Msaada: Natafuta mwalimu wa vyombo vya muziki-Morogoro

Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
262
217
Habari?

Wakuu msaada tafadhali. Nina vijana (watoto wangu) ambao napenda wajifunze kupiga vyombo vya muziki kama kinanda (keyboard) na Guitar kwa kuanzia. Tafadhali anayemjua mwalimu ama shule ninayoweza kuwapeleka wanangu hapa Morogoro mjini anipe namna ya kuwapata.

Shukrani
 
Kama wewe ni mkristo, wape connection watoto wako na kwaya ya kanisa; believe me that hakuna walimu wazuri wa muziki kama wanaopatikana kwenye hizo kwaya. Hapo watoto wako watajifunza kupiga guitar, keyboard, drums nk. Hata kwenye kuimba kanisani wanaanza kufundishwa kuanzia kwenye basics
 
Nina likizo, napiga kinanda na base gitaa. Tangaza offer ili nije within two weeks watajua
 
Kama wewe ni mkristo, wape connection watoto wako na kwaya ya kanisa; believe me that hakuna walimu wazuri wa muziki kama wanaopatikana kwenye hizo kwaya. Hapo watoto wako watajifunza kupiga guitar, keyboard, drums nk. Hata kwenye kuimba kanisani wanaanza kufundishwa kuanzia kwenye basics
Asante kwa ushauri, mimi ni mkristo ila kanisani kwangu hakuna kwaya wala mwalimu wa mziki.
 
Upo wapi? Morogoro?
Mkuu ukitaka wawe wazuri wala usiwapeleke au kuwapa hawa walimu wakukariri ambae anamfundisha mtoto kukariri pia ukimwambia hata iyo uliocheza ni minor anakuuliza minor ndio nn?

Tafuta mwalimu atakae wafundisha kwa kusoma noten kisha maujuzi watajiongezea kadri wanavyokuwa.

Ungekuwa dar ninheku propozia shule ila morogoro sina uhakika.

Wapiga kinanda wa kikatoliki watafute walau hawa wanajua piano tena kwa note tatizo walilonalo wengi wanapiga style moja si watundu.

Walokole wengi hawajui note na wanapiga code tatu tu kwaajili ya mapambio hapa nao kazi kweli kweli.

Wasabato wengi wanacheza na accompaniment piano hawawezi hapa napo si vema mtoto akaanza na accompaniment atakuwa mremavu. Ila ukikuta msabato anaejua note na piano huyo bana usimwache wanajuaga kuchezea sana kwakuwa mziki wao upo katika maadhi mbalimbali, kama vile Jazz, country, RnB nk

Sasa baada ya kukuonesha hayo yote na kwakuwa Tz tunamis sana walimu wa muziki wajuzi. Tafuta mwl wa note, ukikosa tafta mkatoliki wengi wanajua note, akisha wafundisha kusoma staff note. Wapeleke kwa msabato awape sasa utundu flan amaizing wakuchezea piano.

Mwisho kabisa, nunua keyboard ndogo home kwako, download youtube masomo ya kujifunza piano for beginners. Wape mazoezi.

Gitaa sitazungumzia maana nilianzaga tu nikaacha sina uzoefu nalo. Thou badae nitajifunza pia.
 
mkuu kwa dar ni shule gani wanafundisha? Natamanigi sana nijue kupiga hivi vyombo
 
Mkuu, shukrani kwa maelezo! Nitajaribu kuwatafuta hawa waheshimiwa pamoja na kuwa ingekuwa rahisi nikimpata mtu ambaye anafundisha kuliko kumuomba ambaye hafundishi. Keyboard, guitar na organ ninavyo, shida ni waalimu. Nimedownload video za kujifunzia lakini inakuwa ngumu kwa watoto kujifunza nadhani wanahitaji mwalimu atakayewaelekeza vizuri kwa vitendo. well, thank you a million.
 
Habari?

Wakuu msaada tafadhali. Nina vijana (watoto wangu) ambao napenda wajifunze kupiga vyombo vya muziki kama kinanda (keyboard) na Guitar kwa kuanzia. Tafadhali anayemjua mwalimu ama shule ninayoweza kuwapeleka wanangu hapa Morogoro mjini anipe namna ya kuwapata.

Shukrani
Mimi sitanii kwani Nape alikuwa anatuburudisha mlimani na codian ya mzee Mnauye. Anaweza na hivi ndo wizara yake. Halafu ulizia kwa vijana wa band ya Fr. Kanuti pale karibu na general hospital Moro kwenye late 80s walikuwepo. Sitanii.
 
Nami napenda sana kujifunza hasa kinanda. Nikiwa kanisani nikiona inavyopigwa na wanaojua huwa nafifahi sana na ninaona kama kweli hiyo ibada imekaa poa sana.
 
Habari?

Wakuu msaada tafadhali. Nina vijana (watoto wangu) ambao napenda wajifunze kupiga vyombo vya muziki kama kinanda (keyboard) na Guitar kwa kuanzia. Tafadhali anayemjua mwalimu ama shule ninayoweza kuwapeleka wanangu hapa Morogoro mjini anipe namna ya kuwapata.

Shukrani
Nitafute nikuunganishe na jamaa mmoja mkipatana atakusaidia sana anajua km vyombo vitano including hivyo...
 
nilisikia tangazo la wanaotaka kujifunza music na vyombo vya music kanisa katoliki la parokia ya modeko morogoro,nenda hapo modeko kanisani kaulizie.
 
Asante kwa taarifa mkuu, nitafuatilia nione!
 
Back
Top Bottom