Msaada: Niufundi gani nikajifunze veta ambao utaendana na soko la ajira

Kajifunze ufundi Cherehani, jifunze mambo ya kupamba wanaita kudarizi! Na utundu mwingine, Ukimaliza hapo fungua Tailoring Mart yako, anza na cherehani hata mbili tu na tafuta MTU mfanye colabo, kisha lipia kibanda shona Mashati ya kudarizi na magauni yake. Shona Suti na mavazi ya kibubifu!!! Kuwa mwaminifu Kwa kazi yako, tembea huku na huko uone Mungu atakavyobariki kazi za mikono yako hadi ukimbie

Hata mimi pamoja na umri kwenda natamani sana kazi ya kushona na kubuni mavazi......siku moja nitasomea fani hiyo.....

Inalipa sana kwani mtaji wake ni mdogo tu
 
Kajifunze ufundi Cherehani, jifunze mambo ya kupamba wanaita kudarizi! Na utundu mwingine, Ukimaliza hapo fungua Tailoring Mart yako, anza na cherehani hata mbili tu na tafuta MTU mfanye colabo, kisha lipia kibanda shona Mashati ya kudarizi na magauni yake. Shona Suti na mavazi ya kibubifu!!! Kuwa mwaminifu Kwa kazi yako, tembea huku na huko uone Mungu atakavyobariki kazi za mikono yako hadi ukimbie
Hili wazo lako ni zuri kwa upande wangu! Akisha fungua anaweza kupata tenda za kushona nguo za wanafunzi

Au asomee mambo ya udereva na ufundi kidogo wa magari ukisha pata leseni huwezi kulala njaa!

Au mbele kwa mbele afanya biashara ya ufungaji wa kuku wa nyama na mayai, huku unaingiza hela huku unafanya michakato mingine

Tatizo moja la sisi vijana ni uwoga wa kujaribu
 
Hata ufundi Umeme wa majumba nayo ukisoma huwezi lala njaa, Ila ukiamua kusoma hiyo fani jitahidi kutafuta mafundi Umeme waliofuzu na wanaofanya kazi mitaani wakusaidie ili uwe mahiri zaidi
 
mi nilisomea ufundi seremala 2005,kiukweli ni kazi nzuri lakini mimi binafsi sijapata mafanikio sana lakini ni mimi binafsi, fani hii ina idara nyingi kama feniture za aina zote,uezekaji wa nyumba na na kazi za ndani ya nyumba nk nk, jaribu hii mkuu.
 
NIMEKULETEA LIST ZA BIASHARA MBALIMBALI.... KAMATA MOJA UJIKOMBOE


1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, 10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe 2
7. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k 34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental. 51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe 68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel) 71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki 81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji**
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo
151.Kuendesha bodaboda,Taxi,Daladala,Carry

Nimekutana nazo mahali
 
Hili wazo lako ni zuri kwa upande wangu! Akisha fungua anaweza kupata tenda za kushona nguo za wanafunzi

Au asomee mambo ya udereva na ufundi kidogo wa magari ukisha pata leseni huwezi kulala njaa!

Au mbele kwa mbele afanya biashara ya ufungaji wa kuku wa nyama na mayai, huku unaingiza hela huku unafanya michakato mingine

Tatizo moja la sisi vijana ni uwoga wa kujaribu
Na soko ni LA uhakika
 
mi naona fani ya upigaji picha both video and still pictures inalipa sana ukipenda kujiajiri wewe tu ukipenda kuajiriwa ni wewe tu,ukiongeza na video editting utakua umemaliza kabisaaa
 
Kwanini usiwekeze pesa kwenye biashara ya maana na uhakika utazalisha pesa nying Zaid
Biashara si dhamana ndugu ujuzi ni dhama kubwa sana ,biashara ni rahisi sana kuisema lakini kuitekeleza ni ngumunkwa sababu inetegemea mambo mengi ,kwanza mazingira,aina ya jamii unayo taka kuifanyia biashara ,aina ya biashara,gharama za kuendesha niashara hiyo nk. Hivyo ujuzi ni bora zaidi
 
Awali ya yote napenda kumshukuru muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake.

Ni matumaini yangu hamjambo na wote ni wazima wa afya. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28 elimu yangu ni kidato cha nne (form four) sikuweza kujiendeleza kwa njia yoyote kielimu kutokana na hali ya maisha yangu, hivyo kutokana na maisha yangu kuwa magumu na kukulia katika umaskini mkubwa baada tu ya kumaliza kidato cha nne niliamua kutafuta kazi na kufanikiwa kupata kazi ya ulinzi katika kampuni moja hapa mjini.

Kulingana na hali yangu nikawa naweka pesa kama akiba ili nije kujiendeleza kielimu kwani naamini maisha bila elimu ni sawa na bure. Nimefanya kazi ya ulinzi kwa muda wa miaka sita (6) na sasa nimekusanya pesa kwa kiasi lakini ndoto yangu ni ileile bado nataka kujiendeleza kielimu, sitaki kurudia masomo ninachohitaji sasa ni ufundi (taaluma) yoyote iwe kama fani yangu.
Hivyo napata tabu na shida sana nikifikiria ni fani ipi nijifunze na sina hata aidia (idea) na fani yoyote.

Naombeni msaada wa mawazo yenu wanajamvi wenzangu, ahsanteni na Mungu awabariki sana,..

Nawasilisha
Biashara si dhamana ndugu ujuzi ni dhamana kubwa sana ,biashara ni rahisi sana kuisema lakini kuitekeleza ni ngumu kwa sababu inetegemea mambo mengi na kushuka kutoka 100 hadi 0 ni ndani ya saa chache tu unafutika kqtika biashara hasa kwa sisi wenye vimitaji vidogo ,lakin biashara inayegemea mambo mengi hasa kwa wewe unaye anza kwanza mazingira,aina ya jamii unayo taka kuifanyia biashara ,aina ya biashara,gharama za kuendesha niashara hiyo nk na usipo kuwa makini utakaanga mtaji wako . kwa vile umeonesha nia ya kuwa na option basi ujuzi ni bora zaidi maana hadi unaingia kaburini
 
Back
Top Bottom