Msaada swali la hisabati

Njia.
Fikiria Y iwe ni jumla ya Kg za mchele alizo kuwa nazo Alpha

Mchele alio kula=1/4 ya Y=1/4xY=1/4Y

Mchele alio uza=1/3 ya mchele uliobaki
Lakini Mchele uliobaki baada ya kula=Jumla ya mchele-Mchele alio kula =Y-1/4Y=3/4Y
Kwa hiyo,
Mchele alio uza=1/3 ya 3/4Y =1/3x3/4Y
Mchele aliouza= (1x3)/(3x4)Y=3/12Y=1/4Y

Jumla ya mchele wote=Mchele alio kula+Mchele alio uza + Mchele alio baki nao
Y=1/4Y+1/4Y+60
Zidisha na 4 kila upande
4Y=Y+Y+240
4Y=2Y+240
4Y-2Y=240
2Y=240
Y=120

Kwa hiyo Alpha alikua na Kg 120 za mchele
✔ very good, keep it up
 
Dah! Hi corona hii, nilikuwa napitiapitia solution humu kama daftari za wanafunzi wangu vile nisije nikasahau kuweka tiki na kosa. Mpo vizuri, niliowaambia wanione nitawapa zawadi.
 
kivipi? Embu onyesha
twende sawa...

assume mchele wote jumla ni kg X. SO,
jamaa alikula robo ya mchele wote (x/4)
jamaa akauza theluthi ya mchele wote (x/3)
jamaa akabakiwa na kg 60 kwenye stock, therefore,

ukichukua jumla ya mchele wote (X) utoe aliokula (x/4) na aliouza (x/3) unabakiwa na 60kg
X-(x/4 + x/3)=60
x-7/12x=60
12x-7x=720
5x=720
x=144.

sasa alikula robo ya x (144)
1/4*144=36kg

aliuza theluthi ya x (144)
1/3*144=48.
alibakiwa na 60kg.

proof.

144-36-48=60
144-84=60
60=60 hence prooved.
 
Mkuu kumbuka alpha alikula 1/3 ya mchele ULIOBAKI sio 1/3 ya mchele WOTE. Kama angetuambia amekula 1/3 ya mchele wote ndo tungefanya kama ulivyofanya, na kwa hatua hii ndo TRICK PART ya hesabu ilipo. Kwa hesabu zako kama mchele wote ni X na aliokula ni x/4 basi uliobaki ni X-X/4 ambao jamaa ameuza hapo 1/3.
 
dah, ndio mana hua tunafeli yaani swali jepesi nimekosa kizembe sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom