Msaada: Nimegundua baba mkwe ni mchawi

Msaada: Nimegundua baba mkwe ni mchawi

Kama uchawi wake hauna madhara yoyote kwako endelea na ndoa yako sababu mume hana makosa wala hausiki. Familia itakayojengwa na watoto ni kati yako wewe na mume wako baba mkwe hausiki.

Zamani wazee wakitaka kuchumbia na kuoa wanaufuatilia ukoo wote na tabia zao: vitimbi vikizidi vya baba mkwe hama mji wewe na familia yako lakini usimuache mume wako
Ninakuelewa sana, natamani ningechaguliwa mume, haya mambo ya kukutana barabarani na kupendana yana Mengi, mpaka nimeuliza basi ujue kuna jinsi kubwa ambayo tunaathirika, lakini hakika Mungu ni mwema kwetu.
 
Huwezi kumjua mchawi bila na wewe kuwa mchawi hata kuamini katika uchawi ndio maana wanaoamini katika Mungu hakika wa naamini uwepo wa Mungu na pepo na mchawi kwao hana nafasi
Je kuamini katika Mungu na kweli kunafanya hawa wachawi wasiwepo? La hasha, wapo, na ndio maana tunatakiwa kumwabudu Mungu pekee yake, lkn uwepo wao hautatudhuru, hajanidhuru, ila nimejua kuwa yeye ni Mchawi, nimejuaje, wenyewe ndg wamenieleza, ilikuwaje wakanieleza hapo ndipo ambapo sitakueleza, sijasema kanidhuru, hayo ya kwenu, nimesema nimegundua.
 
Duuuhh kuishi na mtu wa hivyo ni mashaka makubwa, Shirikisha Mungu katika maisha yako na hatakuweza. Ila akikushindwa jiandae kuchukiwa.
Hakika ni mashaka, ama kwa hakika unaanza kujiuliza ukute ndio maana hapa ilikuwa hivi, labda hivi, namna hiyo, kuchukiwa tayari, tena vibaya sana, nilikuwa sijaelewa kwanini ila ndio nimeanza elewa.
 
Ulienda kupiga ramli nini,umejuaje kama ni mchawi,au mlikutana angani mkiwa kwenye zile rocket zenu?
 
Nimeelezwa na wenyewe baada ya baadhi ya mambo kutokea, series ya mambo kwa hakika, nikisema wenyewe namaanisha baadhi ya memba wa familia, ilitokea jambo katika kulitatua kwao wakataka kujimlisha mimi, katika kushangaa ndio nikatolewa upofu.
Acha kufuatilia mambo hayo, waachie wenyewe; Wewe hayakuhusu na wala usijihusishe.
 
Acha kufuatilia mambo hayo, waachie wenyewe; Wewe hayakuhusu na wala usijihusishe.
Mimi sihitaji wala kukumbuka yapo tatizo ni kwamba nashangaa, inawezekanaje? Kwanini mtu achague hilo? Wasingetaka nijue jambo nisingejua lolote.
 
Ninakuelewa sana, natamani ningechaguliwa mume, haya mambo ya kukutana barabarani na kupendana yana Mengi, mpaka nimeuliza basi ujue kuna jinsi kubwa ambayo tunaathirika, lakini hakika Mungu ni mwema kwetu.
Hakika Mungu ni mwema ubarikiwe.
Hiyo ni changamoto kama changamoto nyingine za ndoa.
 
Mimi sihitaji wala kukumbuka yapo tatizo ni kwamba nashangaa, inawezekanaje? Kwanini mtu achague hilo? Wasingetaka nijue jambo nisingejua lolote.
Achana na hayo maneno ya umbea, huna ushahidi. Hata hao waliokwambia hayo maneno sina hakika kama walikuonesha ushahidi. Ni vyema zaidi kukaa kimya kwa mambo tusiokuwa na ushahidi na hakika nayo.
 
Unawezaje kuishi na mume pale unapogundua kumbe baba yake mzazi ni mchawi anayedhuru watu hakika, nawe ulifichwa kila kitu.

Naomba msaada kwa hili

Jamani haya mambo ni magumu sana. Kuna msichana mimi niliachana nae kwa masuala haya tulipotaka kuoana akasema eti kwetu wachawi. Ukweli nilikuja kugundua kuna watu wakutakia mema familia yangu wakamjza maneno. Alipoondoka kuna vitu alisema vitanitokea mbeleni kwa sababu ya uchawi wa ndugu zangu. Baadae nikaoa na vile alivyodhani vitanipata havijanipata akawa alia lia tu nimemuacha. Wakati ukweli yeye ndio alizusha mambo mengi ya uchawi amabao ukimuuliza hata ukaje hajui. So nafikiri hivi vitu ni vya kusemwa tu hakuna uhakika. Ni dalili za kukosa elimu kwa mtu kuendekeza haya mambo. Ila mwisho wa yote uongo hua unajitenga
 
Na wewe nae ni mchawi labda mlikutana angani umeona umewahi kabla ya yeye hajakutangaza.
 
Unawezaje kuishi na mume pale unapogundua kumbe baba yake mzazi ni mchawi anayedhuru watu hakika, nawe ulifichwa kila kitu.

Naomba msaada kwa hili
Na kama ulifwata hela kwao. Utashaa !!

We mrudie Mungu tu na wengine wajifunze kukurupuka sio issue.

Kujua kajuaje inaweza ikawa ni maono ya ki Mungu tu (i cant judge that). Shida inakuja pale watu wanapodhani hamnaga uchawi. Unamuombaje Mungu kama hukubali uwepo wa shetani. Its funny.
 
Back
Top Bottom