Msaada Nipo Nje ya Inchi.

Kumbe unaongelea hao sawa, Mimi toka 1998 nimeingia SA nimetumia Asylum seeker,Passport ya Tanzania na baadae Id ya SA na passport yao nimeifuta baada ya kutotaka kufanya kazi SA sasa natumia mkwaju wa Tanzania tumefanya utundu wote kuhusu makaratasi kwa sababu kampuni zetu zilikua zinafanya kazi nje ya SA...
Nimeshaeleza hapo juu jinsi tunavyoishi SA au China au Hong Kong ni kugonga kwa kutoka Nchi Jirani ili uongeze muda zaidi ya hapo hakuna na muda mwingine ukikutana na mkorofi hasa Beit bridge anakupa siku chache inatakiwa aende Botswana nauli ni kidogo tuu na ndio wanavyoishi hivyo sio Home Affairs ukagonge walishafuta huo mchezo 2002 nadhani...

Ndugu nimeona mchango wako ila sijelewa kuhusu huo mkwaju na maana teyari niko illegal na pia je hiyo visa ya miaka mitatu na weza ipata kwa ghalama gani?
 
Ndugu nimeona mchango wako ila sijelewa kuhusu huo mkwaju na maana teyari niko illegal na pia je hiyo visa ya miaka mitatu na weza ipata kwa ghalama gani?
Mkuu kwa kuwa upo Cape ni bora ufatilie ile karatasi ya kikimbizi ufanye mpango wa kuishi ukiwa nayo ile inakuruhusu kufanya kazi,mambo ya kuongeza siku yapo Johannesburg ukiweza unaweza kwenda Jozi wanaofanya hiyo kazi waaminifu ni wale madereva kwenye kampuni za Wazambia bus za abiria Shalom au Jordan bus unawapa wanaenda kukugongea ya miezi mitatu wanachukua rand 1000 kwa iliyozidi siku...kupata kibali cha muda mrefu wanatoa Airport unapoingia au ukitumia Botswana boarder kuingia SA,Beit bridge watata..utafanikisha tuu ni swala dogo sema upo Cape ndio maana unaliona gumu...
 
Hiyo nayo nimejaribu pia hazi ya ikimbizi wanatoa pretoria huku capetown ni kurenew tu ila ninampango wakutafuta chama cha Watanzania hapa Capetown je utakuwa unafahamu kilipo maana niko kwenye hali mbaya ya kifedha kwenda jorberg sitaweza au pretoria maana pia nikifika huko inabidi tena nitoe pesa je utakuwa una fahamu kuhusu hiko chama?
 
Kwanza hatuhitaji kuingia South Afrika kwa visa kama una hold hati ya Tanzania.


pili upo South sehemu gani? Unaishi wapi? Unafanya nini hapo ulipo sasa.... Hujaeleza vizuri mkuu tukuelewe.

Jieleze vizuri Mzee baba.
Wewe hujui unachoongea. Kuingia huhitaji viza sawa, lakini muda uliopewa ukiisha unatakiwa uextend viza yako au usepe. Free visa on entry does not mean uishi huko muda wote unaotaka. It's only a stay of three months.
 
Je watanisaidia kuniludisha nyumbani au watanisaidia kupata Visa!!

Bro hapa SA uitaji kuwa na viza mzee, hapo ni residence permit or work permit. Kama miezi mitatu uliyopewa imeisha ya kukaa free , nenda ubalozini omba kuonana na afisa mmoja Mr lupembe mueleze tatizo lako, au pale geti waweza kukuzingua kuwa kama hauna appointment nae, wee nenda pale getin na document zako uwaeleze unaenda ku-certify document zako kumbuka kutoa copy hizo document i hope utaweza kuingia ndani na uweze kuwaeleza shida yako.
 
Bro hapa SA uitaji kuwa na viza mzee, hapo ni residence permit or work permit. Kama miezi mitatu uliyopewa imeisha ya kukaa free , nenda ubalozini omba kuonana na afisa mmoja Mr lupembe mueleze tatizo lako, au pale geti waweza kukuzingua kuwa kama hauna appointment nae, wee nenda pale getin na document zako uwaeleze unaenda ku-certify document zako kumbuka kutoa copy hizo document i hope utaweza kuingia ndani na uweze kuwaeleza shida yako.

shukrani bro ila nipo Capetown nilijaribu kuwapigia simu wakapokea wadada nika waelezea tatizo langu wkaniambia hatuwezi kukusaidia kwa sababu hiyo si kazi yetu ni kazi ya home affair. JE unanishauri ni jaribu tena?
 
Pita njia za panya chief, maana kuliko kuingia mikononi mwa maaskari ya huko SA ni bora udakwe Kwenye kambi za jeshi unaiba kifaru....
Duuh yaan jamaaa kaomba msaada wa kimawazo ili ajue la kufanya na ameleta humu akijua Kuna watu wanaweza mpa mawazo lkn naona anapondwa tyuuu sio fresh matatizo yanatokeaga tyuu apewe msaada kwa anayejua bana
 
Taarifa zimekamilika ila Nilikuwa nataka Nisaidiwe nifanyaje ili niishi kisheria ila sijauliza maswala ya kazi maana kuna wengine wanazani kupata kazi inayoeleweka nirahisi sivyo huku nilazima uwe kisheria ndo upate mkataba wa kazi other wise unafanya kazi kama wanazo fanya watanzania wengine hapa SA na dhani hapo nimeeleweka.
 
Ok.

Kuomba vibali vya kazi kuna mawili...ukose au upate.

Kwangu mimi mtu akianza kutafuta kibali cha kazi kabla ya kupata kazi nitamshangaa.

Kwanza unatumia pesa ilihali hauingizi pesa...Na unaweza kulipa hizo Rand 3000 ukakosa hicho kibali.

Pata kazi hata kama ni mbovu kama usemavyo itakusaidia kupata makaratasi na kuishi.
Mkuu ulishawahi kuishi nje au unaongea tu? Nani akupe kazi wakati unaishi kinyume cha sheria? Kwanza kwa nchi kama South Africa kupata kazi hata kama una documents zote ni vigumu sana. Labda uwe na critical skills. Sembuse unaishi illegal upate kazi? Hiyo haiwezekani. Ukiwa illegal kazi unayoweza kupata labda ya kunyoa salon za wabongo na waburundi. Au ujingiize kwenye kuuza unga na ujambazi. Hizo ndio kazi za wabongo wanaoishi huko illegally. Sasa hivi huyo wakimdaka ni lindela tu. Aombe asikutane na Immigration officers. Pona yake ajifanye mkimbizi akachukue karatasi la ukimbizi Durban au Pretoria. Wakimdaka kabla ya hilo karatasi la ukimbizi safari ya bongo imewadia.
 
Tehteh...

Nilikuja kwenye huu uzi maana nayajua yote na shida zote hizo ndiyo maana nilisistiza mtoa mada aseme alipo kwama nimsaidie napoweza.

Wewe ni mfuko mzee baba..acha nitoke kwenye uzi ufurahie.

kakujibu sahii maana ulikuwa uwelewi nikikuambia unasingizia maelezo hayaja kamilika
 
Back
Top Bottom