Fahari ya kusini
JF-Expert Member
- Nov 26, 2022
- 427
- 1,668
Nimeoa, ndoa yangu ina miezi 6 lakini mke wangu kaondoka nyumbani na kaniacha anadai talaka ananishutumu kuwa nina mahusiano na Mama yangu. Nyumbani kwetu tumezaliwa watatu na wote ni wakiume, mimi ndiyo mtoto wa kwanza, nina miaka 33 na nina kazi nzuri tu. Muda wote wa maisha yangu nimekuwa nikiishi na Mama yangu, yeye ndiye kila kitu kwangu, baba yupo lakini muda mwingi yuko bize na kazi, anafanya kazi mkoa mwingine hivyo maisha yangu kumuona Baba ni mara moja kwa mwaka na hata akiwepo hahangaiki na sisi.
Makuzi yangu yote ni mimi na mama, kila kitu changu namuambia Mama yangu, amekuwa kama rafiki yangu, sina marafiki wengine iwe ni wa kiume au wa kike, wengi ni ile kuonana tu ila mambo yangu ya ndani yote huwa namuambia Mama yangu na anajua kila kitu changu. Kwa jinsi nilivyozoea na Mama yangu sina siri naye, tangu nikiwa mdogo naweza kuvua nguo mbele ya mama yangu, naweza kuoga nikatoka bafuni narudi chumbani namkuta amelala kitandani kwangu basi navua nguo uchi kabisa naniona.
Wakati mwingine hata nikiwa naumwa labda nina fangasi sehemu za siri anakagua na kunishauri. Hatujawahi kuwa na mahusiano wala yeye Mama havui nguo mbele yangu, anaweza kulala chumbani kwangu labda usiku lakini hatuvuki mipaka najua ni Mama yangu na namheshimu. Mimi kwangu ni kawaida, wadogo zangu wao hawataki hicho kitu ni kama wanamuonea aibu mama ila kwangu sioni shida kwani ni mama yangu, kama amenizaa, akanitawaza, akaniogesha nikiwa uchi sioni kama ni kitu cha ajabu.
Nilipooa mpango ulikuwa ni kuishi kwa mama na nilimuambia mke wangu kuwa kamwe siwezi kuishi mbali na Mama yangu hivyo kama hawezi kuishi na Mama yangu mimi siwezani naye. Aliniambia hana shida yoyote kwani mama alimpendea na walikuwa karibu. Baada ya ndoa nilikaa kwa mama kwa miezi miwili tulikuwa vizuri ila baadae tukahama kwani nilipata kazi sehemu nyingine, ni hapa hapa Dar lakini kutokana na umbali ikabidi tukapangishe. Sasa mama huwa na kawaida ya kuja mara kwa mara hasa weekend analala au anakaa hata wiki kwani yeye ana biashara zake hivyo hakuna mtu wa kumsumbua.
Shida inakuja hivi, kila akija mke wangu anakasirika, yaani namuona hana raha namuuliza shida nini haniambii. Kuna siku nilikuwa bafuni naoga, Mama akaingia chumbani na kukaa, mke wangu akawa anamuambia Mama subiri kidogo fulani anaoga, mama akacheka akamuambia kwani kuna kipya sijakiona. Basi mimi nikatoka hivyo hivyo nikiwa uchi nikajifuta na kupaka mafuta mbele ya mama na mke wangu kabla sijamaliza mke wangu alitoka huku akilia.
Mimi na Mama wote tulishangaa kwani yeye alishawahi kuniona uchi na hata Mama yangu ameniona uchi sikuona kitu cha ajabu. Kuna siku nyingine mke wangu aliingia chumbani akanikuta niko uchi navaa nguo na Mama yangu kaka kitandani tunaongea. Aliongea kwa hasira na kutoka tena huku akilia! Mama alikasirika kidogo kwani aliona kama dharau, hivyo baada ya hapo alimuambia hapendi hiyo tabia yeye akija chumbani anaondoka kumuacha. Mimi pia nilikasirika lakini cha ajabu mke wangu aliondoka siku hiyo hiyo akidai kuwa nina mahusiano na Mama yangu hivyo hataki tena hii ndoa, ananidai sana talaka na hataki kuwa na mimi.
Tayari tuna mtoto mmoja ambaye tulimpata kabla ya ndoa, sitaki mtoto wangu kulelewa na mwanaume mwingine. Sitaki kuwa mbali na mtoto wangu ila sijui ni kwa namna gani nitaishi na mwanamke ambaye hata hampendi Mama yangu. Ni kitu gani cha ajabu kwa mama aliyenizaa na kunilea kuniona uchi.
Nimejaribu kumuelewesha kuwa ni mambo ya kawaida mama yangu hata nikiumwa ndiye ananihudumia lakini yeye hataki kashikilia msimamo kuwa natembea na Mama yangu. Naomba ushauri, hivi huyu ni mtu anayenipenda kweli au anatafuta sababu tu ya kuniacha, kuna ubaya gani mtu kuwa huru na Mama yako? Nisaidie maana sioni tatizo, Mama yangu tunaheshimiana sana. Maka kaniambia kama hataki aondoke lakini bado nampenda niko tayari kumsamehe kama akiomba msamaha lakini hataki nifanye nini?