msaada uendeshaji kituo cha yatima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada uendeshaji kituo cha yatima

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongoseke, Aug 11, 2012.

 1. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wa jamvi wenzangu natumai hamjambo,

  Ndugu zangu nina mpango wakuanzisha kituo cha kulea watoto yatima hapo nchini mungu akipenda baada ya miaka 2 ijayo ntapokuwa nimerudi rasmi kuishi home tz mpaka sasa nipo ughaibuni' nimekuwa nikiwaza jambo hili toka nkiwa na miaka 18 hivi na chanzo chake ni baada ya baba yangu kufariki nikiwa na miaka 15 tu huku nikiwa na wadogo zangu wa 5 ambao kweli walikuwa wadogo sana'na mimi ndio nlikuwa mkubwa,ukweli mama yetu ambae mimi anakuwa ni mama yangu wa kambo ambae alinilea mimi ndio tulibaki nae'hakuwa na kazi yyte na alikuwa hajui kabisa kazi'ilibidi nikiwa na umri ule nibebe jukumu zima la family nikiwa na 15yrs tu'

  Kwa kweli hapo ndio nlielewa maana ya yatima yale maisha tuliyoishi sisi mpaka leo huwa siyasahau'ndio maana leo naomba ushauri wa uendeshaji wakituo cha mayatima naimani hapa kuna watu wengi wanafaham jambo hili'
  Nafaham mtoto ana mahitaji mengi uangalizi,elimu,chakula na mengine mengi'
  Kifupi naombeni msaada kwa anaejua jinsi ya kuendesha kituo kama hicho anipe japo mwanga kidogo naweza kuanzia wapi'please hii sio seheme ya utani kwa hiyo mtu kama hana cha kuchangia ni bora apite kimya tu'
  NB: nategemea kufungua kwa kutumia pesa yangu wengine msije na mawazo kama nampango wakukusanya michango hapana nachohitaji ushauri tu natanguliza shukrani
   
 2. h

  hidekel Senior Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anzia wizara husika inayoendana na mambo ya ustawi wa jamii watakupa mwanga nini cha kufanya. ila tengeneza proposal yako, ikiwa ni pamoja na mambo mbalimbali unahitaji kuwa na bodi ya wadhamini -Trustee- (ninavyohisi). kwa mpango huo utakwenda mbele
  Asante
   
 3. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shukrani sana ndugu yangu naendelea kupokea maoni ya wadau wengine
   
 4. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Ebu tuwasiliane kupitia kitalolo@gmail.com tunaweza kushirikishana mawazo. Asante
   
 5. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shukran ndugu ntakutafuta
   
 6. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  nakupongeza kwa uwo moyo na wazo ilo,kuna mdau apo juu kakupa mawazo mazuri na amekujibu,sina la zaidi ni kukupongeza kwa uo moyo wa kusaidia
   
 7. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yah ndugu yangu kweli tuombeane dua tu
   
Loading...