Matumizi ya mono, poly, ama amorphous solar panel yanategemea hali ya hewa ya sehemu alipo mtumiaji. Pia zipo zaidi ya aina tatu za solar panels ingawa nyingi bado zipo kwenye maabara kwa ajili ya utafiti.
Mono ni nzuri sana na ufanya kazi kwa ufanisi katika maeneo ambayo upata mwanga wa moja kwa moja kutoka juani bila kupitia kwenye mawingu (direct/beam solar radiation). Poly na Amorphous ni nzuri kwenye maeneo ambapo mwanga wa jua ni hafifu kutokana na ukungu ama mawingu (diffuse solar radiation).
Kwa hiyo, kumshauri mtumiaji wa Kibosho atumie Mono nikutaka kumfanya 'kuzika' hela zake za manunuzi ya panel. Wa Kibosho atumie amorphous ama poly panels. Hata hivyo mbali na bei kuwa haijachangamka kwa panels hizi zina changamoto zake zinazohimilika.