Zingatia yafuatayo kabla hujaamua kununua bati la kuezeka nyumba yako

munirah

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
551
218
Kabla hujaingia kwenye kundi la walio wengi wanaolalamika kuhusu ubora wa bati katika kutoboka,kushika kutu, kupauka kwa sababu ya maamuzi yao wenyewe au kupotoshwa na wauzaji wenye tamaa ya pesa, Pata #ElimuNaUelewa Kuhusu mambo makuu matatu unayoweza kuyazingatia kabla hujaamua kununua Bati la kuezeka nyumba yako.

1. Matirio/Contents
Bati linaundwa kwa madini maalum kama Aluminium, Zinc na Silicon. Bati lenye mjumuiko wa madini mengi ya Aluminium na Zinc ndilo linapendekezwa kutumika kuezekea nyumba za kuishi kutokaka na uimara wake wa kuhimili hali tofauti za hewa, Gharama lakini pia kuwa na kipindi kirefu cha kuwepo bila kupoteza ubora wake toka lilipoanza kutumika.

Japo ni ngumu kupima kwa macho lakini ni sahihi ukimuuliza anayekuuzia juu ya masuala kama haya muhimu ili ufanye maamuzi sahihi.

2. Geji/Gauge
Huu ni unene wa bati/Thickness unapimwa kwabkifaa maalum micrometer screw gauge ambayo tunayo kuweza kumsaidia mteja kutofautisha geji 30 na 28 na zingine kama 26,24,22

Geji 28 ni bora zaidi kwa uezekaji wa nyumba za kuishi na gharama yake ni kubwa zaidi ya geji 30. Utajuaje hii ni gauge 30 au 28?

Ni ngumu kujua geji kama huna uzoefu na hapa panahitaji umakini mkubwa. Geji imara inapendekezwa kwa uezekaji wa nyumba zilizokaribu na Pwani ya bahari kwani husaidia zisitoboke na kupata kutu haraka.

Sasa basi kwakuwa ni ngumu kujua geji kwa macho au kwa kushika, RBS Mabati (Instagramu) tunatumia kifaa maalum kuweza kupima sampuli mbalimbali na kumwezesha mteja wetu kutofautisha geji na kufanya maamuzi sahihi ya kununua bati lililo na ubora alioutarajia.

3. Uso wa bati /Surface
Katika kutofautisha uso wa bati unaweza kufanya hivyo kwa kushika kwa mkono tu na kuona utofauti ni kutumia zana yoyote.

a. Mtelezo/Glossy (Rangi inateleza)

b. Chenga chenga/Matte (Ina rangi yenye vipele na Mng'ao madhubuti, imeongezwa nakshi na ubora zaidi katika rangi) Hazipauki haraka na huwa na muonekano wa kuvutia.

SIFA NYINGINE ZA BATI AMBAZO NI ZA JUMLA NI KAMA.

1. Muundo/Profile
Hapa tunazungumzia Migongo midogo au mipana na Muundo wa kigae.
Muundo wa bati unaweza kubeba sifa zote kuu 3 za bati zinazoelezea UBORA wake kama ilivyoelezwa hapo juu.

2. Rangi/Colours
Kuna zaidi ya rangi 9 za bati na hii inampa mteja uhuru wa kuchagua rangi apendayo lakini pia ni muhimu kuzingatia "code" ya rangi ya mtaa wako kama Kuna mapendekezo

Mada ya Ubora wa rangi za bati ni Mada inayojitegemea zaidi maana ni pana mno tunaweza kuijadili kwa muda wake. Lakini rangi za bati zinatakiwa kuzingatia standard za kimataifa kwa kipimo cha AZ150. Ni lazima mzalishaji azingatie ujazo wa rangi (unene wa rangi) kwenye bati.

3. Vipimo/Size
Upana wa bati unaweza kuwa 80cm hadi 110 cm.
Upana wa bati hauathiri ubora wa bati husika isipokuwa unaathiri zaidi bei na idadi ya bati utakazohitajika kulipia. Hii ni kusema upana wa bati ukiwa mdogo basi bei yake itakuwa ndogo na utanunua bati nyingi kufunika nyumba yako ukilinganisha na upana mkubwa ambayo utalipa bei kubwa lakini pia utapunguza idadi ya bati utakalofunika eneo husika. Mwisho aliyechagua upana mkubwa na aliyechagua mdogo wanaezeka nyumba zao bila madhara katika ubora wa bati.

4. Bei/price na Makadirio

Bei za bati unaweza kuzitenga katika makundi makuu matatu.

a. Bei za juu - Ubora wa Juu kuanzia 28G yaani 0.35mm. Zina Warrant ya zaidi ya miaka 10. Hizi sasa ndo bati za kuezeka kwa ubora kwa nyumba za kuishi. Wakati huo Geji 26 na 24 zikiwa bora zaidi hutumika kuezeka viwanda, magodauni au majengo makubwa kwa sababu ya unene na uimara wake.

b. Bei za Kati - Ubora wa Kati kuanzia 30G warrant ya zaidi ya miaka 5. Hizi tunapendekeza zaidi kutumika kwa mtu anayewaza ubora zaidi badala ya bei. Kumbuka hapa tunazungumzia unene wa 0.25mm yaani geji 30 halisi ambayo unaweza kununua ikiwa Mtelezo/Glossy au Chenga chenga/Matte.

c. Bei za Chini - Ubora wa chini/duni ofa nyingi na warrant ndogo au warrant ya mdomo. Hizi mara nyingi huuzwa kwa bando yaani pisi 16. Zinatofautiana ubora kiwanda na kiwanda. Yafaa kuwa makini kuchagua. Mara nyingi bati hizi hutumika kwa matumizi ya muda mfupi kama kuweka uzio katika miradi ya serikali au majengo makubwa. Unene wake ni 0.2mm.

RBS Mabati tunawasaidia wateja wetu kuweza kufanya Makadirio ya idadi ya bati watakazotumia kuezekea na tunawapa bajeti ya mabati kulingana na aina ya Matirio, Geji, Uso wa bati na Upana na Urefu wa bati.

Hii inawasaidia wateja wetu wasiweze kupewa makadirio makubwa au madogo na baadhi ya mafundi ambao hawana uzoefu au wasio waaminifu katika tasnia hii ya UEZEKAJI.

USIFANYE MAJARIBIO KATIKA NYUMBA YAKO. Chagua huduma toka kwa wataalamu waaminifu na wenye uzoefu katika sekta ya bati ili usiwe miongoni kwa wanaojutia kununua mabati bila kufanya UTAFITI.
 
Watu wa karibu na bahari walikua waendelee kutumia tu mabati ya ASBESTOS ila watu wanojifanya kujua mambo wakaingilia kati wakajidai mabati ya ASBESTOS yanasababisha kensa ilimradi wauze mabati yao tu

ASBESTOS sijui kama yanapatikana tena TZ hii ukiezeka ASBESTOS mpka kirembwe kinakuja kutumia nyumba ya babu yake
 
Kabla hujaingia kwenye kundi la walio wengi wanaolalamika kuhusu ubora wa bati katika kutoboka,kushika kutu, kupauka duma toka kwa wataalamu waaminifu na wenye uzoefu katika sekta ya bati ili usiwe miongoni kwa wanaojutia kununua mabati bila kufanya UTAFITI.
Si useme tu mnauza mabati, mbona uzi unaohusu elimu ya mabati upo katika jukwaa hili tena umeelezewa kitaalam sana
 
Kwani hapa JF haturuhusiwi kuweka uzi juu ya uzi? Je unadhani unaweza kuongelea mabati ukamaliza kila kitu au ww umeamua tu kuwa negative. Pole sana ndugu. Sisi tunashauri, tunasaidia wateja pia kupata bidhaa husika kwa uaminifu na katika rates halisi. Acha wivu wa kijinga
 
Watu wa karibu na bahari walikua waendelee kutumia tu mabati ya ASBESTOS ila watu wanojifanya kujua mambo wakaingilia kati wakajidai mabati ya ASBESTOS yanasababisha kensa ilimradi wauze mabati yao tu

ASBESTOS sijui kama yanapatikana tena TZ hii ukiezeka ASBESTOS mpka kirembwe kinakuja kutumia nyumba ya babu yake
Umeongea vema. Biashara ina vita vya kila aina. Propaganda nayo imetawala, ni muhimu mteja kuwa mtulivu na kufanya machaguzi sahihi na kuzingatia ubora
 
Asante kwa Bandiko la Ujenzi Mkuu.

WANA JF TUNAKUSHUKURU, NA UBARIKIWE.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Tanzania Ndiyo Imejaa Maajabu Na Uhovyo Mwingi Kama Vile Hakuna Mamlaka Zinahusika Na Mabati. Tembea Mikoani Utaona Aibu Tupu Hass
Hizi Kampuni Zinzotengeneza Bati Kwenye Upande Wa Rangi Hawajui Kazi

Mapaa Tele Ya Nyumba Yamepauka Kama Vile Hazikuwa Bati Za Rangi
Wahuni Ni Wengi Sana Bora Ununue Bati Lisilo La Rangi Mbele Huko Utapaka
Kuliko Kuuziwa Bati Baadaye Zinapauka Mpaka Aibu
 
Ni vema kujua rangi zote hupauka lakini inategemea na brand. Ukiingia sokoni kwa kudhani rangi hazipauki utakuwa unafanya makosa. Na tena ukiingia sokoni kwa kuteka bidhaa mteremko wa bei basi utaangukia pua zaidi. Cheap is expensive always. Nunua uhalisia wa bei na warrant.
 
