Msaada wa haraka hii hesabu!!!

Wale wataalam wa hesabu hebu nisaidieni namna ya kusolve hii haraka, nimejaribu njia zote nimeshindwa (Log... etc), sasa sijui ni uzee unanisumbua!!


2[SUP]x[/SUP]=4X

The answer is 4, sasa tatizo ni namna ya kuipata hiyo 4.

kaka hiyo sio Hesabu ni HISABATI hesabu kila mtu anaweza zile za kuuzia machungwa ndo hesabu!!!
 
nami nakubali hiyo sio hesabu ila ni hisabati, na naomba watu wawakubali watu waliofanya vizuri ktk mambo mbalimbali. "APPRECIATION WANDUGU"
 
2^x =4x......log
log2 ^x=log4x.
Xlog2=log(2^2)X.
Xlog2=log(2^2)+logX.
Xlog2=2log2+logX
logX=Xlog2-2log2
logX=(X-2)Log2
X=(X-2)2
X=2X-4
4=2X-X
X=4.

Kuanzia leo!!! I salute u! Mweleshe tu kama base na log ya namba zinafanana jibu lake ni moja
 
wakuu wote mnaohoji log ilivyopotea nilishasawazisha kwenye post yangu iliyofatia labda ilikuwa ngumu kuiona. fata mtiririko huu ili tuelewane
2[SUP]x[/SUP] =4x..............................................apply log
log2[SUP]x[/SUP]=log4x.
Xlog2=log(2[SUP]2[/SUP])X.
Xlog2=log(2[SUP]2[/SUP])+logX.
Xlog2=2log2+logX
logX=Xlog2-2log2
logX=(X-2)Log2.........................gawanya kwa (x-2)log2both sides
logx =1
(x-2)log2
logx =1.............................................................andika hiyo katika mfumo wa log under base,


log2(x-2)

log [SUB]2(x-2)[/SUB]X=1..................................................................................ibadilishe katika exponential form
2(x-2)[SUP]1[/SUP]=x
2x-4=x
2x-x=4
X=4.

Huyu ndie mke nilipaswa kua nae!!! kichwa nzuri hata nikikuambie tusinunue cheni na tununue matofari haraka utanielewa!!! hongera sana!! proud of u!!
 
Nimeipenda hii.
Nimeanza kufanya mazoezi ya kukokotoa maana dogo anakuja kwa kasi sana, nisije nikaumbuka bure
 
hapa bila kuchora graph au kutumia try and error method hamna jibu.

Wajua hisabati kweli?

Njia aliyotumia mdada ni sawa kabisa hakuna cha graph hapo!! kaaply theory za log tu!!

amenikumbusha mbali sana niliwapeleka noma
 
kaka hiyo sio Hesabu ni HISABATI hesabu kila mtu anaweza zile za kuuzia machungwa ndo hesabu!!!


Za kuuzia machungwa ni MA.GA.ZI.JU.TO........... Remember? kwangu mimi hesabu ni jenero tem hata kuhesabu vidole ni Hesabu.
 
dada angu husninyo , nadhani hapo kwenye red utakuwa umpitiwa , hauwezi kuzi ingiza hizi no (x-2) ndani ya log kienyeji hvyo ,
nakumbuka hii hesabu ilituangaisha sana o-level , mwisho wa siku soln pekee kwa mwanafunzi wa o-level ni kuchora graph tu.
Log ina limitations zake katika kusolve matatizo , na mojawapo ni ili , its unsolvable kwa kutumia log concept ,
ndo maana ukifika a-level unafundishwa other estimation techniques kama newton raphson na nyinginize

hapo kapitiwa
 
Samahani sana dadangu mpendwa. nashukuru sana umenipa mwanga, ni kijana (mtoto) wangu mmoja amenitumia hiyo hesabu na kwamba nikishinndwa nimpe hela (huwa tunashindana). sasa najua kabisa atanibana kwenye maswali kama hayo nikirudi nyumbani. ulivyonitumia hiyo soln ilibidi nichekicheki vitabu hapa lakini havisemi kitu kama hicho.

Kitu ulichosema hapo ninavyojua ni kwamba Log[SUB]10[/SUB]10 ndio moja, sasa kwa case yetu hiyo red 10 haipo, itakuaje moja!!

wakuu sikupenda kujiingiza kwenye hii mada lakini nimelazimika na huyu husninyo anavyokuwa anajibadilisha jinsi kama siyo jinsia kwa kila mada hii anakuwa anategemea nini au watu hawafuatilii michangoo yake humu jamvini...huyuhuyu kuna sehemau amejitambulisha kuwa yeye ni he na siyo she....hapa bwana Dasa amembana na ghafla amekanusha kuwa yeye siyo he ni she........

