Msaada: Ugomvi wa rafiki yangu na mkewe

Msaada: Ugomvi wa rafiki yangu na mkewe

Sasa hivi ukigharamia elimu ya mwanamke utavuna dharau tu
^^
 
haa haaa labda ana mimba changa akampime. hizo harufu siku zote hajaziona?

Hilo la mimba hata mi nimehisi mwenzangu,na kama jibu ni ndiyo basi jamaa avumilie2 kwamda upepo utapita.
 
Kuna jamaa analalamika hapa kazini katoka nyumbani kakwazana na mkewe ambae mara nyingi hawaishi kukwazana na pia inavyoonekana mke kamchoka sana jamaa yetu ingawa jamaa anadai anampenda sana mkewe.

AnaDAI amemgharamia mambo mengi sana toka wanasoma na jamaa anadai kipindi bado wanasoma jamaa akiwa Mzumbe demu UDSM alikuwa akimsumbua sana na kuna siku alitoka chuoni akaenda kwa dsm kwa huyo mkewe akiwa na wazo la kwenda kumuua nae ajimalize bt alipofika akajawa na huruma na hofu maana jamaa ni mcha Mungu sana.

Sasa ya leo ni kwamba wameamka asubuhi na mkewe cha kushangaza mkewe anamwambia jamaa unanuka majasho jamaa akamuuliza unaposema mi nanuka jasho unamaana gani maana hata ww unatoa jasho mkewe kamjibu hili jasho ni la kiume mbaya.

Zaidi huyo mkewe akaanza kunusa baadhi ya mashuka mpaka yaliyofuliwa anasema eti yananuka kimsingi jamaa akajisikia vibaya sana kwanini mkewe anasema hivyo miaka yote wameishi huu ni mwaka wa 5 wanaishi mkewe hakuwahi tamka hayo.

Kweli huyu jamaa niko nae ofisi moja kusema kwamba hana harufu kali ya jasho hapana na ni msafi sana.

Ila jamaa anadai mkewe ni msaliti yaani ana cheat maana ni mwl.siku moja aliambiwa mkewe alikuwa anashikwashikwa kiuno na mkuu wa shule jirani wakati wakiwa kwenye sherehe na mkewe hakumkemea huyo mwl. mwenzie.

WAKUU NYIE MNALISEAJE HILI HASA HILI LA LEO LA JASHO KWANI JAMAA HANA AMANI NA ANAFIKIRIA KUACHANA NA MKEWE.

Bora tu asiwe anatoka kule kwenye wanakula kisusio atammalisa kweli!!
 
kakutana na mwenye jasho lenye harufu ya strawberry....
 
haa haaa labda ana mimba changa akampime. hizo harufu siku zote hajaziona?

Hilo linawezekana hasa,tatizo watu hawana vifua kaambiwa ananuka jasho kaenda kulalamika ofisini badala ya kutumia akili yake kidogo tu kujiuliza kwa nini harufu isikike leo?
Possible bidada ana ujauzito
 
hivi na wanawake wangekuwa wanafanya maamuzi kama ya kina munisi na mushi na kwa jinsi walivyo victims wakubwa katika mahusiano kungekuwa na mwanaume amebaki hapa duniani kweli?

Na soon kibao kitageuka tu,wanavyotuteketeza na kutudhalilisha kama wanawake wote ni wakosaji na wanaume wote ni malaika wanadhani hiyo manati ya mzungu inaachia risasi kwa kuangalia jinsia ya aliyeifyatua?
 
hivi, kuna mtu hapa Tanzania hanuki jasho? kumradhi ila hata boss wangu pamoja na pesa yote aliyonayo kikwapa ndo kiwapa! unakuta mtu kashikilia simu 3 (iphone, samsung, blacberry) lakini hata hafikirii kununua deodorant. kusema ukweli kikwapa hapa bongo ni janga la kitaifa!
 
Watu wengine wa ajabu kweli. kwani ukisema muhusika ni wewe tutagoma kutoa ushauri?
 
hizo tabia za ugomvi ugomvi huwa ni za wanawake WAFUPI... natanguliza Samahani zangu za Dhati.
 
hizo tabia za ugomvi ugomvi huwa ni za wanawake WAFUPI... natanguliza Samahani zangu za Dhati.

mkuu japokuwa umeomba radhi ila umekosea sana,kimo sio sababu ila ni hulka na tabia ya mtu.
 
Back
Top Bottom