Kwani hapa JF haturuhusiwi kuweka uzi juu ya uzi? Je unadhani unaweza kuongelea mabati ukamaliza kila kitu au ww umeamua tu kuwa negative. Pole sana ndugu. Sisi tunashauri, tunasaidia wateja pia kupata bidhaa husika kwa uaminifu na katika rates halisi. Acha wivu wa kijinga
Kumbe simba dumu gauge 30 zinazokaa 16 kwa bando ni za kiwango cha chini?
 
Tanzania Ndiyo Imejaa Maajabu Na Uhovyo Mwingi Kama Vile Hakuna Mamlaka Zinahusika Na Mabati. Tembea Mikoani Utaona Aibu Tupu Hass
Hizi Kampuni Zinzotengeneza Bati Kwenye Upande Wa Rangi Hawajui Kazi

Mapaa Tele Ya Nyumba Yamepauka Kama Vile Hazikuwa Bati Za Rangi
Wahuni Ni Wengi Sana Bora Ununue Bati Lisilo La Rangi Mbele Huko Utapaka
Kuliko Kuuziwa Bati Baadaye Zinapauka Mpaka Aibu
Hakuna bati isiyopauka.
 
Ni vema kujua rangi zote hupauka lakini inategemea na brand. Ukiingia sokoni kwa kudhani rangi hazipauki utakuwa unafanya makosa. Na tena ukiingia sokoni kwa kuteka bidhaa mteremko wa bei basi utaangukia pua zaidi. Cheap is expensive always. Nunua uhalisia wa bei na warrant.
Sasa kama rangi zote hupauka, brand inahusikaje hapo
 
Kabla hujaingia kwenye kundi la walio wengi wanaolalamika kuhusu ubora wa bati katika kutoboka,kushika kutu, kupauka kwa sababu ya maamuzi yao wenyewe au kupotoshwa na wauzaji wenye tamaa ya pesa, Pata #ElimuNaUelewa Kuhusu mambo makuu matatu unayoweza kuyazingatia kabla hujaamua kununua Bati la kuezeka nyumba yako.

1. Matirio/Contents
Bati linaundwa kwa madini maalum kama Aluminium, Zinc na Silicon. Bati lenye mjumuiko wa madini mengi ya Aluminium na Zinc ndilo linapendekezwa kutumika kuezekea nyumba za kuishi kutokaka na uimara wake wa kuhimili hali tofauti za hewa, Gharama lakini pia kuwa na kipindi kirefu cha kuwepo bila kupoteza ubora wake toka lilipoanza kutumika.

Japo ni ngumu kupima kwa macho lakini ni sahihi ukimuuliza anayekuuzia juu ya masuala kama haya muhimu ili ufanye maamuzi sahihi.

2. Geji/Gauge
Huu ni unene wa bati/Thickness unapimwa kwabkifaa maalum micrometer screw gauge ambayo tunayo kuweza kumsaidia mteja kutofautisha geji 30 na 28 na zingine kama 26,24,22

Geji 28 ni bora zaidi kwa uezekaji wa nyumba za kuishi na gharama yake ni kubwa zaidi ya geji 30. Utajuaje hii ni gauge 30 au 28?

Ni ngumu kujua geji kama huna uzoefu na hapa panahitaji umakini mkubwa. Geji imara inapendekezwa kwa uezekaji wa nyumba zilizokaribu na Pwani ya bahari kwani husaidia zisitoboke na kupata kutu haraka.

Sasa basi kwakuwa ni ngumu kujua geji kwa macho au kwa kushika, RBS Mabati (Instagramu) tunatumia kifaa maalum kuweza kupima sampuli mbalimbali na kumwezesha mteja wetu kutofautisha geji na kufanya maamuzi sahihi ya kununua bati lililo na ubora alioutarajia.

3. Uso wa bati /Surface
Katika kutofautisha uso wa bati unaweza kufanya hivyo kwa kushika kwa mkono tu na kuona utofauti ni kutumia zana yoyote.

a. Mtelezo/Glossy (Rangi inateleza)

b. Chenga chenga/Matte (Ina rangi yenye vipele na Mng'ao madhubuti, imeongezwa nakshi na ubora zaidi katika rangi) Hazipauki haraka na huwa na muonekano wa kuvutia.

