Ushauri: Nitumie bati la mgongo mpana au simba dumu la geji 28?

Ushauri: Nitumie bati la mgongo mpana au simba dumu la geji 28?

SAWEBOY

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2011
Posts
241
Reaction score
175
Waungwana wana JF,

Mwenzio nipo hapa mbili haikia...na wala tatu haisogei...naomba ushauri wenu maridhawa kabisa ili mwisho wa siku nisijuitie uamuzi wangu.

Ni hivi...nina boma langu la nyumba nataka kuezeka (Four rooms each with private toilet and bathroom, public toilet inside and outside, kitchen, sitting room and dinning room, and office/library). Sasa mwanzo niliwaza niezeke kwa kutumia bati la migongo mipana haya ya kisasa kutoka Alaf. Lakini kwa sasa nimeona bei ya bati hilo la migongo mipana itanigharimu karibu sh. milion 8 bati peke yake. Hapo bado fundi, mbao, misumari n.k

Mwisho wa siku, nafikiria sasa kununua bati la Alaf lakini la simba dumu...la geji 28 ambapo kwa bati za kutosha nyumba wastani itagharimu kama milion 3 na nusu. ukijumlisha mbao+fundi+misumari and any other cost haiwezi kuzidi milioni 10.

Mkononi nina milioni 20, nafikiria nikitumia hilo la migongo mipana hiyo 20 mill itaisha yote, but nikitumia hili la simba Dumu...naweza save milion 10 ambayo inaweza fanya kazi zingine au nikaweka akiba.

Je wadau kwa ushauri wenu kadiri ya uzoefu wenu katika mambo ya ujenzi mnanishauri nini? nitumie bati la migongo mipana kuendana na fashion? au nitumie tu bati la simba dumu la geji 28 kuokoa gharama?

Natanguliza shukrani kwa ushauri wenu. ASANTENI.
 
Kama unataka Bati za Rangi Nunua za Migongo Midogo lakin zile zilizopigwa rang elfu 24 kwa Geji 28 kama sijakosea sina uhakika na eneo ulilopo na House itakaa vzr tu.....Hongera sana Mjini hakuna Baba Mwenye gari au Mwenye Kitambi yupo mwenye nyumba na ndo wanaume wa mjini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom