Kwanza mkuu Paypal hawakati hata senti moja kwa mnunuzi bali wanachukua kamisheni kwa muuzaji. Pili unapolipia bidhaa kwa Paypal yaiwezekani kuibiwa, kinachofanyka ni hichi:-
Unapojisajili kwenye Paypal wao wanaweka taarifa za akaunti yako, unaponunua bidhaa kutoka kwa muuzaji yeye hawezi kuzipata taarifa za akaunti yako ila wewe unawapelekea taarifa Paypal kisha Paypal wanamlipa fedha muuzaji aliyekuuzia wewe bila ya kumpa taarifa za akaunti yako ya benki. Hivyo basi njia hii ni salama kwenye ununuzi.
Vile vile eBay sio wanaokutafuta wewe na kukutumia bidhaa unayonunua, eBay hawana bidhaa hata moja bali wauzaji mbali mbali huuza bidhaa zao kupitia mnada wa eBay. Kwa hiyo unaponunua bidhaa kwenye eBay uwe makini na kuhakikisha kwamba muuzaji yuko tayari kupost mzigo kuja Tanzania. Wengi huorodhesha nchi ambazo wako tayari kupost, ikiwa hakuorodhesha unaweza kumuandikia email na kumuuliza muuzaji kabla ya kununua, kama yuko tayari kupost Tanzania na atakuchaji shilingi au dola ngapi.
Mwisho kabisa ukilipia bidhaa kwenye eBay na kulipa kwa Paypal, iwapo mzigo haukukufikia Paypal wanakurudishia fedha zako zote bila ya kukata hata senti moja. Lakini huchukua muda kama wa mwezi mmoja kufanya uchunguzi ni kwa nini mzigo haukukufikia na kuhakikisha kwamba wewe sio tapeli uliyepokea mzigo kisha unajifanya hukuupata. Mimi binafsi nilishawahi kununua simu miaka michache iliyopita, nakumbua ilikuwa ni HTC Advantage kwa £300.00, kumbe jamaa alikuwa ni tapeli akaingia mitini kwa hiyo nililipwa pesa yangu ingawa ilichukua takriban siku 40 hivi.[/QUOTE)Mkuu mi naongea vitu ambavyo ninavifanya kila siku baada ya kununua kitu mtandaoni kwa kutumia paypal,watakutumia electronic receipt so wewe soma ile receipt imeandikwa wamekata asi;imia ngapi maana kila kitu kipo wazi kabisa alafu check balance ya pesa zako ni sh ngapi coz paypal huwa hawafanyi kazi za bure bure.