Msaada tutani: naomba kupewa ufafanuzi kuhusu utofauti wa 'salio' na 'kiasi kilichopo' kwa watumiaji wa atm mashine

Socw

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
1,304
2,583
Wakuu, muda mfupi uliopita nimetoka kutoa pesa kwenye mashine ya atm ya nmb. Baada ya kuchukua pesa nikachukua na risiti pia. Kwenye ile risiti niliona kitu ambacho siku za nyuma sikukitilia maanani ila leo kilivuta makini yangu.
Salio lilikuwa limeandikwa na pia kiasi kilichopo kilikuwa kimeandikwa. Mkanganyiko nilioupata ni kuwa figure za 'salio' na 'kiasi kilichopo' zinatofautiana kama laki moja na 10 hivi, kwa maana ya kuwa kiasi kilichopo ni pungufu kwa laki moja na kumi kwa salio. Na kulingana na miamala niliyofanya nyuma kiasi cha salio ndicho sahihi. Wenye uelewa na haya mambo tafadhali, elimu inahitajika.

Natanguliza shukurani.
 
Kwenye ATM kama una 15,000, 5,000 tu ndio utakayoweza kuitoa, 10,000 iliyobaki haiwezi kutolewa.

Hiyo 5,000 ndio inaitwa salio na 15,000 ndio kiasi kilichopo
 
Yawezekana ni network tu ikitulia itakaa sawa,jaribu kuangalia tena,Halafu NMB si benki ya kutunzia akiba yako waja kulia kilio cha jibwa koko la mtaaa wa akina mwajuma nichokonoe!!
 
Kwa ATM nyingi za NMB 5000 huwa haitoki ndiyo, sasa kwa nini difference ifike laki moja ilhali laki moja inaweza kutoka?
 
Yawezekana ni network tu ikitulia itakaa sawa,jaribu kuangalia tena,Halafu NMB si benki ya kutunzia akiba yako waja kulia kilio cha jibwa koko la mtaaa wa akina mwajuma nichokonoe!!
Daaah aisee,nimetoa pesa ikanipa risiti ya mtu aliyepita na si risiti yangu....nikabaki nacheka tu.
 
Wakuu, leo tena nimeenda kutoa pesa kiasi kimepungua kutokea pale kwenye figure ya 'kiasi kilichopo' kwa lugha nyingine kuna laki kama na kumi hivi haijulikani ilipo. Nimepiga huduma kwa wateja naona sijibiwi wananisikilizisha matangazo tu.
 
Hata mimi iliwahi kutokea nikiwa Dar es Salaam kulikuwa na kama 200k+ kutoa 100k kwenye akaunti yangu ya benki ikaandika sina salio nilivuta subira jioni sikupata aidha hiyo tena. Kama unauhakika na pesa iliyomo wala usihofu pesa yako ipo salama na utaikuta
 
Nilichukulia poa, ila leo nimeenda kutoa nimekuta inazidi kupungua kutoka pale kiwango ambacho si sahihi. Nataka kesho mapema nikawaone aisee, 100k sio kitoto.
 
Suala lako sio la kawaida nenda kaonane na meneja wa benki yawezekana kuna mtu alitoa pesa kwa SIM banking mobile au benki
 
Back
Top Bottom