Wenzangu nimepata gari kampala kuna mtu anataka kuniuzia , lakin naomba kujua utaratibu wa kuingiza magari kutoka nchi zetu jirani kama kenya na uganda ,kodi yake tunalipaje? Ni kama mtu aliyelinunua japan?
Naomba msaada wenye ambao ujuzi na uzoefu wa kuingiza magari kutoka nchi jirani,
Ndugu yetu kauliza swali la msingi sana, kwakweli bandarini kuna gharama nyingi ikiwemo gharama zenyewe za kutumia bandari, clearing agent nk, mdai anataka kujua ni gharama zipi atatakiwa kuzilipia na zingine ambazo ataziokoa kwa kununua gari uganda, tumsaidie jamani
Inaonekana humu hakuna mwenye uzoefu wa kweli kuhusu kuingiza gari toka nchi jirani. Kikokotozi kilichopo website ya TRA kinakadiria kodi kwa gari zilizoingizwa kupitia bandari toka Europe na Japan tuu. Hakuna option ya kuweka nchi wala boda. Mkuu kama ulifanikiwa kuingiza naomba utupe mchakato ulikuwaje na ulilipia nini na nini KAOROGOMA