SIFA NYINGINE ZA BATI AMBAZO NI ZA JUMLA NI KAMA.

1. Muundo/Profile
Hapa tunazungumzia Migongo midogo au mipana na Muundo wa kigae.
Muundo wa bati unaweza kubeba sifa zote kuu 3 za bati zinazoelezea UBORA wake kama ilivyoelezwa hapo juu.

2. Rangi/Colours
Kuna zaidi ya rangi 9 za bati na hii inampa mteja uhuru wa kuchagua rangi apendayo lakini pia ni muhimu kuzingatia "code" ya rangi ya mtaa wako kama Kuna mapendekezo

Mada ya Ubora wa rangi za bati ni Mada inayojitegemea zaidi maana ni pana mno tunaweza kuijadili kwa muda wake. Lakini rangi za bati zinatakiwa kuzingatia standard za kimataifa kwa kipimo cha AZ150. Ni lazima mzalishaji azingatie ujazo wa rangi (unene wa rangi) kwenye bati.

3. Vipimo/Size
Upana wa bati unaweza kuwa 80cm hadi 110 cm.
Upana wa bati hauathiri ubora wa bati husika isipokuwa unaathiri zaidi bei na idadi ya bati utakazohitajika kulipia. Hii ni kusema upana wa bati ukiwa mdogo basi bei yake itakuwa ndogo na utanunua bati nyingi kufunika nyumba yako ukilinganisha na upana mkubwa ambayo utalipa bei kubwa lakini pia utapunguza idadi ya bati utakalofunika eneo husika. Mwisho aliyechagua upana mkubwa na aliyechagua mdogo wanaezeka nyumba zao bila madhara katika ubora wa bati.

4. Bei/price na Makadirio

Bei za bati unaweza kuzitenga katika makundi makuu matatu.

a. Bei za juu - Ubora wa Juu kuanzia 28G yaani 0.35mm. Zina Warrant ya zaidi ya miaka 10. Hizi sasa ndo bati za kuezeka kwa ubora kwa nyumba za kuishi. Wakati huo Geji 26 na 24 zikiwa bora zaidi hutumika kuezeka viwanda, magodauni au majengo makubwa kwa sababu ya unene na uimara wake.

b. Bei za Kati - Ubora wa Kati kuanzia 30G warrant ya zaidi ya miaka 5. Hizi tunapendekeza zaidi kutumika kwa mtu anayewaza ubora zaidi badala ya bei. Kumbuka hapa tunazungumzia unene wa 0.25mm yaani geji 30 halisi ambayo unaweza kununua ikiwa Mtelezo/Glossy au Chenga chenga/Matte.

c. Bei za Chini - Ubora wa chini/duni ofa nyingi na warrant ndogo au warrant ya mdomo. Hizi mara nyingi huuzwa kwa bando yaani pisi 16. Zinatofautiana ubora kiwanda na kiwanda. Yafaa kuwa makini kuchagua. Mara nyingi bati hizi hutumika kwa matumizi ya muda mfupi kama kuweka uzio katika miradi ya serikali au majengo makubwa. Unene wake ni 0.2mm.

RBS Mabati tunawasaidia wateja wetu kuweza kufanya Makadirio ya idadi ya bati watakazotumia kuezekea na tunawapa bajeti ya mabati kulingana na aina ya Matirio, Geji, Uso wa bati na Upana na Urefu wa bati.

Hii inawasaidia wateja wetu wasiweze kupewa makadirio makubwa au madogo na baadhi ya mafundi ambao hawana uzoefu au wasio waaminifu katika tasnia hii ya UEZEKAJI.

USIFANYE MAJARIBIO KATIKA NYUMBA YAKO. Chagua huduma toka kwa wataalamu waaminifu na wenye uzoefu katika sekta ya bati ili usiwe miongoni kwa wanaojutia kununua mabati bila kufanya UTAFITI.
Hili nalo nichangamoto unaweza ukawa unajua vitu vingi lakini muuzaji akaupiga sifa nyingi zinahitaji utaalamu mfano kujua geji mpaka upime ni ishu ila kwa uzoefu nilioupata bora ununue bati za ALAF au Ando hawa kidogo wanaaminika kwenye ubora.
 
Kitu ambacho nilikuwa sikojui kwenye bati kumbe bati za geji 30 kumbe kuna bati za 30GA na 30GB na hata ubora ,uzito na bei ni tofauti kabisa
 
Asante mkuu Munirah, kwahiyo kwa ushauri wako ni brand gani ya mabati ndio unashauri mtu anunue??
 
Back
Top Bottom