Msaada: Ph.D ina umuhimu gani kwa mwalimu wa sekondari?

VendoPatrick

Member
Jun 12, 2016
15
5
Kuna mwalimu anafundisha sekondari hapa Iringa ameomba kwenda kusoma Phd. Sasa najiuliza ya kazi gani kwake?
 
Elimu ni hazina.Kuwekeza katika elimu ni muhimu kuliko kuwekeza katika magari,mashamba,maduka,nk.Nakushauri hata wewe kama fursa ipo piga shule,tena hapo pana Colleges kibao,yaani mimi ninawaonea wivu sana watu wanaofanyakazi Iringa,Dodoma,Dar na Moro maana kuna vyuo vingi vinatoa cert,Dip nk,tena evening class, ningekuwa huko ningepiga kila aina ya kozi.
 
Duuh wewe utakuwa kilaza wa ukweli. Yani umeshindwa kuona/kutambua umuhimu wa mwalimu kujiendeleza kielimu hadi ngazi ya PhD ! Mimi nampongeza sana huyo mwalimu na namuombea kwa mungu aendelee mbele hadi aukwae u-profesa kabisa.
 
Yaani maana yake hataki tena ualimu wa sekondari. Huwezi soma PhD ukarudi kufundisha sekondari, unless umechagua mwenyewe kufundisha sekondari, wapo walimu wa namna hiyo wachache kama aliyenifundisha chemistry. She was the best teacher i've ever had.
 
Nimekuelewa mkuu
 
Pale Mlimani nilifundishwa na maprofesa wengi ambao waliwahi kufundisha primary wakajiendeleza wakafundisha sekondari na hatimaye wakapata PhD na kuwa maprofesa. Na kwa kawaida hawa wanafahamu umuhimu wa elimu na ni walimu wazuri sana yaani anakufundisha mpaka unaelewa hata kama ni slow learner au ki.la.za kama ile mutoto yetu ileeee!

Wewe umepanga kuwa mwalimu wa sekondari maisha yako yote mpaka unamshangaa mwenzio anayetaka kujiongezea elimu? Umenisikitisha!
 
Kweli umenishangaza. Elimu hiyo inaweza mfungulia milango mingi. Anaweza pata nafasi za uongozi kwenye secta ya elimu, kufundisha vyuo na mengine mengi. Yeye hajioni mwalimu wa sekondari miaka 5 mbele kama wewe !!
Nampongeza saaana.
Yaani yeye ana GPA ya 2.0undergraduate na masters ni 3.0 sasa nilikuwa najiuliza akimaliza hiyo Phd atafundisha chuo gani? Na hivi wanakomaa kuhusu GPA kuanzia 3.8undergraduate na4.0masters in case anataka kuwa lecturer wa vyuo vikuu.
 
Kila chuo kina qualifications zake za wewe kuwa lecturer vipo vitakavomkubali ...
 
Kuna mwalimu anafundisha sekondari hapa Iringa ameomba kwenda kusoma Phd. Sasa najiuliza ya kazi gani kwake?
Mwalimu nimshauri mkubwa sana aisee....kwakiwango cha phd, anao uwezo kumsoma kila mwanafunzi individually na kuwashauri wanafunzi ku specialize kwenye masomo yanayoendana nao kwa ajili ya future careers...India mfano chekechea walimu wao ni phd na masters in some schools...kambale mkunje angali mbichi.

Watu wngi wanahangaika kuanzia chekechea, primary, secondary na mavyuoni wanasoma tu na akilini hajui atakuja fanya kazi gani...
ni umaskini tu lakini naamini PHDs ndio ilibidi wafundishe primary schools kutengeneza future work force ya Tanzania. Au hata PHD mmoja kila shule kuwa mshauri wa masomo na careers.
 
Kila chuo kina qualifications zake za wewe kuwa lecturer vipo vitakavomkubali ...
Saizi Ndalichako anakagua vyuo vyote na anataka viwe na uniform qualifications na ameanza na TEKU sasa hunijibu kuwa huyu bwana itakula kwake?
 
Mwalimu nimshauri mkubwa sana aisee....kwakiwango cha phd, anao uwezo kumsoma kila mwanafunzi individually na kuwashauri wanafunzi ku specialize kwenye masomo yanayoendana nao kwa ajili ya future careers...India mfano chekechea walimu wao ni phd na masters in some schools...kambale mkunje angali mbichi.

Watu wngi wanahangaika kuanzia chekechea, primary, secondary na mavyuoni wanasoma tu na akilini hajui atakuja fanya kazi gani...
ni umaskini tu lakini naamini PHDs ndio ilibidi wafundishe primary schools kutengeneza future work force ya Tanzania. Au hata PHD mmoja kila shule kuwa mshauri wa masomo na careers.
Good idea
 
Kwa nchi za wenzetu bila degree ya Kwanza au ya pili uwezi fundisha hata chekechekea, PhD holder anaweza fundisha secondary au chuo. Ni malengo yako tu.
 
Saizi Ndalichako anakagua vyuo vyote na anataka viwe na uniform qualifications na ameanza na TEKU sasa hunijibu kuwa huyu bwana itakula kwake?

kwani serikali imeweka sheria kwamba kuwa lecturer lazima uwe na GPA kuanzia ngapi..?! mimi bado sijaona hebu nambie ntapata wapi..? link nkasome
 
Kiukweli serikali haijaidhinisha viwango vya GPA zinazotakiwa ila ni kasumba ya vyuo vingi vya Tz kama UDSM, UDOM, SUA,DUCE,MUCE, SAUT, RUCU, ST. JOHN, MWENGE, etc. Kutaja vigezo hivyo vya GPA nilivyokuwa nimevitaja hapo awali.
 
Back
Top Bottom