Msaada: Uvimbe wa wanawake kwenye kizazi

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
Hi Jamani, mambo vipi? Shost wangu kaambiwa anao uvimbe kwenye kizazi, ametumia dawa, hakuna majibu mazuri. Ameambiwa yalazimu operesheni.

Ila kuna tetesi kwamba akifanyiwa operesheni tu hatapata mtoto tena! kuna ukweli katika hilo? Je, wapi pazuri au daktari gani mzuri kwa operesheni za namana hiyo? Naomba kutoa hoja!!
 
ametumia dawa za kienyeji kwa miezi sita! alipocheck tena kakuta unaongezeka!
 
Dawa hata za hospitali ni za kutuliza tu dalili, yaani kupunguza maumivu na kupunguza wingi wa damu unaomtoka akiwa kwenye hedhi lakini haziwezi kuuondoa huo uvimbe, uvimbe unaondoka kwa operation tu.

Operation zipo za aina mbili, ya kutoa uvimbe na kuacha kizazi au kutoa pamoja na mfuko wa uzazi, hii ya pili hufanywa kwa watu ambao either hawataki kuzaa tena au wanauvimbe mkubwa sana kiasi kwamba hata ukitoa uvimbe peke yake ukaacha kizazi, kizazi kinachobaki hakifanyi kazi tena kwa hiyo hutolewa kizazi chote. Hii ya kutoa uvimbe haisababishi mwanamke kutozaa tena, wapo wengi ninaowafahamu ambao walitolewa uvimbe, kizazi kikaachwa na wakazaa tena zaidi ya mara moja.

Mwambie rafiki yako awahi hospitali, asiendekeze dawa za kienyeji, itakuwa too late akichelewa.

Sijui uko wapi lakini popote anapopatikana gynaecologist anaweza akakupa tiba muafaka. Tafadhali muone gynaecologist (daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama) na sio daktari yoyote, vivimbe hivi huhitaji utaalamu wa namna ya kuvitoa au kutibu.

Kila la kheri.
 
Mwambie ajaribu kuonana na DK Kaisi yupo Muhimbili ni dk mzuri sana wa kina mama
 
Dr Kaisi hapractice siku hizi, alipatata stroke, anafundisha tu. It is true he is among the best gynaecologist in the country. Any gynaecologist can help her, I dont want to mention names but I believe any gyanecologist can help.
 
Ohoo maskini sikuwa na habari hizi Mungu amsaidie Dk Kaisi
 
Amuone Dr Kapona, Dr Thomasi wapo Tumaini hospital. Kama kapotolo alivyoshaur aonane na dr wa masuala ya wanawake popote, tena vema kuwahi . Namtakia mafanikio.
 
uo uvimbe unaitwa fibroids ni common sana kwa wanawake weusi,wapo wanawake wengi wanapata watoto bila kuudistabu chakula chake kikubwa ni oestrogen mwanamke akiingi menopause uvimbe unanyauka .kuna ambao unaota ndani ya kizazi na mingiine nje ya kizazi.kuna docta mzuri sana mwanza anaitwa dr kilonzo alimsaidia ndugu yangu na amefanikiwa kupata watoto wawili.fibroids zake zilishindikana kutibika kwa madocta wengine wa dar akaelekezwa kwa dr kilonzo.sina contact zake ila kama kuna mtu yoyote unamjua wa mwanza atakusaidia kumsaidia rafiki yako good luck ........
 
Ahsanteni sana, ushauri wenu umekuwa na manufaa ajabu! nimempigia amesema anaenda Lugalo J3. Yuko Dar, na access ya Muhimbili nadhani sio rahisi kihivyo. Naamini hata Lugalo anaweza kupata msaada, ama sivyo?
 
Access ya Muhimbili ni rahisi sana kama ana uwezo wa kulipia huduma ya haraka (fast track), kama anaweza naweza kumpa contact ya daktari bingwa atakayeweza kumsaidia vizuri. Lugalo kuna gynaecologist yes lakini kwa raia kuna kaugumu kidogo labda kama ni mjeshi au ana mtu kule, otherwise kila la kheri.
 
uo uvimbe unaitwa fibroids ni common sana kwa wanawake weusi,wapo wanawake wengi wanapata watoto bila kuudistabu chakula chake kikubwa ni oestrogen mwanamke akiingi menopause uvimbe unanyauka .kuna ambao unaota ndani ya kizazi na mingiine nje ya kizazi.kuna docta mzuri sana mwanza anaitwa dr kilonzo alimsaidia ndugu yangu na amefanikiwa kupata watoto wawili.fibroids zake zilishindikana kutibika kwa madocta wengine wa dar akaelekezwa kwa dr kilonzo.sina contact zake ila kama kuna mtu yoyote unamjua wa mwanza atakusaidia kumsaidia rafiki yako good luck ........

hata mie namjua, nadhani huyu doctor ni maarufu sana hapa mwanza so akiwa mjini akimuulizia anampata, ht me nilimcndikizaga frend wangu hapo, clinic yake inajulikana kwa jina hilo hilo la doctor kilonzo
 
Nyie mnamzungumzia Kilonzo wa wakati huo. Kilonzo wa sasa si mzuri saana nadhani tamaa ya pesa imeingia. Hakuna hata haja ya kujaza majina hapa Daktari yoyote wa magonjwa ya wanawake atamsaidia
 
Access ya Muhimbili ni rahisi sana kama ana uwezo wa kulipia huduma ya haraka (fast track), kama anaweza naweza kumpa contact ya daktari bingwa atakayeweza kumsaidia vizuri. Lugalo kuna gynaecologist yes lakini kwa raia kuna kaugumu kidogo labda kama ni mjeshi au ana mtu kule, otherwise kila la kheri.

Kapotolo, shukrani za wazi kwako na kwa wengine wenye nia kama yako. Kwa kweli nashukuru sana. Nimeongea nae anasema uwezo wa fast track anao ila hajui pa kuanzia. Kama hutajali pls unaweza ukani-PM jina la daktari na jinsi ya kufanya ili aonane nae. Kwa mara nyingine nashukuru na nitaendelea kuwapa feedback accordingly.
 
samahani huu uvimbe unaongelewa hapa ndio 'Cyst" au ni vitu viwili tofauti?
 
aku

aende

LOLIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOONDOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Mwisho wa matatizo
 
nasisitiza kwa herufi kubwa, kuwa tatizo hilo naomba uende haraka hospitali kwa ajili ya operation hakuna njia tofauti na hiyo maana huo uvimbe unakuwa na size kuzidi hata ngumi ukipasuka ni hatari!!

Na matatizo hayo wengi wamesababishiwa na njia za kuzuiya mimba au lah, lkn mie nime-experience kwa wataalamu kama tuwaitavyo ma-gyno specialist wote maarufu mjini hata professor /dr mgaya wa muchs hakuna solution hapo!! Dawa ni kutuliza maumivu lkn usiende kokote utapote ndugu yangu muda na hali itakuwa tete!! Aende tu akaserve maisha yake! Nasisitiza hakuna dr. Atakayemshauri atumie dawa atapotoka! Nina mfano halisi so achana na maneno uende haraka!!
 
Back
Top Bottom