Kwa ajili ya kupulizia kuta...wataalamu wanaita IRS (in-door residucal spraying), dawa inayotumika ni aina ya pyrethroids kama vile Icon. Nenda maduka ya pembejeo (especially TFA) ukanunue Icon na utafute mtaalamu wa mambo ya fumigations akusaidie.
Hata hivyo, dawa hizi zinaua zaidi mbu wa malaria aina ya anopheles wakati wale wasumbufu aina ya culex hawafi sana. Na kama unaishi mjini (Dar au miji mingine), mbu wanaosumbua zaidi ni culex. Dawa nyingi zinazotumika kuua mbu hawa hazifai kupuliza kwenye kuta!