Msaada, nimueleze kaka juu ya tabia hii ya mkewe?

Msaada, nimueleze kaka juu ya tabia hii ya mkewe?

Kwanza nakupongeza sana kwa msimamo wako, na pia nakusisitiza usithubutu abadan kutembea na mke wa mtu yeyote yule si wa kaka yako tu. Wewe bado ni kijana mdogo sana huyo mke wa kaka yako atakutumbukiza kwenye matatizo makubwa sana na kaka yako na ndugu wote wa upande wenu pindi itakapogundulika, na kwa wengi wetu sisi wanaume hilo ndio kosa kubwa kuliko yote akilifanya mwanamke kwa mumewe na kupewa baraka ya kumuacha mke, hivyo kosa utajuta maisha yako yote kwani utakuwa umetenganisha familia ya kaka yako hata watoto wao hawatakusamehe.
Kumbuka kwamba mke si ndugu na anaweza kuachika siku yoyote kwa sababu yoyote, ni tofauti mno na kaka yako.
Nakushauri kama huyo shemeji yako ataendelea kukusumbua ni bora umueleze kaka yako hili suala vinginevyo huyo mwanamke anaweza kukusingizia kuwa wewe ndie unaemtaka na hivyo kukosana na kaka yako, hili ni muhimu hata Kama kaka yako atakuwa upande was mke wako lakini itakusaidia sana kuliko kukaa kimya. Jioni njema.
 
We mtoto wa mama nini?mwanaume huwezi kumkoromea mwanamke?mwambie live asikulete upuuzi na mikosi kwenye familia yenu la sivyo utamwambia kaka ako...lazima umuonyeshe kitu anachokitaka ni kuleta laana kwenye familia yenu..man up acha kuwa mwepesi mwepesi
 
Ohooo mbuzi kala mkeka. Nachoamini hakuna siri chini ya jua na hata mkifanya siri kwa miaka mingapi ipo siku mtashikwa live bila chenga. Nakushauri umwambie bro ako upo busy huna muda wa kumsaidia hizo kazi maana ukienda afu ubaki na msimamo wako yatakukuta mengi 1.Mke kumwambia kaka'ko unamtaka kimapenzi, ukafukuzwa kama mbwa na bro wako mkakosana nae 2.Mke kukuchukia suala la msosi liwe la kuvizia pindi bro wako yupo au akupe hata sumu maana akili zao wanazijua wenyewe.
Kaka usimwambie maana ukimwambia atauliza wife afu wife akuruke aseme we ndo unamtaka. Bro akiambiwa hvo na wife aanze uchunguz huku wife akijenga chuki na wewe. Itokee siku akuite chumban mwake umfungie pazia mlangon afu apige kelele unambaka, bro afike asikie wife anasema "Sinilikwambia mume wangu, ona sasa", hapo ndo umekwisha na utarudi kwenu. Ukweli utajulikana bro wako akiwa na wajukuu.
NB
Usijaribu kufanya mapenzi na shemeji yako laana itakutafuna. Potezea uende kwa mujibu wa sheria nahisi ukitoka huko utakuwa Mzalendo hasa.
 
Mitihani ya dunia ndo hiyo.

Jaribu kumueleza shemeji yako athari zinazoweza kutokea kaka yako akibaini, msistize sana anaweza kukuelewa akatafta baharia mwingine.

Suala la kumueleza kaka sio zuri, wanaume sometimes wanaweza kuwa dhaifu sana kwa wake zao...ukimwambia kaka yako ni sawa na umempa option ya kuchagua Kati yako na shemeji yako.
Mƙuu umeongea point sn unaweza ƙuwa mshauri hata wa milembe na vichaa wakatulia kula tano!
 
Je akifanyiwa visa na huyo shemejie ya kwamba amemtaka yy hv unajua tabia za wanawake?je unamfaham derila?
Ivi unajua mara nyingi kaka mtu ni ngumu kua upande wa mdogo wake kwenye kesi kama hizo? Shemeji anaweza msweet talk mumewe na mdogo mtu ankaonekana ndo alimtaka shemeji!!!
Huyo kaka atafute tu njia zingine za kumkwepa wifi mtu...
 
Utakapoishi nae nyumba moja hutaweza kuhimili majaribu. Muombe kaka upange kwako au akuelekeze kwa mshkaji ukae nae. Huyo mwanamke anaweza akakuwekea wingu kwenye mafanikio yako ukimuendekeza, kuwa makini na msimamo zaidi
Ila tunza ushahidi wowote wa kuonyesha yeye ndio alikutska ili akikuchukia kwa kumkataa uwe na cha kujihami siku akimwaga mboga
 
45e6210b249a269578abc2e2dd83f1cc.jpg
Huenda Shem anahitaj msaidizi wa mumewe, so kaona asipeleke fursa kwengine
 
Kama huwezi kumueleza tumia busara za wazee wao watamfikishia ujumbe bila shida na udugu wenu ukaendelea, ukichelea kusema subiri kufumwa hapo ndio utajua.
 
Wakubwa poleni na majukumu baada ya hapo naomba niende moja kwa moja kwenye maada yangu mimi ni kijana wa umri wa miaka 19.

Kaka yangu alioa miaka 3 iliyopita. Kaka huwa ananiomba niende kumsaidia kusimamia shughuli zake lakini cha kusikitisha mke wa kaka yangu ananihitaji kimapenzi kwa muda wa miaka 2 sasa.

Nimekuwa nikijitahidi kumkwepa na kumpotezea. Sasa nimemalza shule kaka anataka tukaishi wote kwake ili kumsaidia kusimamia shughuli zake lakini nasita sana kwenda sababu ya shemeji na kaka ndiye ninayemtegemea.

Je wadau nimueleze kaka juu ya tabia ya mkewe? Maana sipendi hao watu wagombane.
kijana ukwel utakuweka huru, mwambie kaka yako kinaga ubaga kuhusu ishu hiyo ya shemeji yako
naamin atakuelewa
 
Back
Top Bottom