Msaada Unahitajika: CPU ina beep (+Red Light) mara nne na haionyeshi kitu

Stavros Myles

JF-Expert Member
Jun 7, 2020
350
390
Hi kwa wanateknolojia wa Jf.Niende moja kwa moja kwenge tatizo lililonikumba. Betri (CMOS Battery) ndogo ya CPU ya Hp iliisha nikafanya mkakati wa kuisaka lakini nikiwa kwenye mchakato nikasema ngoja niiwasbe hii Deaktop hivhivi bila yakuwa na betri.

Nilifanikiwa kuitumia Desktop kwa siku mbili. Siku ya tatu wakati naiwasha niliskia sauti ya kitu kilichoungua (Paaaaa ) ikiambatana na harufu ya kitu kilichokuwa kinaungua, niliwahi kuzima kwenye Socket ya ukutani.


Siku iliyofuata nilijaribu kuiwasha tena, hapa niliambulia sauti ya mfululizo iliyokuwa inaruka sekunde moja then inapiga tena (tena ilikuwa inaambatana na rangi nyekundu kutoka kwenye LED). Sauti hii (Beeping sound) ilikuwa inatoka mara nne mfululizo then inaanza tena.


Nili google na kuingia kwenye support site ya hp, baada ya kuingia huko nilipata ufumbuzi wa muda mchache, mara ya kwanza nilijua shida uwenda ilikuwa ni RAM, baada ya kuitoa RAM na kusafisha slots za RAM na kuirudishia RAM mahali ilipokuwa tatizo liliendelea. Nilijaribu kuangalia processor kama ilikuwa imecheza lakini bado haikuwa hivyo. Nikaona bora nisafishe air vents za CPU, hata baada ya kutumia kitambaa kisafi kutoa/kufuta vumbi still tatizo lilibaki palepale.
Kitu pekee nilichokuja kukimalizia kuangalia ilikuwa ni sehemu ya power source, hii baada ya kuifungua sikufanikiwa kugundua shida yoyote kwani kila waya ulikuwa uko tightly held kwenda kwenye mahali ambapo ilitakiwa kuwepo nilifunga lakini tatizo bado liliendelea kuwepo.


Nilijaribu hata ku 'unplug' power source then nilibonyeza sehemu ya kuwashia CPU kwa sekunde 15 lakini mambo yalikuwa yale yale.

Leo nimejaribu kuiwasha tena mambo yamejirudia yale yale, ila kama bahati nimefanikiwa kuipata harufu yakitu ambacho kilikuwa kama kinaungua sehemu ya Power Supply. Sina assurance kwamba Power Supply inaweza kuwa imeungua kabisa au shida ni betri. Kama unaweza kunipa hints za signs za kuungua kwa Power Supply nitashukuru sana .


Nawasilisha.
IMG_20220304_143338_7.jpg
 
Chief-Mkwawa, nafikiria kutafuta Power supply mpya. Kwa hii iliyopo sidhani kam nitafanikiwa nayo. Kuhusu kuifunga vizuri nimeifunga vizuri, nakumbuka nilipo "doubt" ufungaji wa PSU niliifungua nakuicheki vizuri tena almost mara tatu.
 
Troubleshoot kimoja kimoja, hasa psu
Ila kama ulisikia mlio asilimia kubwa check capacitors kama kuna iloyopasuka, check capacitor zote za motherboard na za psu kama kuna iliyovimba.
 
Chief-Mkwawa, nafikiria kutafuta Power supply mpya. Kwa hii iliyopo sidhani kam nitafanikiwa nayo. Kuhusu kuifunga vizuri nimeifunga vizuri, nakumbuka nilipo "doubt" ufungaji wa PSU niliifungua nakuicheki vizuri tena almost mara tatu.
Sasa kama taa na sauti zinatoa utasemaje tatizo lipo kwenye power supply, Power Supply ingezingua ama kuunguza kitu chochote umeme usingepita kuingia kwenye mashine yaani usingeambulia chochote.
 
Back
Top Bottom