Msaada: Naondoaje uraibu wa kusikiliza muziki?

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,684
Yaani hata nikisikia mlio wa ambulance tu basi akilini naisikia 'Brigedier Sabari' ya alpha blond,

Yaani nikisikia tu neno 'mpenzi' basi haraka kichwani huja wimbo 'Sanura' wa Tongolanga kwenye kile kipande kinachosema,

''Unachonishangaza mpeenzi, huzoeleki;

Huwa unashindwa wapi zaiidi, tele kwa tele;

Siku ya kwanza mapenzi yetu na leo yote ni saawa;

Mengiii mageni nayaona kwako, we una kipaji mamaaa".

Nikisikia tu neno 'what' basi haraka huja kichwani nyimbo kadhaa za dmx zikiwemo "what's ma name, what these they want" n.k

Nikisikia tu neno 'hela' basi haraka kichwani huja ule wimbo wa jafarai uitwao "toa hela".

Nikisikia tu neno 'salamu au wazazi' basi haraka huja ule wimbo wa "Salaam baba na mama" wa wale zilipendwa.

Nipo hivyo karibu kila wakati hadi funga yangu inatetereka, nafanyaje kujitoa?!!!
 
Shetani kakuelemea,zidisha ibada. Miziki inakuwa ndiyo falsafa yako ya maaisha, inakuwa kipimo cha maamuzi,unakuwa mtumwa. Namuomba Allah akunusuru, nilikuwa huko najua,kila jambo nilikuwa napima kwa kufananisha na nyimbo fulani japo yule muimbaji maisha yake yaliharibika
 
Nipo hivyo karibu kila wakati hadi funga yangu inatetereka, nafanyaje kujitoa?!!!
Hutoboi mkuu bila kudetox na nyimbo za deen yako. Kama Muslim, detox na mawaidha. Kama ni Christian do the same.

Mimi nikisikia ka wimbo asubuhi, either mtu kaimba au nimeusikiliza mwenyewe. Huo wimbo utaniganda almost siku nzima. Nikitaka kuutoa, nasikiliza zangu gospel.
 
Tzgospel Radio sikiliza hapo
 
Yaani hata nikisikia mlio wa ambulance tu basi akilini naisikia 'Brigedier Sabari' ya alpha blond,

Yaani nikisikia tu neno 'mpenzi' basi haraka kichwani huja wimbo 'Sanura' wa Tongolanga kwenye kile kipande kinachosema,

''Unachonishangaza mpeenzi, huzoeleki;

Huwa unashindwa wapi zaiidi, tele kwa tele;

Siku ya kwanza mapenzi yetu na leo yote ni saawa;

Mengiii mageni nayaona kwako, we una kipaji mamaaa".

Nikisikia tu neno 'what' basi haraka huja kichwani nyimbo kadhaa za dmx zikiwemo "what's ma name, what these they want" n.k

Nikisikia tu neno 'hela' basi haraka kichwani huja ule wimbo wa jafarai uitwao "toa hela".

Nikisikia tu neno 'salamu au wazazi' basi haraka huja ule wimbo wa "Salaam baba na mama" wa wale zilipendwa.

Nipo hivyo karibu kila wakati hadi funga yangu inatetereka, nafanyaje kujitoa?!!!
Kwahiyo hata mlio wa itv saa mbili usiku unaweza kucheza
 
Nyimbo zinaweza kukufanya kuwa ZOBA jitafutie vitu positive uanze kufatilia Kama kusoma vitabu n.k

Kuandika
Kusoma Quruan

Kutazama mawaidha

Kuwa karibu Sana Mungu wako nyimbo zenye kusifu ngono na pombe ni uchafu.
 
Kwani unapata madhara gani?? Nikajua ni mimi tu, nasikiliza music with memories..kila wimbo bas nitakumbuka nilikuwa mahali fulan na mwaka fulan, either kama mtu alikuwa anaupenda huo wimbo basi nitamkumbuka, vibuti nilivyotembezewa viko kwenye memory ya muziki, inafika muda huwa nakwepa kusikiliza oldies!
Kuna nyimbo hata sizipendi, siwezi kuzitafuta hata zikiplay accidentally basi nitaziskip.
Mbali na yote, without music,life would be a mistake!
 
Ujitoe ili iweje au ili ufanye nini ? Lazima akili iwe occupied na kitu fulani sasa wewe unataka replacement iwe nini ?

To each their Own...
 
Muziki Ni sabuni ya roho bt remember too much of something is poison.

Tafuta ishu ya kufanya usikae kizembe unaonekana una- idol Sana mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom