Msaada tafadhali, jinsi ya kuishi na "bp" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tafadhali, jinsi ya kuishi na "bp"

Discussion in 'JF Doctor' started by NGUGO, May 10, 2012.

 1. NGUGO

  NGUGO Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF salamu,
  kwa mara ya kwanza nimegundurika na tatizo la maradhi ya shinikizo la damu, dr aliponipima akasema nina kipimo cha 160/110 ambacho alisema ni kiwango cha hatari. SWALI:-
  1. Je! Ni vyakula na vinywaji gani havipaswi kuvitumia ukiwa na maradhi haya?.
  2. Ni mtindo gani wa maisha mwenye maradhi haya anapaswa kuishi?
  NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU KWENU WANA JF.
   
 2. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  polesana mkuu,wataalam wanakuja kukueleza
   
 3. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ndg Ngugo, swali lako ni zuri, kwa kusema kweli BP yako hiyo hiko juu! maswali yangu ni haya, je unalala vizuri na huna mawazo mengi? umewahi pima figo zako kuangalia kama una magonjwa? vipimo gani vya maabara umewahi pima au kama umepima biochemistry analysis unaweza weza ni PM nivione, nini kimekufanya uende kwa dr? unaumri gani? umewahi angalia sukari yako mwilini? je, kuna yoyote katika ndugu zako anaugonjwa huo? umewahi pima ECG au Echocardiography? hali yako ya macho unaionaje, unaweza mtafuta dr wa macho pia akuangalie. je, una uzito gani na urefu gani?
  kuhusu vyakula kula zaidi mboga za majani, matunda, maharage, samaki. usile vyakula vya mafuta hasa ya wanyama, nazi na ya pamba. fanya mazoezi ya kutembea angalu dk 20 kila siku. kuogele au hata mchakamchaka (jogging). usikae sana kuangalia tv, punguza uzito. achana na pombe au kunywa dry wine glass moja (angalia usiizoee sana). tumia dawa kama ulivyoagizwa na dr,(kamwe usipuuzie)
   
 4. NGUGO

  NGUGO Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikushukuru sana bwana Vicent, majibu ya maswali uliyouliza ni haya:-
  1. Umri 57 yrs
  2. Uzito 117 kgs
  3. Urefu 1.97 M
  4. Kazi ya ujenzi wa barabara- nafikiri ni mazoezi tosha.
  5. Kuwaza kupo, hasa ukiwa mtu wa majukumu kifamilia.
  6. Pombe, - Konyagi mix Cokacola,sio kulewa.
  7. Kisukari - sina.
  8. Macho - miwani ya kusomea.
  9. VIPIMO nilipima kwenye hospital ya wachina (TIENS) na kipimo cha ki-umeme kwenye kiganja wakaona matatizo :-
  a. Uti wa mgongo.
  b. Allergy ya ngozi.
  c. BP.
  d. Figo.
  e. Artteries.
  f. Macho.
  g. Nk.
   
 5. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nimekuelewa, hivyo vipimo vya kichina sivielewi, ila uzito wako ni mkubwa una BMI ya 30.15 kg/m[SUP]2 .
  [/SUP]kawaida inatakiwa kuwa 18.5 to 24.9kg/m[SUP]2 .
  [/SUP]Kazi yako si mazoezi tosha, usifikilie hivyo, yengekuwa mazoezi tosha basi uzito ungelipungua. konyagi na cocacola ni vinaongeza sukari mwilini, hasa cocacola na hivyo vinaweza sababisha pressure (hasa pombe ni njia moja wapo ya kusababisha pressure, kwani hufanya mishipa ya damu kusinyaa na kuongeza msuko wa damu katika mishipa na hata taratibu huharibu moyo, na baadae kupatwa na magonjwa ya moyo.
  ningekushauri upime vipimo hivi, halafu unitumie ili niweze kukupatia ushauri zaidi. s-creatinin,cholesterol, s-LDL, S-HDL, ALAT, ASAT, S-GT,S-GLUCOSE, URIC ACID, Albumin, ECG, URINALYSIS, TSH, T4,
  Na kama unavuta acha. baada ya vipimo hivyo twaweza ongea vizuri. pressure husababisha magonjwa ya moyo. figo kutofanya kazi vizuri na hata kupata kiharusi kama hutibiwi. kwa ushauri wangu kuwa mwangalifu. zingatia niliyo kuwaambia. kwa majibu yako hapo juu naona wew huijui hatari ya pressure. ukisikia watu wanaangunga ghafla na kuparalyse au kufa jua wengi chanzo ni pressure. chunga afya yako. lala mapema , baada ya kzi pumzika na fanya mazoezisi ya nguvu sana,
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu,
  Kwanza kabisa natumaini umri wako ni wa kijana kama nitakuwa sahihi.

  Pili, kabla ya kupata ushauri wowote ni lazima kwanza utambue nini chanzo cha High blood pressure. Hili litasaidi sana kujua nini ufanye na nini uache au pengine matatizo mengine yashughulikiwe. Mathalani, unaweza kuwa na tatizo la figo n.k. Suala la kipi ufanye linategema ufahamu zaidi wa chanzo kwanza.

  Kinachonishangaza ni kwamba huwezi kupima BP mara moja na kujihakikishia kuwa unayo. Inaweza kuwa BP ilikuwa juu kutokana na hofu tu uliyokuwa nayo kwa wakati fulani.
  Inaweza kuthibitika kuwa una BP pale kutakapokuwepo na vipimo vya kutosha katika nyakati tofauti

  Kwa hicho kipimo kimoja ni wazi kuwa diastolic ipo juu ya kiwango, japo systolic ipo juu lakini ujuu wake si wa kuogofya kama wa diastolic.

  Ushauri wangu: Kwanza jua chanzo,mtaalam wako aridhike na vipimo vya kutosha na si kimoja.
   
Loading...