Foundation
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 1,420
- 611
Ni kweli mkuu, japo ameuliza kama yeye Njaa bado nina imani kupitia uzi wake wengi watafaidika.
Mkuu JF ni kisima cha burudani,elimu nk
Last edited by a moderator:
Ni kweli mkuu, japo ameuliza kama yeye Njaa bado nina imani kupitia uzi wake wengi watafaidika.
Naunga mkono hoja...Mkuu JF ni kisima cha burudani,elimu nk
Wakuu...., asanteni sana kwa ushauri. Nimefanikiwa kupata design kadhaa za paa na ushauri mwingi sana. Ukweli ni kwamba hizo hela ni ndogo, nimefanikiwa kupata bati za migongo midogo 120 kutoka jeshini (rangi ya blue). Fundi ameniambia niongeze walau million 3 ili nyumba imaliziwe na kuezekwa. Kwa bahati nzuri million 3 zimepatikana na sasa mambo yanaendelea. Nitawaletea mrejesho wa nyumba baada ya kuezekwa ndani ya wiki 2. Siwezi kutaja majina ya wote walio toa ushauri na wale walio ni-PM. JF daima...Thanks....
nitumie upana wa nyumba na urefu.tuma kwenye 0787803577
niidesign ktk archcard then nikupe hesabu kamili mkuu.
Mkuu naomba unieleze kwa kina jinsi ya kuchana mbao za mnazi hatua kwa hatua.bado sijakupataMkuu JF ni sehemu ya kupeana ujuzi na uzoefu hiyo pesa 4.2m ni nyingi sana na chenji inabaki,tafuta mbao za minazi na utafute mtu wa kukata mbao za mnazi kwa nyumba hiyo minazi 16 inatosha zunguka sehemu mbali mbali hapa dsm ukikuta wanaangusha mnazi waombe huo mnazi,kukata kwa mashine mnazi mmoja kuchonga mbao ni sh 4000 kwahiyo gharama za mbao za minazi 64,000/= Kuna wengine wanauza mnazi kwa 10,000 wengine hawauzi ukikuta wameukata wanatoa bure so tuassume total 220,000/=plus usafiri 80,000/= Nunua bati za ALAF zile ngumu za 20,000/= kwahiyo nyumba yako nlivyoangalia zinaingia kama 60 tuassume 80 kwa design yeyote(Total 1.6m) kuna mafundi wazuri sana wa bei rahisi design yeyote ya paa na ufundi kujenga wanafanya kwa 600k) mpaka sasa tushatumia 2.5m tuweke 100k ya usafiri 2.6m! Hapo utabidi uongeze matofali kama 100 kwa ajili ya kuzungusha juu,utahitaji waya kwa ajili ya kushikia fenzi tuassume makolokolo yote hayo laki4 pamoja na kununua ndoo za rangi kwa ajili ya kupaka hayo mabati yalete muonekano mzuri ila rangi ya bati uipake baada ya miezi kama miwili hivi baada ya kuzijengea then 1.2m inabaki kwa mambo mengine humu JF kuna wengine wanakatisha tamaa na bei za ajabu ajabu! Mbao ya mnazi ni miaka 100 hailiwi na mdudu yeyote! Na ndio maana kitanda cha mbao ya mnazi bei yake haishikiki 77 walikuwa wanauza 1.2m
hiyo mbao ya mnazi sasa, kuipata ni ishu, huo mnazi una umri gani!?
Asante sana mkuu King Kong III kwa hakika nimejifunza kitu cha maana sana kuhusu mbao ya mnazi, sikujua kuwa inafaa kwa namna hiyo! Zanzibar Spices mchango wako ni madini.