Msaada: Pesa yangu inapotea bila kujua inaenda wapi!

Msaada: Pesa yangu inapotea bila kujua inaenda wapi!

Jaribu hili kila ukiuZa ikifika elfu kumi kaweke kwenye simu yani tigo pesa au mpesa usisubiri mpka mzigo uishe
 
Pia uwe unamtolea Mungu fungu la kumi kama biashara yako faida elfu 10 unatoa elfu 1 unapeleka msikitini au kanisani unaweka kwenye bahasha una mwambia Mungu nakutolea kama ulivosema tukutolee naomba unilindie biashara na umlaani yeyote atayeniibia
 
mkuu pole sana,
unajua hii hali inatokeaga sana kwa hapa mjini...
jua ni kali sana ivyo nakushauri katika mizunguko yako jitahidi unywe maji ya kutosha hayo ni mawenge hutokea endapo maji yatapungua mwilini.
 
Hakuna kitu kama hicho muanzisha uzi anajichanganya tu wewe unauza elf 20 unarudi nyumbani na elfu 2 hiyo biashara si itakuwa imeshakufa mana mauzo kama hiyo elfu 20 sina hakika kama hiyo biashara ni kubwa
basi akishaziesabu anavyorudi nyumbani azishike asiweke mfukoni
[emoji23]
 
Ikiwa unajua mahesabu vizuri yaani huzidishi change wala nini pendelea kutoa fungu la kumi LA kila kipato chako hautapoza tena
Hahitaji mambo ya kiibada huyo, angalia haja acknowledge hata comment moja ya kiibada, amepanick alipoambiwa aende kituo cha afya na kamfata jamaa PM eti wakamkamate chuma ulete, ana imani flan ya kishirikina
 
Chuma ulete wanakufanyia ushenzi.
Jaribu kutembea na hirizi mfukoni.
 
chuma ulete weka kipande cha mkaa unapohifadhia hela ni suluhu
 
Badilisha kwanza hiyo avatar yako, msiwe mnavamia vamia tu picha za mitandaoni/movies bila kujua asili au nyuma ya pazia picha imebeba nini...
 
Hahitaji mambo ya kiibada huyo, angalia haja acknowledge hata comment moja ya kiibada, amepanick alipoambiwa aende kituo cha afya na kamfata jamaa PM eti wakamkamate chuma ulete, ana imani flan ya kishirikina
Duh bas acha aendelee tuu kupoteza....
Kwanza nsha anza kuhisi sio mkweli
 
Hahitaji mambo ya kiibada huyo, angalia haja acknowledge hata comment moja ya kiibada, amepanick alipoambiwa aende kituo cha afya na kamfata jamaa PM eti wakamkamate chuma ulete, ana imani flan ya kishirikina
Mkuu sina umani yoyote ila kama upo uwezo wa kumkamata mwiz wang kwann nisimkamate yeye anajua uchungu wa kupoteza hela na jua lote la dodoma
 
Tatzo hili limenitokea takriban siku tatu zilizopita na leo nikajaribu kuzungusha mzigo nikiwa makini sana nilichukuwa mzigo wa elfu kumi na baada ya kuumaliza ndani ya lisaa limoja nikarudi geto na kukagua hela nikajikuta nina elfu mbili mia saba (2700)
Jaribu kufanya hivi
- Kila ukipokea fedha, usiweke mfukoni, bali weka kwenye mpesa, Ukizingatia huduma zipo kila kona.
- Then lete mrejesho
 
Back
Top Bottom