The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,460
- 17,273
Sijui ni sababu ya kodi ama umasikini lakini gharama za maisha Tanzania zinasikitisha sana.
Hii nchi kweli bado masikini na kuja kutoka hapa sio leo.
Leo ukiagiza gari ya mwaka 2001, gari ambayo nchi karibu zote Duniani zimeiondoa barabarani kwa sababu ya kimazingira na kiafya isipokua Tanzania lakini kodi yake utakimbia.
Gari ambazo nchi nyingine zinagawiwa bure Tanzania kodi yake haina mfano.
Sasa basi ingekua ahueni kwa pale unaponunua gari ya miaka michache kama 5 ama 6, lakini wapi, ununue la zamani kodi kubwa, ununue jipya kodi kubwa , sasa hawa wanyonge wataendeshaje magari?
Zaidi ya 90% ya magari yanayoagizwa Tanzania yana umri wa zaidi ya miaka 12. Serikali kila kukicha inapandisha kodi ya vitu sio kupunguza.
CCM hata tukiwapa miaka 800 hakuna kitu watafanya nchi hii zaidi ya kuwafukarisha watanzania.
CCM iko madarakani miaka 60 lakini zaidi ya 80% ya Watanzania ni masikini wa kutupwa, wanaitwa wanyonge.
Chini ya ccm, petroli lita moja Malawi/Zambia kwa pesa za Kitanzania ni 1,200 hadi 1,600 Tanzania ni 2000+. Hayo mafuta yanapitia bandari ya Dar
Chini ya ccm, simenti Zambia/Malawi/Kenya kwa pesa za Kitanzania ni kati ya 10,000 hadi 12,000, Tanzania ni zaidi ya 24,000.
Chini ya miaka 60 ya ccm, sukari nchi jirani kilo moja ni kati ya 800 hadi 1,200, Tanzania ni zaidi ya 2,800.
Njoo kwenye mabati, mbao, thamani za ndani na vitu vingine, nchi jirani zinazotuzunguka pamoja na kua vitu vyao vinapitia bandari ya Dar lakini bei iko chini sana, Tanzania ni mara 2 yake.
Watanzania wanaenda kununua nguo, viatu na vitu vingine Uganda wakati hiyo mizigo ya Uganda inapitia bandari ya Dar es Salaam.
Leo hii baada ya miaka 60 ya uhuru CCM wanakuja na hadithi za kununua ndege, kujenga madaraja, huku zaidi ya 80% ya watanzania ni fukara wa kutupwa, si vituko hivi?
CCM hata tukiwapa miaka 800, hakuna kitu watafanya zaidi ya kuwafanya watanzania waendelee kua fukara wa kutupwa.