mjusilizard
JF-Expert Member
- Nov 7, 2019
- 923
- 1,586
Salaam wanabodi,
Mwaka 2018 nilipata bahati ya kuitwa interview ya shirika la Ujerumani ambapo katika usaili waliniuliza endapo ningekuwa nimefanikiwa kwenda kufanya kazi huko Ujerumani na katika majukumu yangu nikakutana na mashoga ningefanyaje? Kazi niliyoomba ilikuwa ni Kusimamia Mradi wa Vijana kwenye moja ya kambi za vijana kule.
Mwaka jana tena nikapata nafasi ya kuitwa kwenye interview BBC ambako nako nikaulizwa swali endapo katika kuandaa makala zangu za kuchapishwa mitandaoni nikafuatwa na mashoga wakataka niwachapishie habari zao, ama ikatokea mashoga wamekuja kwneye kitengo changu kutaka kuchapishiwa habari zao ningefanyaje? Kazi ilikuwa ni Meneja wa Machapisho ya Mitandaoni.
Katika maswali hayo je, ni jibu lipi lilitakiwa kuwa sahihi kwa unavyodhani? Nilitakiwa niseme nini na nisiseme nini katika kujibu hilo swali? Ungeulizwa wewe swali hilo katika interview ungejibu nini?