Msaada: Nilitakiwa kujibu vipi hapa?

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
918
1,576
Salaam wanabodi,

Mwaka 2018 nilipata bahati ya kuitwa interview ya shirika la Ujerumani ambapo katika usaili waliniuliza endapo ningekuwa nimefanikiwa kwenda kufanya kazi huko Ujerumani na katika majukumu yangu nikakutana na mashoga ningefanyaje? Kazi niliyoomba ilikuwa ni Kusimamia Mradi wa Vijana kwenye moja ya kambi za vijana kule.

Mwaka jana tena nikapata nafasi ya kuitwa kwenye interview BBC ambako nako nikaulizwa swali endapo katika kuandaa makala zangu za kuchapishwa mitandaoni nikafuatwa na mashoga wakataka niwachapishie habari zao, ama ikatokea mashoga wamekuja kwneye kitengo changu kutaka kuchapishiwa habari zao ningefanyaje? Kazi ilikuwa ni Meneja wa Machapisho ya Mitandaoni.

Katika maswali hayo je, ni jibu lipi lilitakiwa kuwa sahihi kwa unavyodhani? Nilitakiwa niseme nini na nisiseme nini katika kujibu hilo swali? Ungeulizwa wewe swali hilo katika interview ungejibu nini?
 
Ungewajibu kuwa ningewasaidia kadiri ya mahitaji ya kundi kwani wapo pia wanahaki kufurahia maisha hapo kazi ungepata.(jibu hili kama ulikuwa na uhtaji sana na hiyo kazi)

Ila kama ww ni msimamo mkali ukijibu vice versa jua hiyo kazi kwako haipo.
Asante sana, hapa nadhani ilibidi kuwa hivi, shukrani sana
 
Mimi sio mtaalamu ila as a professional haitakiwi imani yako binafsi iathiri kazi yako. Unatakiwa work ethics zako zisiwe affected na imani yako binafsi. Kutoa huduma kwa watu wote kwa haki sawa iwe kipaumbele chako. Regardless ya dini, rangi , kabila au utikadi zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana, hapa nadhani ilibidi kuwa hivi, shukrani sana
 
Ushoga ni sexual orientation! Kutokuwa shoga maana yake uko oriented kwenye heterosexual. Na kwa kuwa bado ni kundi dogo katika jamii, sexual orientation yetu haija-favour ushoga basi hilo ni kundi ambalo linachukuliwa kama misrepresented, discriminated! Tabia zao zinachukuliwa Kama dhambi, au kwenda kinyume na asili.

Sasa haki za Binadam ikiwemo kusikilzwa, Uhuru wa kutoa maoni, na kuwakilishwa hauna mipaka. Uwe shoga, uwe Chadema, CCM, uwe mlemavu, mwanamke, mvulana, mweusi, mweupe, mjaluo, Mngoni, Africa au Asia, ulaya haki zote za Binadam zinakuhusu internationally. Hivyo, kwa mtazamo wa kidunia lazima uwasikilize na kuwafikiria, kwa sababu nao ni sehemu ya Jamii unayoihudumia.

Tahadhari.
Kuna baadhi ya nchi, Kabila na dini Jambo hilo linapingwa vikali. Ukisema tu nitawasikiliza utaonekana moja kwa moja unaenda kinyume na S.A.W au Jesus mwana wa Nazareth.

Hitimisho
Nje ya hiyo tahadhari watu wote ni sawa, hivyo wanahitaji fair and equal treatment.

Nawasilisha.

Lugumya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lugumgya,
ASANTE SANA SANA, natamani siku hiyo ningekuwa nimesoma hii pengine muda huu ningekuwa Ujerumani, hahah, barikiwa!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom