Msaada please: Nataka kuishaki tigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada please: Nataka kuishaki tigo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by bigcell, Mar 16, 2012.

 1. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  wana jf natafuta msaada wa kisheria jinsi ya kuishtaki mtandao wa tigo,wamezidi kuniibia(over charge) ni mwaka wa 3.5 sasa sina hamu nao kabisa.Nataka wanilipe fidia inatisha sana yaani wana wizi wa wazi wazi.

  Kwanza hawapokei simu ukiwapigia customer care, nina mwaka na miezi miwili sijawahi kusikia sauti ya mhudumu wa wateja.

  Pili tarehe 16/02/12 niliweka vocha ya Tsh. 5000/- muda wa saa moja na unusu nilipiga simu kwenda tigo kwenye no 0712.... niliongea kwa dk 28.12. Nikajaribu kupiga hesabu 1 sec = Tsh. 2+vat 40cents =Tsh 2.40 so; (2.40*60=Tsh. 144*28.12=4049 ndio niliyotumia).Hivyo basi tsh 5000-4049=950.72, na hapo wakti naongeza kulikuwa na bakaa ya 224 hivyo hesabu ingekuwa 5224-4049= 1175. Kwa hiyo basi 1175 waliichukua. ikanibidi niende tigo customer care center kwa hapa dsm pale mlimani city, nikawakuta wahudumu nikapewa no: ya foleni zamu yangu ikafika nikaenda kwa muhudumu. Kilichofuata nikatoa maelezo yangu na hesabu zangu wakajifanya hawajui hizo hesabu wakanipa zao jibu likaja wamenichukulia 1760, wakarudia tena hesabu ikaja 1475, sikuwaelewa tukabishana sana mwisho wa saa wakaniuliza matumizi ya kwa siku nikawaambia kwa wizi wao natumia hadi Tsh: 8,000- 10,000/- kwa siku. Kwa ufupi huo ni mfano mmoja nina mlolongo mrefu wa matatizo kama hilo hapo juu, ambalo nikiliandika hapa ntawachosha. Kama akitokea mwanasheria wa kunishauri nini cha kufanya nitampa details zote tokea mwaka 2010 tatizo lilipoanzia.

  Nawakilisha.
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Sasa mkuu miaka 3.5 wanakuibia nawe umewang'ang'ania tu? Siku hizi biashara huria achana na huo mgongo wa chura, hamia kwingine. Mie walinilamba sana tuuu, nilichofanya ni kuhamia kwengine kwenye kaunafuu kadogo.
   
 3. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  hilo pia wazo zuri mkuu nashukuru sana.
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hilo ni tatizo linalotukuta wote. Anayeweza kutoa mlinganisho wa gharama za mitandao yote na kutujuza upi ni nafuu kuliko yote afanye hivyo ili tufanye uamuzi kutokana na ushahidi. Kwa mfano Voda huko nyuma kidogo ukinunua muda wa maongezi kwa M-pesa walikuwa wanakuongezea 10% kwenye salio. Siku hizi wanadai wanaongeza 25% lakini haziongezwi kwenye salio bali wanasema upige namba fulani ili uone nyongeza yako. Sasa nitajuaje kama hiyo nyongeza ni ya kweli kama siwezi kuhakiki matumizi yake? Hii mitandao yote ni MaRICHMOND.
   
 5. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nadhani umetumia jambo la busara kabla ya kwenda kushtaki moja kwa moja kwa kuwafuata, sasa nenda TCRA barabara ya sm nujoma peleka malalamiko yako,
   
Loading...