Babu nawe uzee utakuletea shida sasa, nilisema sababu kuu ni nimechoka. Kwenye mabano nikaweka visa vya pombe nilimaanisha alcohol na si the elected president.
Nataka kuachika kwa kuwa nimechoka sitaki tena kusuluhisha. Maana hayo nilishayafanya sana ila anarudia makosa yale yale yaani ni mfululizo wa visa.
Ngachokaa mbee na ndo hapo nataka nifanye kitu kimoja tuu yeye mwenyewe aseme sikutaki tena.
Mahakamani atanishinda na pesa zake after all hata akisema nguo zangu niache ntaacha maana sihitaji pesa yake wala mali yoyote niliyochuma nae wala mali niliyochuma kabla sijaolewa vyote namuachia. Nataka mwanangu tuu basi nikaanze upya.
Nikisema nimechoshwa na visa mjue nimechoka kwelikweli.....
Jeuri yake ya pesa inahusika vipi na mahusiano yenu?
Na mtu anakuchoka vipi sasa bila visa?
But anyway, here's the plan. Jaribu kuwa mlokole, unashinda kanisani kila siku. Siku ambazo yuko home, waalike wapendwa mnene zile scripted languages. Akivumilia hayo, baki tu. Good luck.
Natamani kujua ni visa gani hivyo umevichoka kiasi hiki mpaka unaomba kuachika,kweli pesa si kila kitu😢😢
Nilitaka kumwambia hivo na amesema hataki vikao wala nn najaribu kujiuliza hivi alitaftiwa huyu mme au la na jee hakumuona before kwamba n mlevi au vipi
We unataka uachike ili ukafanye umalaya vizuri.
Mbona umesahau nyepesi ambayo inawezekanika, usimpe unyumba ama kama hakupi unyumba kwa zaidi ya miezi kadhaa waweza tumia hilo kuomba talaka maana umechoka kuishi kama kaka na dada, ama mnyime akuchoke akuache.
kiongozi game ya home inautamu wake, akiamua jamaa hata na pesa zake atatulia....Jamaa anapesa asipopewa game anaenda kutafuta MAPAKA nje anajilia kiroho safi mkuu, agomee vingine lkn sio game
Hakuna kisa chochote,wanawake wengi wa sikuhiz sio wavumilivu tu,mimi kaka yangu alikuwa chapombe haswaaa kwa miaka kadhaa leo hii kaacha pombe na ana maendeleo haswa na Anampenda mke wake sanaa na kumsifia mara kwa mara kwani ndio kamfanya mpk akaacha pombe na bad companies.
Nakupenda dada mchungajiTeh movie hamna mpendwa, starring kafa hata kabla ya mpambano
Teh twajuana kwa vilemba yakhe
Nakupenda dada mchungaji
Ahsante mpendwa kwa upendo
Ahsante mpendwa kwa upendo
Yaani akaanzishe maisha yake mwenyewe halafu tena atambue kuwa haja achwa !!? Imekaaje hii mpendwaMkunde Original, uliapa kwa kinywa chako kuwa kifo ndio kiwatenganishe.., vinginevyo hakuna kuachika endeleza maisha kwa shida ama raha!
Vinginevyo sepa zako ukaanze maisha yako maana inaoneka hiyo ndoa ni zigo la misumari kwa upande wako.., japo huenda mumeo yeye ana amani ya kumtosha! Ila uwe unakumbuka kuwa hujaachika bado!!
Mkunde Jina lako linaniambia Wewe ni DaDa Yangu kikabila Ingawa Sitaki kuamini Hivyo.
Ingawa Sipo katika ndoa lakini kwa Hili nitajaribu kukushauri kwa Kiasi nijuavyo. Mapenzi au ndoa ni Ya mke na mume na Hata ikitokea mikwaruzano Hukaa na Kuijadili kisha Kutafuta Suluhu na Hatimaye kumaliza Ugomvi.
Kutaka Kujitawala bila kujua Athari Zake ni kukosa Maono Ya Mbele Uendako... Usiongee kwa kuwa upo na uwezo wa Hilo lakini angalia ni Athari Zipi ambazo zitampata mtoto kwa kukosa malezi Ya Baba?
Kusema Kuwa Huna Mchepuko na Wala Hata Ukiachwa Hutaanzisha Uhusiano mpya hapo ni Kujitetea tu lakini watu wenye Akili zetu tunaelewa kuwa yupo ambaye ameshakushika Sikio na Unataka Kuondoka Ili Ukajitawale Kwa Huyo Mtu..
Lakini Kumbuka Thamani ya mtu haipimwi kwa kulipa ovu kwa ovu bali kwa wema..
NDOA NI
UVUMILIVU
KUJALI
KUTHAMINI
KUHESHIMU.
Kuwa Muangalifu Dada Usije kuruka mkojo ukakanyaga Kinyesi.
Habari za jumapili waungwana,
Kimya kingi kina mshindo mwingi....... iko hivi nataka kuachika...... sababu nimechoka. (vituko vya pombe)
Vituko vimezidi nimekuwa nikiongea na tunayazungumza na mwenzangu ila anarudia yale yale. Nataka kusonga mbele niendelee na maisha maana kama kulia nimelia sana kama kuvumilia nimevumilia sana.
Msaada wako ni niambie nifanyaje au nitumie njia ipi niachike bila ugomvi bila mimi kuwa na mchepuko bila kumlipizia visa alivonifanyia. Pia sitaki kutoroka nataka nikiachika niondoke na mwanangu na si kuwa baada ya hapo ntaanza mahusiano mapya laah.
Nataka nijitawale mwenyewe nifanye yale nnayotaka na kumpa mwongozo mzuri mwanangu aje kuwa mtu mzuri baadae.Mwenzenu nimechoka nimechoka sitaki cha padri wala askofu wala maongezi ya familia wala kikao cha ukoo.
Naomba nisaidie ikiwezekana January nianze 2016 maisha mapya.
Ubarikiwe kwa maoni yako.
Unataka ujitawale!!!???
Mungu alimwambia Hawa.. "kwa tamaa zako siku zote utakuwa chini ya mme wako" wewe unataka kwenda wapi?