Msaada: Uvimbe wa wanawake kwenye kizazi

asanteni wote kwa ushauri leo nilimtembelea doctor wa wanawake na nikamweleza kila kitu akaniambia itakuwa appendex nimepatiwa dawa nimeambiwa nirudi next week.japo nashindwa kuelewa kama ni apendex kwanin niumie nikiwa period na nikimaliza tu
 
Naomba uende hospitali mapema sana ndugu. Hizo Diclopa hazitatui tatizo kabisa.
Nenda Masana hospital mbezi pale. Wakautoe huo uvimbe.
Mara nyingine ukichelewa sana huwa una develop kuwa cancer ya kizazi. Mungu aepushie mbali, ila uwahi wakautoe.
Hizo dawa za kichina haziyayushi huo uvimbe, ni biashara tu.
Ugua pole.

asante ndugu nitazingatia hilo
 
Dawa hata za hospitali ni za kutuliza tu dalili, yaani kupunguza maumivu na kupunguza wingi wa damu unaomtoka akiwa kwenye hedhi lakini haziwezi kuuondoa huo uvimbe, uvimbe unaondoka kwa operation tu.

Operation zipo za aina mbili, ya kutoa uvimbe na kuacha kizazi au kutoa pamoja na mfuko wa uzazi, hii ya pili hufanywa kwa watu ambao either hawataki kuzaa tena au wanauvimbe mkubwa sana kiasi kwamba hata ukitoa uvimbe peke yake ukaacha kizazi, kizazi kinachobaki hakifanyi kazi tena kwa hiyo hutolewa kizazi chote. Hii ya kutoa uvimbe haisababishi mwanamke kutozaa tena, wapo wengi ninaowafahamu ambao walitolewa uvimbe, kizazi kikaachwa na wakazaa tena zaidi ya mara moja.

Mwambie rafiki yako awahi hospitali, asiendekeze dawa za kienyeji, itakuwa too late akichelewa.

Sijui uko wapi lakini popote anapopatikana gynaecologist anaweza akakupa tiba muafaka. Tafadhali muone gynaecologist (daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama) na sio daktari yoyote, vivimbe hivi huhitaji utaalamu wa namna ya kuvitoa au kutibu.

Kila la kheri.
Kumbe kaka wale wanaosema saga tangawizi na vitunguu kunywa mwez kapime utakuta umeisha kumbe ni waongo.
 
Naomba uende hospitali mapema sana ndugu. Hizo Diclopa hazitatui tatizo kabisa.
Nenda Masana hospital mbezi pale. Wakautoe huo uvimbe.
Mara nyingine ukichelewa sana huwa una develop kuwa cancer ya kizazi. Mungu aepushie mbali, ila uwahi wakautoe.
Hizo dawa za kichina haziyayushi huo uvimbe, ni biashara tu.
Ugua pole.
Na wanavyojua kuuza bei kubwa sasa
 
Back
Top Bottom