Msaada: Nimegundua baba mkwe ni mchawi

Sasa hapo mmeo akirithishwa mikoba ile unakua mke wa mchaw.....pole aisee
Ahahahah, kwani unafikiri hilo siogopi mshikaji, maana haya mambo hayana formula. [emoji12] [emoji12] [emoji12] niombee aisee sio mambo ya matani haya, ghafla nakuja hapa nalia, ninavalishwa kaniki
 
Hakuna Uchawi Mbele ya Mungu Mwenye Enzi Yote
Huko unakopita tulishapita na Mwisho wa siku Mungu ndiye Alfa na Omega
Amina, nahitaji tu kupata matumaini, najua Mungu ni mwema sana ila mie mwanadamu kuna wakati nakata tamaa na haya majaribu.
 
Asante, nitazidi kwenye maombi.
 
Na wewe nae ni mchawi labda mlikutana angani umeona umewahi kabla ya yeye hajakutangaza.
Inaweza ikawa ni kweli nami ni mchawi, lkn kama umtu mzima umeolewa ama kuoa unaweza kuelewa ninayoongea kama sivyo, ngoja ufike huko.
 
Ahahahah kweli ningefwata pesa ningeshaaa, ila bahati iko upande wangu, ni kapuku mwenzangu tu.
 
Unawezaje kuishi na mume pale unapogundua kumbe baba yake mzazi ni mchawi anayedhuru watu hakika, nawe ulifichwa kila kitu.

Naomba msaada kwa hili
Kama unaamini ktk Mungu, then huna tatizo. Jina la Yesu Kristu ni kuu kupita yote. Cha kufanya, kama huyo mumeo siyo mchawi basi ujue babu yake anaweza either kutoa kafara mumeo au mtoto wako. Ila ukiwa unasali na kumuamini Mungu, kufunga na kusali sana, mchawi hana nguvu juu ya familia yako. Ila unachotakiwa jirizishe kwanza kabla ya kuamini, ulizia watu wazima au tafuta source ya information ili uconfirm.
 
Kupata access ya huko chumbani ni ndoto maana lazima niende kijijini kwao, huko kwa wazazi wake ambako ninadhani kwa sasa hapana.
Ok ila kama hajawahi kukudhuru usijali na kama ikatokea akaja kwako nijulishe
 
Mke wangu umeshafika huku? Una uhakika baba ni mchawi au hisia zako tu?
Sio hisia mpnz Wangu, we si umeconfess mwenyewe ukaniambia hujui cha kufanya waona aibu jamani na mzee anawachezea timbwili wenyewe jamani? Tuzidi kuomba tu mume wangu, mie hata sitaki urithi hiyo mikoba.
 
Ila hakuna ulicjomkosea Mungu bali alikuweka hapo kwa sababu maalumu.
Hata kanisani wameniambia hivyo hivyo, mmh Mungu mtata sometimes ni nouma, majaribu mengine mazito mnoo mwenzenu.
 
Unawezaje kuishi na mume pale unapogundua kumbe baba yake mzazi ni mchawi anayedhuru watu hakika, nawe ulifichwa kila kitu.

Naomba msaada kwa hili

Contagious,
Je mumeo kama mumeo umesha wahi kuona uhusika wake kwa namna yoyote kwenye haya maswala? umeshawahi kumwuliza kuhusu haya na alikujibu nini?
Binafsi naona kama mumeo yeye pia wale ni wazazi wake tu hatuchagui tuzaliwe na nani.. kama hahusiki au hajui huna sababu ya kuumiza roho yako. Kaa mbali na hao wachawi basi muombe mungu.
Lakini kama na mumeo na anajishirikisha hapo ni jambo lingine.
 
Baba mkwe wako ni mchawi ila wewe ni mshirikina.
Naamini unaelewa tofauti ya iliyopo kati ya uchawi na ushirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…