Msaada: Niufundi gani nikajifunze veta ambao utaendana na soko la ajira

Awali ya yote napenda kumshukuru muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake.
Ni matumaini yangu hamjambo na wote ni wazima wa afya. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28 elimu yangu ni kidato cha nne (form four) sikuweza kujiendeleza kwa njia yoyote kielimu kutokana na hali ya maisha yangu, hivyo kutokana na maisha yangu kuwa magumu na kukulia katika umaskini mkubwa baada tu ya kumaliza kidato cha nne niliamua kutafuta kazi na kufanikiwa kupata kazi ya ulinzi katika kampuni moja hapa mjini.
Kulingana na hali yangu nikawa naweka pesa kama akiba ili nije kujiendeleza kielimu kwani naamini maisha bila elimu ni sawa na bure. Nimefanya kazi ya ulinzi kwa muda wa miaka sita (6) na sasa nimekusanya pesa kwa kiasi lakini ndoto yangu ni ileile bado nataka kujiendeleza kielimu, sitaki kurudia masomo ninachohitaji sasa ni ufundi (taaluma) yoyote iwe kama fani yangu.
Hivyo napata tabu na shida sana nikifikiria ni fani ipi nijifunze na sina hata aidia (idea) na fani yoyote.
Naombeni msaada wa mawazo yenu wanajamvi wenzangu, ahsanteni na Mungu awabariki sana,..
Nawasilisha
Ujenzi au ufundi selemala
 
Ni nzuri sana hii kama utapata mtu wa kukupa mitambo yake uopareti,,,,kuchukua laki kwa siku ni kawaida sana ila ni kazi za msimu wa kiangazi tu
Hii nzuri lkn mpaka upate kitengo jasho la meno lazima likutoke
 
Kitu cha msingi kuliko vyote ni kuchagua fani ile ambayo roho inapenda
Sisi tunaweza kukushauri tu wewe ndio unajua talanta yako imelalia wapi. Inahitaji uwe makini kujitafiti. Usiache soko la Ajira liamue specialization yako.
Nimeishaona mtu amehangaika zaidi ya miaka 20 ana switch on different careers baadaye akaja kuangukia kwenye welding ambayo anaifanya extremely well, ana workshop zaidi ya 7 hapa mjini ktk muda mfupi sana
 
Back
Top Bottom