo kwenye uti wa mgongo kuna mishipa fulani imepishana.

Jaribu kwenda kwenye hospital kubwa wanaweza kugundua nini tatizo
 
1. Unapresha hujafumaniwa??
2.umemlaghai mtu kitu au umegombana na mtu??
Ipo hivi unaweza kuwa unaogopa kisa hayo mawili umemrusha mtu au umefumaniwa so akilini kwako imejengeka wasiwasi hadi imeleta ganzi.

3. Kulogwa kupooo so kuwa makini
 
Mama yangu anatatizo kama lako yeye ni upande wa kushoto. Alienda hospitali mbili tofauti zote wakamwambia anatatizo kwenye uti wa mgongo kuna mishipa fulani imepishana. Jaribu kwenda kwenye hospital kubwa wanaweza kugundua nini tatizo
Tiba je au ni mpaka leo tatizo bado lipo
 
Umri 27 , sina ugonjwa chronic , nimeenda hospital Mico
Hivi mnazipendeaga nini hizo hospitali za binafsi?

Sasa mkuu, nenda MNH au MLOGANZILA kaonane na Neurosurgeon.

Huko kwingine utapigwa pesa, mwisho wa siku utapewa rufaa ya kwenda hukohuko ambako ulikuwa unapakimbia.
 
1. Unapresha hujafumaniwa??
2.umemlaghai mtu kitu au umegombana na mtu??
Ipo hivi unaweza kuwa unaogopa kisa hayo mawili umemrusha mtu au umefumaniwa so akilini kwako imejengeka wasiwasi hadi imeleta ganzi.

3. Kulogwa kupooo so kuwa makini
Maybe, sijataka kuanza na haya kwanza ngoja nihangaike na menngine ila ntawachek wazee nao
 
Hivi mnazipendeaga nini hizo hospitali za binafsi?

Sasa mkuu, nenda MNH au MLOGANZILA kaonane na Neurosurgeon.

Huko kwingine utapigwa pesa, mwisho wa siku utapewa rufaa ya kwenda hukohuko ambako ulikuwa unapakimbia.
MNH naenda kitengo gani? nipe direction kidogo au naulizia Neurosurgeon
 
Habarini wadau,
Kama wiki sasa nimepata hili tatizo la miguu kufa ganzi, wa kushoto ndio sanaa mpaka sasa nakuwa siu feel kwa kiasi kikubwa, nikajua itaenda ikipungua ila naona ipo same au kama inapungu basi taratibu sanaaa kiasi chja kwamba siwezi jua,

Kama kuna yoyote mwenye ujuzi au alishawahi kukumbana na hili akapona msaada wako unahitajika

Hospital nimeenda mara mbili mara ya mwisho leo, mara ya kwanza niliambiwa inaweza kuwa ni upungufu wa Vitamin b12 maana dalili pia zinaambatana na ngozi kuwa kavu sana uchovu n.k nikachoma sindano kadhaa za vitamin b12 pamoja na vidonge ila mpaka leo maendeleo ni hafifu tu, leo nikaenda kucheki sukari pamoja na syphilis kwa mujibu wa dokta maana niliambiwa asilimia kubwa itakuwa ni sukari ila majibu yote hayo yamekuwa negative

Msaada kwenye hili tafadhali maana nahisi ni nerve damage somewhere ila sijui cause ndio inaniogopesha nahofia isije ikawa permanent hii feeling which is bad sana kwa upande wangu
Pole,
Kuna mambo zaidi nahitajji kujua:

1: Ganzi ilianzia wapi, na mpaka sasa iko sehemu gani mguu/miguu?

2: Ilianza miguu yote kwa pamoja?

3: Una maumivu yoyote kwenye uti wa mgongo?

4: Unafanya kazi zote nzito za kuinama?
 
Uzito
Umri
Hiv/aidis
Ukosefu wa calcium
Vitamin B
Kurogwa

Cheki kimojawapo
Uzito wa kawaida, 68 age 27 ngoma sina nimepima last week, vitamin B natumia dawa zake , kurogwa naweza check next
 
Mkuu Fanya mazoezi ya jogging kwa wiki Moja ukiwa na viatu na tracksuit toka jasho la kutosha halafu wiki ijayo lete majibu. Utanishukuru badae
 
MNH naenda kitengo gani? nipe direction kidogo au naulizia Neurosurgeon
Kama una bima nenda directly waambie nahitaji kuonana na neurosurgeon au daktari wa mishipa ya fahamu....

Unaweza kuanzia just kwa general physician, then uone feedback utakazopata, maana inawezekana ni katatizo kadogo tuu..
 
Back
Top Bottom