Msaada: Shule ya Serikali nzuri ( Kwa O - Level) ni ipi?

ntule

Senior Member
Feb 18, 2014
105
29
Wadau wa Jf ,nina mtoto wa kike kamaliza darasa la saba , sasa wamempaga shule ya kata ,shule yenyewe haifanyi vizur kabisa,na mtoto wangu uwezo wake ni mzuri kiasi ,amepata wastan wa B ,kwa maana ya
Eglish A
Kiswahili A
Hisabati B
Sayansi C
Study's c
Kwa matokeo hayo natamani nipate shule ya govement ya bonding na iwe ya girls. Ambayo ni nzuri ,napendekza mikoa minne ,singida ,arusha, moshi, na manyara ,au dodoma pia ,mm nipo manyara ,babati mjini,

Nisaidie kujua shule nzuri na kuweza kumpeleka mtoto ,maana hata yeye anasema baba mm nataka kusoma sana lakin nitafutie shule nzuri ya bonding, shule aliye chaguliwa ni ya day ,kata, Asante mwenye kufahamu shule nzuri anisaidie jina la shule ,kama unamawasiliano ya shule husika pia nitashukuru sana ,
 
Hawezi kutoka day aingie boarding na sio bonding ndg, sheria hiyo imekuwepo muda mrefu sasa kwa government labda apate shule day lakini zina hostel .vinginevyo mpeleke za binafsi private japo kupata nzuri muda huu umeshachelewa sana
 
Hata moro kuna shule nzuri sana za binafsi kama unataka mwanao afanye vizuri hangaika kupata hizo kuna shule inaitwa Lamirium girls wanaufaulu mzuri sana ila kusoma awe na bidii asipofikia wastani wao watamtoa tu
 
Shule nzuri za Serikali ni:
I/ Vipaji Maalum kama Tabora girls, Weruweru etc
2/ Shule za Ufundi kama Tanga, Moshi etc
3/ Za Bweni kama Songea na Korogwe girls etc
Ila bahati mbaya wote hao wamechukuwa wastani wa "A" hivyo ili upate nafasi ni lazima uvae Shati la Mikono Mirefu!
 
Hawezi kutoka day aingie boarding na sio bonding ndg, sheria hiyo imekuwepo muda mrefu sasa kwa government labda apate shule day lakini zina hostel .vinginevyo mpeleke za binafsi private japo kupata nzuri muda huu umeshachelewa sana
Kwani pravate nazo huwa zinajaa ,au ni hela yangu tu??
 
Shule nzuri za Serikali ni:
I/ Vipaji Maalum kama Tabora girls, Weruweru etc
2/ Shule za Ufundi kama Tanga, Moshi etc
3/ Za Bweni kama Songea na Korogwe girls etc
Ila bahati mbaya wote hao wamechukuwa wastani wa "A" hivyo ili upate nafasi ni lazima uvae Shati la Mikono Mirefu!
Asnte nimekuelewaa mkuu
 
Zile nzuri zinajaa kuna kiwango maalum cha idadi ya wanafunzi kwa darasa na wakaguzi wa elimu hupita kukagua ukikiuka unafungiwa shule labda uwe streams nyingi ili uwe na wanafunzi wengi ila ndio ufaulu unakuja kuwa hafifu waalim hawatoshi
 
Mi nakuomba usipoteze muda wa mtoto wakati unatafuta aendelee kusoma alikopangiwa ila kupata serikalini boarding ilikuwa zamani muundo ulishabadilika na sasa hivi hakuna asiyetetea kitumbua chake kila mtu ni muoga ndg yangu kutumbuliwa nakushauri ukaombe apate shule ya kutwa yenye hostel ila kama ni mapepe jinyime mpeleke hizo za kulala shuleni boarding private
 
Shule zote za bweni za serikali wamechukua pure/cream kabisa yaani wenye wastani wa A...kama unataka mwanao asome vizuri adjust bajeti yako mpeleke private...kwa hapo kwako Manyara uanweza mpeleka hapo St.Pio Kibaigwa ni wazuri na Ada zao zipo chini sana.
 
Wadau wa Jf ,nina mtoto wa kike kamaliza darasa la saba , sasa wamempaga shule ya kata ,shule yenyewe haifanyi vizur kabisa,na mtoto wangu uwezo wake ni mzuri kiasi ,amepata wastan wa B ,kwa maana ya
Eglish A
Kiswahili A
Hisabati B
Sayansi C
Study's c
Kwa matokeo hayo natamani nipate shule ya govement ya bonding na iwe ya girls. Ambayo ni nzuri ,napendekza mikoa minne ,singida ,arusha, moshi, na manyara ,au dodoma pia ,mm nipo manyara ,babati mjini,

Nisaidie kujua shule nzuri na kuweza kumpeleka mtoto ,maana hata yeye anasema baba mm nataka kusoma sana lakin nitafutie shule nzuri ya bonding, shule aliye chaguliwa ni ya day ,kata, Asante mwenye kufahamu shule nzuri anisaidie jina la shule ,kama unamawasiliano ya shule husika pia nitashukuru sana ,
Moshi sio mkoa,inaonekana mzazi mwenyew chenga mno.
 
Shule nzuri za Serikali ni:
I/ Vipaji Maalum kama Tabora girls, Weruweru etc
2/ Shule za Ufundi kama Tanga, Moshi etc
3/ Za Bweni kama Songea na Korogwe girls etc
Ila bahati mbaya wote hao wamechukuwa wastani wa "A" hivyo ili upate nafasi ni lazima uvae Shati la Mikono Mirefu!
Weruweru sio vipaji maalumu...za vipaji ni tabora girls,kilakala na msalato plus na kisimiri though ni mixture
 
YA SERIKALI BORDING O LEVEL MIKOA MINGINE HAKUNA ILA IPO MOJA TU CHUNYU WILAYA YA MPWAPWA MKOANI DODOMA NI PAZURI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom