Msaada - Taarifa za Muhimu juu ya Safari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada - Taarifa za Muhimu juu ya Safari

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mgombezi, Feb 21, 2012.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana Jamii...!!!

  Ninayo imani kubwa na jukwaa hili kutokana na manufaa mbalimbali tunayoyapata hasa katika kupata taarifa za muhimu zinazohusu shughuli zetu za kila siku.

  Wa-ndugu nipo katika maandalizi ya safari; kama ratiba yangu hapo chini inavyoonyesha:

  Siku 1 - Kuondoka Dodoma kuelekea Iringa kupitia Mtera (Tutalala Iringa)
  Siku 2 - Kuondoka Iringa kuelekea Makambako (Tutalala Makambako)

  Siku 3 - Kuondoka Makambako kuelekea Songea (Tutalala Songea)
  Siku 4 - Kuondoka Songea kuelekea Tunduru (Tutalala Tunduru)
  Siku 5 - Kuondoka Tunduru Kuelekea Masasi (Tutalala Masasi)
  Siku 6 - Kuondoka Masasi kuelekea Ikwiriri (Tutalala Ikwiriri)
  Siku 7 - Kuondoka Ikwiriri kuelekea Bagamoyo (Tutalala Bagamoyo)
  Siku 8 - Kuondoka Bagamoyo kuelekea Same (Tutalala Same)
  Siku 9 - Kuondoka Same kuelekea Arusha (Tutalala Arusha)
  Siku 10 - Kuondoka Arusha Kuelekea Tarangire National park (Tutalala Tarangire)
  Siku 11 - Kuondoka Tarangire kuelekea Babati (Tutalala Babati)
  Siku 12 - Kuondoka Babati kuelekea Dodoma via Kondoa (Mwisho)

  Vilevile naambatanisha ramani ya hii safari.

  Route.png

  Naomba taarifa zifuatazo:

  1. Hali ya barabara (mfano Dodoma Iringa na nyinginezo)
  2. Muda wa safari (mfano kutoka Dodoma kwenda Iringa na nyinginezo)
  3. Sehemu nzuri kwa chakula katika ya eneo moja na jingine (mfano kati ya Dodoma na Iringa)
  4. Vivutio ambavyo naweza kuona wakati wa safari (njiani) au katika miji nitakayopita.
  5. Nyumba ya kulala wageni au sehemu wanapofanya camping katika miji tutakayolala; gharama nafuu na yenye ubora. (Kama unaweza kunipatia Jina, namba ya simu au email)
  6. Na taarifa nyinginezo ambazo unaona zinaweza kunifaa katika maandalizi yangu.
  7. Nauli ya basi


  Naamini kila mmoja atachangia kwa sehemu ambayo atakuwa na uzoefu nayo. Natanguliza shukrani zangu kwa michango yenu.
   
 2. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wa-ndugu hamjawahi kusafiri kama mimi?????
   
 3. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wa-ndugu, kwani JF imegeuka kuwa FB; watu wanataka mambo ya mahusiano tu (mapenzi). Tunaanza kukosa msaada JF, siamini macho yangu. Watu 28 wame-visit hii thread, hakuna msaada wowote. Jamaani tumekuwa hivi....!!!!????
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ngoja mimi nivunje ukimya,
  Kutoka Dom mpaka Iringa ni mwendo wa masaa manne kama ni gari binafsi na hamna haraka sana,ni km 250 hivi. Cha maana utakachoona njiani ni nyumba za kiasili za wagogo maeneo ya Chipogolo, baadae utaweza kuliona bwawa la Mtera na kuvuka juu yake. Kwa kipindi hiki kuna uoto wa kijani njia nzima.

  Hakuna Hotel kwa kiwango chako,ila unaweza kupata chakula pale stand Mtera, kama mpenzi wa nyama choma utaipata Migori. Barabara ni ya vumbi Dom mpaka Iringa. Kingine utakachoona ni Uwanja wa ndege wa Nduli na shamba la ng`ombe wa maziwa.Ukishavuka Mtera, basi utakuwa uko chini ya himaya ya Lukuvi.

  Angalizo, mitaa ya kati hapo usile ovyo,waweza pata tumbo baya ghafla. Karibu Iringa, vipi nikuchagulie mahali salama pa kulala?
   
 5. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Malila; taarifa nzuri sana. Naomba kuuliza, hivi kutoka Iringa mpaka Makambako inaweza kuwa masaa 4, maana nilisafiri hiyo njia muda kidogo. Halafu unaweza kuniambia gharama ya guest house hapo Iringa (Double room).
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni masaa mawili na nusu mpaka matatu kwa mwendo wa kitalii kama mna gari yenu. Tahadhari Iringa mjini usiku kuna tatizo la misosi baada ya saa nne usiku. Baada ya muda huo itabidi mwende ktk mahotel ya gharama kubwa zaidi, au mkale nyama choma pale Miami, lakini kuna walevi kiasi. Sehemu nzuri ya chakula kwa pale ktkt ya mji ni Staff Inn, wana chakula kizuri au MR Hotel iko karibu na stand ya mabasi.

  Gharama za G/House zinategemea jinsi ww ulivyo,labda kama unataka mambo makubwa au ya kawaida. Lakini kwa nyumba nzuri zenye usalama, andaa kt ya 15,000/ mpaka 25,000/ kwa double yenye ukisasa. Iko moja pale karibu na Stand, ina parking ya magari ndani ya fence, kwa sababu hamna haraka, basi pale patawafaa. Pale no totoz, no maji ya mende,na car park ya uhakika kama hupendi makuu.

  Mara nyingi tunalala pale kwa sababu ya usafi na usalama.
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi Malila ulishafika pale Miami siku za karibuni? Wale vijana wamejitahidi sana kufanya renovation, na huduma zao ni za kuridhisha mno kwa mtu wa kawaida ila kwa mtu asiyependa ulevi/walevi pale patamkwaza sana. Na pale Babanusa kwa mambo ya misosi si 24/7? Ila kama jamaa wanataka ukisasa zaidi hapatawafaa, kwani watu wa kima cha chini ni wengi sana. Nadhani wakishindwa kote huko waende SAJUS kwa Mama Pindi Chana, pale mpaka saa sita usiku utapata huduma.

  Na hiyo nyumba ya kulala wageni unamaanisha MR Hotel? Kusema ukweli jamaa wanajitahidi but hata Kalenga ni nzuri pia but tatizo lao ni parking. Kuhusu Makambako, kuna hotel fulani ipo mwanzoni kabisa, baada ya kukata kona ya kwenda Njombe (upande wa kulia) inaitwa Midland, huduma zao ni nzuri sana na bei ni reasonable kabisa, vilevile kuna Gold Tower upande wa kushoto, ila kama jamaa wanataka ukisasa zaidi waende DURBAN HOTEL ni nzuri sana kwa maeneo yale
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Babanusa ni pazuri kabla ya saa saba mchana, baada ya hapo kwa mtu uliyepanga safari vizuri hapafai kabisa, unaweza piga kiporo. Kando ya Babanusa ndio wapo Staff Inn. Ukiingia chooni kwa akina Babanusa ndio utajua kwa nini sipafagilii kwa mtu anayetaka kula kuku kwa mrija.

  Nyumba ya Wageni ni WIHANZI GUEST HOUSE ipo upande wa chini kutoka stand kuu kama unaenda Frelimo, ila hawana chakula pale. Usalama ni bomba, asubuhi kama unasafiri kwa basi unasindikizwa na mlinzi wao mpaka stand.Mgombezi inabidi uandae meno, Iringa kuna mahindi ya kuchoma live.

  Nakubaliana na wewe kwa habari ya Makambako,nilishalala pale siku moja mwaka jana. Kipindi hiki ni kizuri hakuna baridi.Ukifika Njombe mwanzoni kabisa baada ya kupita Polisi, upande wa kulia, nunua NUMBU za kutafuna. Wauzaji wameshaziosha tayari kwa kuliwa.
   
 9. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Malila; ngoja niendelee kupata taarifa nyinginezo, nikiona burget inaruhusu basi tutawasiliana.
   
 10. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu Entrepreneur; Asante sana kwa taarifa nzuri, nitaendelea kuheshimu jukwaa hili. Vipi kuhusu gharama za malazi na hapo inakaribia 15,000/= - 25,000/= kwa double room?. Vipi kuna guest ya bei nafuu zaidi ya hapo na inafaa kwa kulala, maana ukiangalia safari yangu kila mahali nitalala usiku mmoja tu.

  Vipi kati ya Iringa na Makambako, kuna kivutio kinginecho zaidi ya zile nguzo za umeme zilizopisha makaburi (nimesahau hilo eneo).
   
 11. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu Malila; unaweza kunisaidia jina la kisayansi la huyo ndege/mnyama, ili niweze ku-google na kupata picha yake.
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Pole Mkuu, hicho kivutio cha makaburi na nguzo hutakiona tena kwani makaburi yalihamishwa kupisha upanuzi wa barabara. Na kwa budget hiyo uliyonayo hapo Midland patakuwa muafaka zaidi.

  Kivutio kikubwa utakachokutana nacho (Iringa to Makambako) hasa baada ya kutoka Mafinga, ni misitu minene ya miti inayozalisha mabao laini na makaratasi
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Vivutio viko vingi sana,ukitoka Iringa mjini kwenda Makambako utaiona fly-over ya kwanza ktk kilima cha kushukia Ipogoro ambayo magari yanapita juu na watu chini.

  Kivutio cha pili ni masalio ya JKT pale Mafinga kama utataka kwenda kuyaona !!!!!!! Kivutio kingine ni misitu ya pines ( Pinus patula) iliyopamba barabara toka Mafinga mpaka Nyololo. Ukifika Nyololo,jiandae kula mishikaki ya samaki toka Igowole ( usile njiani ovyo). Kabla hujaingia Makambako utapita fly-over ya pili ambayo magari yanapita juu na train chini.

  Kivutio kingine utakachokiona njiani ni juisi malidhawa ya Ulanzi, hasa ukifika mitaa ya Tanangozi,Ihemi. Ulanzi hauchemshwi,usinywe ili ratiba yako ya safari isibadilike. Kutoka makambako kwenda Njombe mpaka songea ni mkeka safi.
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu si ndege wala mnyama,ni mmea jamii ya beatroot, isipokuwa zenyewe ni nyeupe na zina maji mengi sana, zinalimwa kama carrots. Ukila nyingi kidogo zinafanya meno kugeuka rangi hasa ukila mbichi. Zilizopikwa ni bomba zaidi. Ukiweza kumpata Fidel wa humu jamvini au Next level wanaweza kukupa jina la kisayansi. Mimi huwa nazipiga sana nikifika Njombe,hadi nasahau chakula kingine.
   
 15. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante sana Mkuu.
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asanta sana mkuu; natumaini FIDEL au NEXT LEVEL watapita na kutusaidia jina la kisayansi.
   
 17. Kayoka

  Kayoka JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,427
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  kwa Songea karibu sana mkuu. Ukifika unaweza kulala Top one pale msamala chumba elfu 30 (chukua tahadhali na vitasa vya mlango huwa mara nyingi vimetobolewa katundu for chaboringing). Toka songea mpaka tunduru ni barabara ya vungu na it take 8-10hrs hasa hii masika.
  Kwa vivutio songea waweza kwenda ukumbi wa mashujaa ambapo wale majimaji heroes taarifa zao zipo pale.
   
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hata kama hutakuwa na muda wa kukaa sana huko,ni vizuri ukijua salamu zao, kuanzia Mtera mpaka Makambako unaweza kutumia neno kamwene kama salaamu kwa ye yote. Ukifika makambako/njombe utakutana na salaamu tofauti tofauti kama vile mapembelo, kamwene,ughonile,nk.
   
 19. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu Malila, ubarikiwe sana; yaani unanifanya nitamani kuanza safari hata kesho. Hizi dondoo kwangu ni muhimu sana, wenzetu wanapotaka kusafiri huwa wanakwenda hapa....www.tripadvisor.com, ambapo unapata uzoefu kwa waliosafiri.
   
 20. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu Kayoka; nimecheka sana kuhusu hiyo tahadhali, lakini haya ndiyo mambo ya msingi tunapaswa kufahamu kabla ya kwenda sehemu ambayo hujawahi kufika. Vipi kutoka makambako hadi Songea, inachukua muda gani. Vile vile ningependa kufahamu nauli za mabasi ili niweze kuwa na uchaguzi, kati ya kutumia usafiri binafsi au mabasi.
   
Loading...