Wataalamu wa afya msaada wenu kuhusu ugonjwa unanisumbua

Wegr

JF-Expert Member
Apr 27, 2022
224
579
Sitaki kuwachosha niende kwenye lengo moja kwa moja,

Ni wiki ya pili sasa napatwa na joto ikiambatana na baridi kali kichwa kuuma viungo vya mwili kuuma mda mwingine kuchoka hamu ya kula sina.

Nimeenda Hospital nimepima naambiwa sina ugonjwa wowote lakini hali ni taiti sana.

Msaada jamani kama kuna mwenzetu amepitia hali na amepona ametumia dawa gani!
 
Inawezekana ni corona...fanya kama tulivyokua tunafanya enzi za korona..kunywa panadol...piga antibayotike...kunywa maji mengi...
 
Yaani Mkuu nazipiga sana hizo antibiotic lakini zikiisha mwilini hali inarudi pale pale joto na baridi kali kichwa kuuma kwa mda mmoja, yawezakana ni corona maana kipindi kile sikuugua ili kuijua zaidi
 
HIV test umefanya?
 
Aisee ni nini hiko jamani...basi rudia kupima.malaria tena mkuu
 
Back
Top Bottom