Msaada plz matatizo ya macho (upofu)

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
148
Wadau, habari za leo.

Mimi niko mikoani, nina shemeji yangu (dada wa mke wangu) ana binti yake kule Lushoto. Huyo binti imefikia hatua ya kuachishwa shule kwa sababu ya upofu. Mwanzoni alikuwa anaona japo kwa shida ila taratibu kadiri muda ulivyokuwa unaenda akawa haoni na imefikia hatua hata akitaka kwenda kujisaidia anapelekwa kwa kushikwa mkono. Amefanya kila jitihada kumpeleka kule Irente nasikia kuna hospitali akapimwa macho akapewa miwani lakini haikusaidia chochote. Huyo shemeji yangu kwa kweli ukizingatia hawakuenda shule ndo hivyo tena hawana hata exposure yoyote ya kumsaidia mtoto wao, nimewauliza ni kama wamejikatia tamaa tuu.

Naomba wenye uelewa wa jinsi ya kutatua hili tatizo nipeni mawazo wadau, kama kuna sehemu naweza kwenda nikapata msaada, hivi najiandaa kifedha nijitolee nimpeleke popote atakapopata msaada hata kama ni Dar, ila naomba nielekezwe nini cha kufanya. Inaniuma sana binti ameacha shule na hana future tena zaidi ya kukaa ndani tuu.

Nipeni msaada wa mawazo wadau, ni hayo tuu.
 
Back
Top Bottom