Tunda la katikati lilikuwa ni lipi?

Tunda la katikati lilikuwa ni lipi?

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,042
Natanguliza samahani kama kuna watakao kwazika kwa hili swali langu ila ningeomba kupata ufananuzi kwa wanao jua.

Hivi lile tunda la katika lililokatazwa kwenye bustani ya Eden lilikuwa ni lipi?

Mana zipo hoja kwamba tunda lile ilikuwa ni Tendo la ndoa (ngono) na kama imani hiyo ni ya kweli je Eva alafanya na nani ? Mana maandiko yanasema Eva alikula lile Tunda kwanza na kisha Adam aliporudi akampa nayeye akala.!!

Sasa kama ni hivo, je ni kweli kwamba Eva /Hawa alifanya mapenzi na shetani kwanza kisha ndo akaja kufanya na Adam??

Naombeni kujua.
 
Kwenye Biblia hakuna mahali kuna kitu kinaitwa "Tunda la kati"

Bali ndani ya Bustani kulikuwa kuna miti mingi lakini katikati ya bustani (In the midst) kulikuwa na aina mbili pekee za miti,ambayo mmoja ulikuwa ukifahamika kama mti wa matunda ya Uzima,mti huu Mungu alimwambia Adam na mkewe wanaweza kula matunda yake wakati wote lakini pia kulikuwa na mti uliofahamika kama mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao tangu awali Mungu alimwbia Adam na mkewe Hawa wasije wakaugusa mti huo wala wasije wakayala matunda ya mti huo,Kwasababu siku watakapo ugusa au kuyala matunda ya mti huo,basi watakufa hakika!

Matunda aliyokula Hawa na Mumewe Adam yalikuwa ni matunda kutoka katika mti huo wa Ujuzi wa mema na mabaya!

Yalikuwa ni matunda halisi wala si ngonjera za wafuga minyoo kwa kudhani kwamba kulikuwa na fumbo la kwamba lilikuwa ni Tendo la ndoa!,La hasha yalikuwa ni matunda halisi!
 
Bali ndani ya Bustani kulikuwa kuna miti miwili iliyokuwa katikati ya Bustani (in the midst)ambayo ulikuwa mti wa matunda ya Uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo tangu awali Mungu aliwaambia wasije wakaugusa mti huo wala wasije wakayala matunda yake!

Matunda aliyokula Hawa na Mumwe Adam yalikuwa ni matunda kutoka katika mti huo wa Ujuzi wa mema na mabaya!
Uzi ufungwe 🫡
 
Inafikirisha!
Lakini fahamu,siyo tendo la ndoa.
Hii ni kwa sababu Mungu alishawapa ruhusa kufanya tendo la ndoa (hata kama hapakutajwa)-Mwanzo2:21-24
Làkini haiwezi kuwa uzinzi pia kwa sababu walikuwa wawili pekee yao.
Uzinzi ni tendo la Mme au Mke alie katika ndoa kuchepuka.
Lakini ngoja tusubiri Wana theolojia watuambie kwa sababu nasikia hayo mambo yametajwa "kwa lugha ya Picha"! Yanamaanisha na kuwakilisha kitu kingine.
 
Natanguliza samahani kama kuna watakao kwazika kwa hili swali langu ila ningeomba kupata ufananuzi kwa wanao jua.

Hivi lile tunda la katika lililokatazwa kwenye bustani ya Eden lilikuwa ni lipi?

Mana zipo hoja kwamba tunda lile ilikuwa ni Tendo la ndoa (ngono) na kama imani hiyo ni ya kweli je Eva alafanya na nani ? Mana maandiko yanasema Eva alikula lile Tunda kwanza na kisha Adam aliporudi akampa nayeye akala.!!

Sasa kama ni hivo, je ni kweli kwamba Eva /Hawa alifanya mapenzi na shetani kwanza kisha ndo akaja kufanya na Adam??

Naombeni kujua.
Swali zuri.
Tunda lililoongelewa ni TUNDA kama tunda na siyo tendo la ndoa, achana na huo upotoshaji wa siku hizi wa kihuni.
 
Biblia ina mambo matatu;
1. Mawazo huru ya watu waliojaribu kujibu swali la asili ya ulinwengu na vilivyomo, kifo na maisha baada ya kifo (falsafa huru)
2. Stori za kweli za watu wa kale, waliyoyafanya na waliyofanyiwa na asili, stori hizi zina ujumbe flani kwa maisha ya kale, sasa na yajayo.
3. Hekima za watu mbali mbali kama suleiman zenye mafunzo wakati huo, sasa na baadae.

Mambo ya tunda, mbingu, asali, maziwa ni falsasa kwenye lugha ya picha ili kumuelewesha mtu mwenye akili finyu labda ataelewa kitu flani kuhusu maisha. Msiwe hivyo.
 
Ukiangalia vizuri mwanzo kabisa, Mungu aliwaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi. Sasa wasingeweza kuzaana bila kufanya tendo la ndoa, hiyo maana yake sex was part of the plan tangu day one, na haikuwa dhambi hata kidogo. Tunda lilikuwa na maana nyingine kabisa.
 
Natanguliza samahani kama kuna watakao kwazika kwa hili swali langu ila ningeomba kupata ufananuzi kwa wanao jua.

Hivi lile tunda la katika lililokatazwa kwenye bustani ya Eden lilikuwa ni lipi?

Mana zipo hoja kwamba tunda lile ilikuwa ni Tendo la ndoa (ngono) na kama imani hiyo ni ya kweli je Eva alafanya na nani ? Mana maandiko yanasema Eva alikula lile Tunda kwanza na kisha Adam aliporudi akampa nayeye akala.!!

Sasa kama ni hivo, je ni kweli kwamba Eva /Hawa alifanya mapenzi na shetani kwanza kisha ndo akaja kufanya na Adam??

Naombeni kujua.
Maku
 
Sio Tunda la katikati Bali mti wa katikati. Sahisha hilo kwanza. Halafu usipende kuwaza ngono Kila wakati.
 
Kwenye Biblia hakuna mahali kuna kitu kinaitwa "Tunda la kati"

Bali ndani ya Bustani kulikuwa kuna miti mingi lakini katikati ya bustani (In the midst) kulikuwa na aina mbili pekee za miti,ambayo mmoja ulikuwa ukifahamika kama mti wa matunda ya Uzima,mti huu Mungu alimwambia Adam na mkewe wanaweza kula matunda yake wakati wote lakini pia kulikuwa na mti uliofahamika kama mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao tangu awali Mungu alimwbia Adam na mkewe Hawa wasije wakaugusa mti huo wala wasije wakayala matunda ya mti huo,Kwasababu siku watakapo ugusa au kuyala matunda ya mti huo,basi watakufa hakika!

Matunda aliyokula Hawa na Mumewe Adam yalikuwa ni matunda kutoka katika mti huo wa Ujuzi wa mema na mabaya!

Yalikuwa ni matunda halisi wala si ngonjera za wafuga minyoo kwa kudhani kwamba kulikuwa na fumbo la kwamba lilikuwa ni Tendo la ndoa!,La hasha yalikuwa ni matunda halisi!
Una uhakika gani yalikuwa ni matunda halisi??
 
Kulingana na maelezo ya Biblia wakiwa ndani ya Bustani,Matunda yametajwa!

Waliambiwa wale matunda ya miti yote ya iliyokuwa ndani ya Bustani isipokuwa matunda ya mti wa Ujuzi wa Mema na mabaya!

Neno "Kula" ,wewe kwa akili yako kinacholiwa huwa ni halisi au si halisi?
 
Back
Top Bottom