Nini kulikoni..jamani ni wazo tu na halitaki kujibiwa ila siyo vizuri kukanganya wanajamii kwa namna hiyo
 
logx =1............................ .............................. ...andika
hiyo katika mfumo wa
log under base, log2(x-2) log 2(x-2) X=1........................... .............................. .........................ibadi lishe katika exponential
form 2(x-2)^1=x
Husninyo,hapo ndo penye uongo! Huwezi ibadili kiivyo.(X-2)log2 sio sawa na log2(X-2),bali ni (X-2)log2=log2^(X-2) na sio vinginevyo.Ishu hapo ni kutumia gragh tu! Kutumia log concept ni kulazimishana uongo tu!
 
Last edited by a moderator:
Husninyo na dasa mnanikumbusha mbali, asanteni ndugu zangu. Ninachoweza kusema kwa leo na siku zote ni numbers do not lie. Big up.
 
Hapo mie naona kama niko gengeni nanunua nazi, mwe!

yaan,,,naichukia hesabu kama msiba wa kambarage,,,,mliosoma lyamungo sec,,,miaka,ya,1989/92,,,mnamkumbuka mama pallagyo,,,,akitukusanya,,,form/either/jktu,,mnajazwa class ya wa2 35 mnaingia 150,,hata ufanyaje,atakuacha,,sasa siwezi kuipenda tena japo pr loo bonge ya mkali enzi hizoooooooo,acha tu,,
 
Heshima mkuu. lakini kwenye red hiyo sheria ni ipi hiyo!!. hiyo Log jinsi ilivyopotea hapo!!.

maana nilitegemea iwe:

LogX=(X-2)Log2
X=2[SUP](X-2)[/SUP] then uendelee kutoka hapo.

Hiyo sheria uliyotumia hapo juu, naomba ifafanue zaidi.

safi sana husininyo.Hapo kwenye red,their is no such a law.
 
Hapo ndo tungundue tatizo la mfumo wetu wa elimu! Nijuavyo mimi nivigumu kwa mtu ambaye amemaliza shule 20 years ago,hata kama alikuwa mkali kwenye masomo husika endapo hilo somo sio eneo lake la kazi (walau anajikumbushia kila mara)usishangae kumkuta mtu anajiuliza endapo aliwahi kuona kitu kama hicho. Kwa sisi tuliowahi kuwa walimu nadhani huwa inaudhi unapowauliza wanafunzi kuhusu topic fulani ambayo walikuwa wanafundishwa na mwalimu aliyetangulia kisha unaambiwa HATUKUFNDIHWA HAPO! Kumbe wanafunzi wameandika kwa ajili ya test na kisha wanaweka material kapuni. Kwa mtindo huu unawezekana kabisa kushindwa hata mambo madogo ya msingi
Hizi ngoma nilikuwaga vema sana, tatizo ni hizi shule za kufanyia mitihani huwezi amini ngoma imekataa kabisa shiiit. Alafu leo hii nipo kazini kwasababu nilifanya vizuri katika masomo yangu
 
SASA NAONA WOTE CHALI KI2 HICHI SIMCHEZO.
O-level MTUPISHE KIDOGO
IT'S GOING DOWN LIKE THIS...
2^x = 4x
1 = 4x*2^(-x)
1/4 = x*2^(-x)
1/4 = x*e^(-x ln(2))
-ln(2)/4 = -x ln(2)*e^(-x ln(2))
W(-ln(2)/4) = -x ln(2)
W(-ln(2)/4) / -ln(2) = x
Where W is the Lambert W-Function.
Wolfram Alpha approximates the
solution as
0.309906932380
KAMA HUJAELEWA AU KUNA SEHEMU
UMEACHWA ULIZA. MATHEMATICS BONGO NI
UGONJWA WA TAIFA.
 
Nimepitia mabishano na solution zenu pamoja na thread ya huyu jamaa nikiwa na T.O wa advanced mathematics mwaka 2009 ametoka PUGU na kwa sasa yupo UDSm anasoma BCOM finance Tumecheka sana kutokana kuwa hili swali tumeshalifanyia kazi na huyu T.O ELINEEMA MOLA alipata 98% ya Pure math form six.
JIBU LA SWALI KUNA JAMAA MMOJA kapata ameandika comenti kuwa Hufanywa kwa njia ya Inspection yaani makadilio hili swali ni pamoja na lile la 3^x=9x huwa hakuna njia maalumu zaidi ya kupachika number na kuzijaribu kwenye equation.ASANTEN N POLEN KWA KUMALIZA ROUGH KUTAFUTA JIBU. Na pia kama bwana DASA unabisha toa njia niikosoe.
Elineema 🙌
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom