Msaada: Ph.D ina umuhimu gani kwa mwalimu wa sekondari?

Kiukweli serikali haijaidhinisha viwango vya GPA zinazotakiwa ila ni kasumba ya vyuo vingi vya Tz kama UDSM, UDOM, SUA,DUCE,MUCE, SAUT, RUCU, ST. JOHN, MWENGE, etc. Kutaja vigezo hivyo vya GPA nilivyokuwa nimevitaja hapo awali.

nimekuelewa maana kuza kozi nyingine kama medicine , inijinia.. kupata hayo ma GPA makubwa ni kazi sana
 
Tatizo walimu wengi wanasoma masters na PhD bila malengo kwamba wanataka kuwa nani baada ya kupata elimu hizo. Walio wengi ni waoga kuingia mikataba mipya ya ajira na kuacha ya kufundisha sekondari. Kumbuka kwa sasa masters na PhD hazina scale za mshahara serikalini na hata promosheni za madaraka siku hizi hazitegemei sana elimu yako bali ni "know who" ndo maana kuna maafisa elimu wengi ni graduate na diploma huku kuna walimu wenye elimu kubwa wanalamba vumbi la chaki. Hata wakuu wa shule wengi ni diploma holders na wanahenyesha walimu wenye degree na masters. Kama mtu anaamua kusoma above graduate ni vizuri Ila awe tayari kufikiria beyond ualimu wa sekondari na primary huyo ndiye atakuwa na akili
 
Umesema vema mkuu that's a reality.
 
Kiukweli serikali haijaidhinisha viwango vya GPA zinazotakiwa ila ni kasumba ya vyuo vingi vya Tz kama UDSM, UDOM,
SUA,DUCE,MUCE, SAUT, RUCU, ST. JOHN, MWENGE, etc. Kutaja vigezo hivyo vya GPA nilivyokuwa nimevitaja hapo awali.
minimum GPA kwa mujibu wa TCU ni3.5.wengne wanacomplicate ndo GPA za kufoji nyingi.Kuna malecturer wengne hawawez kudeliver kabisa
 
Nikweli unachokisema kuwa Kufundisha Vyuo Vikuu, GPA hizo za 3.5 or above ya Undgr .na 4,Master mashart hayo yapo.
Lakini zipo post nyingi sana zinataka PhD holder lakini hawahitaji GPA.Vile vile hata akirudi kwa mwajiri wake ana nafasi kubwa ya kupata promotion kama vile u-DEO,ukaguzi nk.Anaweza pia akapiga post graduates nyingi za Dip, Cert nk baada ya kumaliza PhD YAKE halafu zika suppliment hizo GPA zake na bado akapata vyuo vya kufundisha.
Kwakweli ni jambo jema alilofanya.
 
Kiukweli serikali haijaidhinisha viwango vya GPA zinazotakiwa ila ni kasumba ya vyuo vingi vya Tz kama UDSM, UDOM, SUA,DUCE,MUCE, SAUT, RUCU, ST. JOHN, MWENGE, etc. Kutaja vigezo hivyo vya GPA nilivyokuwa nimevitaja hapo awali.

Una uhakika na hicho ulichokiandika hapo juu?!
 
Kiukweli serikali haijaidhinisha viwango vya GPA zinazotakiwa ila ni kasumba ya vyuo vingi vya Tz kama UDSM, UDOM, SUA,DUCE,MUCE, SAUT, RUCU, ST. JOHN, MWENGE, etc. Kutaja vigezo hivyo vya GPA nilivyokuwa nimevitaja hapo awali.
Vyuo vikuu huwa na haki na wajibu wakuweka vigezo wanavyotumia kuajiri walimu. Na kigezo kimoja wapo ni kiwango cha ufaulu-GPA au Grades. Hivyo hakuna chuo ambacho hakina hivi viwango. Kwa upande wa serikali kuna kanuni za pamoja za kuajiri na kupandisha vyeo kwa wanataaluma wao (nafikiri kuamzia mwaka wa jana). Hivyo si kasumba kuweka vigezo.
 
Kwa nchi za wenzetu bila degree ya Kwanza au ya pili uwezi fundisha hata chekechekea, PhD holder anaweza fundisha secondary au chuo. Ni malengo yako tu.
Kufundisha secondary huhitaji PhD. Hii haimaanishi kuwa mwenye PhD hawezi kufundisha sekondari. Issue inakuja kwenye umakini wa kutumia human resources-wachumi watakuambia hakuna value for money, na muajiri wako sidhani kama atakulipa mshahara unaoendana na PhD yako. Lakini pia PhD hukufungulia milango mingine hata kama sio kufundisha chuo.
 
Elimu ni hazina.Kuwekeza katika elimu ni muhimu kuliko kuwekeza katika magari,mashamba,maduka,nk.Nakushauri hata wewe kama fursa ipo piga shule,tena hapo pana Colleges kibao,yaani mimi ninawaonea wivu sana watu wanaofanyakazi Iringa,Dodoma,Dar na Moro maana kuna vyuo vingi vinatoa cert,Dip nk,tena evening class, ningekuwa huko ningepiga kila aina ya kozi.

Wewe kama mimi
 
PhD.....!!
Kama haitumiki Secondary, namshauri ajaribu Primary inaweza ikawafaa
tapatalk_1574003001155.gif
 
Back
Top Bottom