Msaada: Safari yangu ya Zambia.

Msaada: Safari yangu ya Zambia.

kitumbotala

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
516
Reaction score
625
Habari ndugu zangu, mwezi wa sita natarajia kuelekea Zambia, natokea Dar es salaam naomba kujulishwa mambo yafuatayo kwa waliowahi kwenda huko.

1. Gharama za usafiri wa Bus Dsm to Zambia
2. Hali ya usalama huko
3. Mahala salama pa kufikia hapo Lusaka (lodge or guest house nzuri standard)
3. Umbali wa kutokea New Kapilimposhi mpaka Lusaka.

Asanteni na karibuni.
 
Mkuu, maisha ya Lusaka hayana tofauti na Dar. Wewe chukua zako bus (ukienda Ubungo Terminal utapata kiasi cha nauli) ukifika Lusaka ulizia tu mtu yeyote utaoneshwa malodge na magesti kibao tu - Manzese-type and the like yako mengi tu. Life ni ya kawaida sana huko.
 
Dar-Tunduma ni 40,000tshs Tunduma-Lusaka nauli inacheza kwenye 200kwacha ambayo haipungui 45,000 za kitanzania ..

Lodging in Lusaka ni gharama kubwa sana tofauti na Dar,....Hio distance ya kapili mposhi we ingia google tu msee
 
Pale border na Tunduma si panaitwa Nakonde? Nakumbuka tulitokaga saa Moja na nusu usiku pale border tukaingia Lusaka saa kumi na mbili asubuhi,askari wanachelewesha mabus kwa ajili ya kuyasachi
Nalog off
 
Nakonde pale kuna mama mmoja tulikutana mwaka
2012 anamiliki supermarket.
 
Kwa kuwa ni mgeni panda Taqwa au Falcon yanayoelekea Zimbabwe yanapita Lusaka nauli ni 90,000 mpaka 80,000 wanakubali ila yanafika usiku sana Tunduma mnalala hapo asubuhi unaendelea na safari hakikisha una kadi ya chanjo wazambia kwenye kugonga passport wanasumbua kama hauna uwape rushwa na sasa hivi safari za bus Zambia ni mchana jioni ya saa kumi na Mbili utakua umefika Lusaka.Wewe una budget ya hotel kiasi gani kwa siku maana kuna blue water ipo njia ya Chawama,Town hapo intercity zipo kama tano hivi Mbili za bei ghari tatu bei ya kawaida ila sio sawa na Dar kwa Nchi za kusini Zambia Hotel zipo juu sana na pia kama kwenda uende na dollar harafu uongee na konda wa bus umpe kama laki au laki Mbili yeye ndio abadilishe hapo Tunduma kwa mgeni watakuchanganyia mahesabu watakuibia tuu wengi wa dasalama wanaibiwa hapo ukiwa mgeni all in all Lusaka gharama za chakula na Tax ni kama bongo tuu...35,000 Zambian Kwatcha Nsima(ugali) na Samaki (Nsomba) Mkubwa...
 
Mkuu inaonenekana unajua meng.

Vipi kuhusu fursa zinazopatikana?

Hivi hyo kadi ya chanjo ni utaratibu gani unatumika kuipata!?

vipi kuhusu maisha ya huko kiujumla!?

gharama za passport?

Vigezo gani vinazingatiwa kupata passport?
 
Fursa mojawapo ni pombe au kilevi kwakwenda mbele
Sidhani kama kuna mzambia ambaye hanywi pombe,aisee Hawa jamaa ni walevi kuliko maelezo! Wanapenda kutembea na six pack,yaani Moja anaiywa tano zilizobakia zipo kwapani utaopoa sana kwa style usimnunulie bia Moja moja hawapendi,ukimpiga na six pack unaonekana Wa maana
Nalog off
 
Back
Top Bottom