Msaada plz hivi mtu akinunua gari kutoka kenya au uganda analipaje kodi

KAOROGOMA

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
510
756
Wenzangu nimepata gari kampala kuna mtu anataka kuniuzia , lakin naomba kujua utaratibu wa kuingiza magari kutoka nchi zetu jirani kama kenya na uganda ,kodi yake tunalipaje? Ni kama mtu aliyelinunua japan?

Naomba msaada wenye ambao ujuzi na uzoefu wa kuingiza magari kutoka nchi jirani,

Asante
 
ukifika mpakani unapaki customs
Nenda kafute usajili wa kenya,jaza Tancis,utatakiwa uambatanishe interpol
Utalipa ushuru,ukipata clearance unaondoka na gari yako,ni vizuri ukamuona wakala wa kutoa mizigo atakupa msaada
 
hata mi nasubiria majibu mkuu. vp ukishushia mzigo bandari ya mombasa kuna unafuu wa gharama?
 
Lazima iwe ifutiwe usajili huko kama inavyokuwa yatokayo Japan au UK. Harafu taratibu nyingine za kodi kama kawaida.
Nadhani ni hivyo.
 
ukifika mpakani unapaki customs
Nenda kafute usajili wa kenya,jaza Tancis,utatakiwa uambatanishe interpol
Utalipa ushuru,ukipata clearance unaondoka na gari yako,ni vizuri ukamuona wakala wa kutoa mizigo atakupa msaada
Ushuru unakuwaje
 
Ndugu yetu kauliza swali la msingi sana, kwakweli bandarini kuna gharama nyingi ikiwemo gharama zenyewe za kutumia bandari, clearing agent nk, mdai anataka kujua ni gharama zipi atatakiwa kuzilipia na zingine ambazo ataziokoa kwa kununua gari uganda, tumsaidie jamani
 
Inaonekana humu hakuna mwenye uzoefu wa kweli kuhusu kuingiza gari toka nchi jirani. Kikokotozi kilichopo website ya TRA kinakadiria kodi kwa gari zilizoingizwa kupitia bandari toka Europe na Japan tuu. Hakuna option ya kuweka nchi wala boda. Mkuu kama ulifanikiwa kuingiza naomba utupe mchakato ulikuwaje na ulilipia nini na nini KAOROGOMA
 
Wewe kalinunue uje Namanga uone moto wake. Kwenye mpaka wa Horohoro yako magari mengi sana yaliyosuswa na wenyewe kwa sababu hiyo hiyo unayofikiria
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom