Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Msaada wa China: Haya ni baadhi tu ya masharti

Duu inauma saaana, natamani bora ningezaliwa mjinga, ningekuwa zangu tu CCM miguuni nimevaa yeboyebo sijui kinachoendelea wala roho isingeniuma, siku hizi nikiona viongozi wanaingia mikataba napata tumbo la kuharisha. Sasa huu ni wa china ambao wanadai hauna masharti, je safari ya ufaransa ilikuwaje? Kanada kwenye mafarasi je? sijui tufanyeje ndugu zangu Watanzania, urithi wa watoto wetu unateketea tukiangalia hivi hivi
 
Kizazi kijacho kitatulaumu sana kwa aina ya mikataba tunayoingia.
Mbaya zaidi huwa hatujifunzi kutokana na makosa.
 
mhh...!ni lazim iwe hivyo cz serkali ya china ipo kwa ajili ya maslahi ya wachina...!
lakini pia tucsahau kuwa china ya sasa si china ile yenye misingi ya ujamaa(pure socialist)NB;hakuna yeyote atakae tuondoa kwenye lindi la umaskini than our own plans our own efforts by our own resources...!
 
Haya aliyoyasema hapa Rais wa china siyo mageni kwani yalikwisasemwa ikiwa ni pamaoja na idadi ya fedha hizo billion 20. Nafikiri mnakumbuka mwaka Jana viongozi wa Afrika walialikwa china na kulipiwa ghjarama yakasemwa hayahaya aliyoyasema Rais mpya wa china! Kinachonishangaza ni jinsi tulivyoshangilia kana kwamba ni kitu kipya sana na kwamba tunapewa bure. Hakuna kitu kinaitwa masharti nafuu - masharti Yao pengine ukiyachambua ni magumu zaidi. Kwa nini atuwekewi wazi mikataba iliyosainiwa.
 
Masharti ni nafuu kabisa mnaopiga makelele nna matatizo ya akili
 
Basi tujengee wewe hiyo bandari bila masharti

Wewe tumeisha kustukia na ajira yako mpya ya kuharibu thread!

Yaani inaingia akilini kweli eti kwa vile mwekezaji basi asiwe na mshindani nadani ya km 200? kwanini kama anajua service zake zitakuwa nzuri? Ahapa tumeliwa
 
Puzzled kidogo umesema ni mkopo toka china alafu tunawapa wanaendesha iyo bandari kwa miaka 50?
Sasa huo mkopo ni wa nini kama wataendesha kwa iyo miaka maana watakuwa wamerudisha ela yao au bila mkopo ilibidi ikae kwao miaka 100 elimu zaidi pls kabla sijalipuka apa
Inauma kama ni kweli
 
Haya aliyoyasema hapa Rais wa china siyo mageni kwani yalikwisasemwa ikiwa ni pamaoja na idadi ya fedha hizo billion 20. Nafikiri mnakumbuka mwaka Jana viongozi wa Afrika walialikwa china na kulipiwa ghjarama yakasemwa hayahaya aliyoyasema Rais mpya wa china! Kinachonishangaza ni jinsi tulivyoshangilia kana kwamba ni kitu kipya sana na kwamba tunapewa bure. Hakuna kitu kinaitwa masharti nafuu - masharti Yao pengine ukiyachambua ni magumu zaidi. Kwa nini atuwekewi wazi mikataba iliyosainiwa.

Pengine bora hii mikataba 17 imesainiwa ofisini, kuna mingine mingi inasainiwa mahotelini, kwenye baa, na kwingineko huko vichochoroni.
 
Ipo siku mtatuelewa tu sisi tuliojipambanuwa kupingana na serikali ya chama cha mwigulu(ccm)
 
Ndiyo mambo aliyoyakataa Mugabe
Yaani wazawa Zimbabwe walikuwa wanalima
kwenye mawe(udongo usio na rutuba) halafu
wawekezaji walikuwa wanalima ardhi yenye
rutuba.

Hii ni hatari kwa Tanzania
Hivi hao waliosaini hawakuona hatari kwa siku
zijazo yaani kuanzia 2014
Kweli Nchi imeuzwa kama wana JF walivyolalama

Hao wanaojiita wasomi sioni hata msaada wao
miaka 50 yaani kusiwepo Bandari tena nchini
hiyo ya Bagamoyo halafu wanaona sawa tu.

Nchi vitu vya kuwekwa wazi wanaficha
Kwanini Mkataba usiwekwe wazi nasi tuutolee
maoni ?

Hey bwana Kennedy ukisema sana watasema una wivu wa kike, huna malezi mema, una gubu, una hila, na kama ukizidi kuwasumbua saaaana watakwambia ulitangulia kutoka miguu badala ya kichwa, yaani huna hadabu.
Hahahahahaaaa usijali kaka nakutania tu ila kweli ulichokisema kina ukweli na ninakusapoti.
 
Last edited by a moderator:
Pengine bora hii mikataba 17 imesainiwa ofisini, kuna mingine mingi inasainiwa mahotelini, kwenye baa, na kwingineko huko vichochoroni.

Mzee ubora wa mkataba hautokani na sehemu uliposainiwa bali ni masharti yaliyomo na jinsi yatakavyotuumiza sisi na vizazi vyetu.
 
Reli nayo imezikwa rasmi!

Nitashangilia ikiwa katika mikataba hiyo kuna kuitengeneza reli ya Kati na kuiboresha ili iwe ya kisasa. Kwa hili litanifanya kwa mbali nifikirie fikirie kuwa bandali ya Bagamoyo ni sahihi kujengwa ili zisaidiane na ya Dar kuipatia reli ya Kati mizigo.
 
Back
Top Bottom