Msaada: Naomba sample ya barua ya likizo isiyo na malipo

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,477
35,352
Habari za usiku waungwana?

Ninataka kupumzika kazi kwa muda wa angalau mwaka mmoja au miwili.

Kuna jambo nataka kulifanya la kibinafsi.

Mimi ni mtumishi wa serikali.

Aliyewahi kuomba likizo isiyo na malipo au anayefahamu kwa undani hili jambo anipe mwanga.

Thanks
 
Kulia juu address yako
Kushoto chini ya katibu wa wizara
K.K katibu wa utumishi
K.k boss wako wa ofisini

Kichwa:yah kuomba likizo isiyo na malipo kwa ajili ya kuhudhuria masomo.

Blaah blaah unaandika kuwa utajisomesha kwa malipo yako ili uweze kuongeza ujuzi Zaidi wa kuitumikia sekta yako..
Wako mtiifu
 
Kulia juu address yako
Kushoto chini ya katibu wa wizara
K.K katibu wa utumishi...
Ukijikomiti kuwa unaenda kuongeza kisomo si watataka na barua ya selection, au watataka urudi na cheti ulichokipata huko masomoni?

Sitaingia kwenye sintofahamu baadaye?

Mimi siendi kusoma, nataka kufanya jambo fulani.

Au ukijikomiti unaenda kusoma hawatataka mrejesho baadaye?
 
Nenda halamashauri watakupa form na mwongozo wa kuandika barua
 
Ukijikomiti kuwa unaenda kuongeza kisomo si watataka na barua ya selection, au watataka urudi na cheti ulichokipata huko masomoni?
Sitaingia kwenye sintofahamu baadaye?.
Mimi siendi kusoma, nataka kufanya jambo fulani.
Au ukijikomiti unaenda kusoma hawatataka mrejesho baadaye?
mrejesho lazima hata kama hukutumia hela yao kwenda kusoma
 
Unamwandikia katibu mkuu kiongozi Ikulu unaipitisha barua hiyo kwa mwajiri wako Kama ni halmashauri ni DED, mkoani RAS,wizarani karibu mkuu, mashirika DG or CEO
 
Kamuulize HR wako atakuelekeza cha kufanya.
Habari za usiku waungwana?

Ninataka kupumzika kazi kwa muda wa angalau mwaka mmoja au miwili.

Kuna jambo nataka kulifanya la kibinafsi.

Mimi ni mtumishi wa serikali.

Aliyewahi kuomba likizo isiyo na malipo au anayefahamu kwa undani hili jambo anipe mwanga.

Thanks
 
Habari za usiku waungwana?

Ninataka kupumzika kazi kwa muda wa angalau mwaka mmoja au miwili.

Kuna jambo nataka kulifanya la kibinafsi.

Mimi ni mtumishi wa serikali.

Aliyewahi kuomba likizo isiyo na malipo au anayefahamu kwa undani hili jambo anipe mwanga.

Thanks
"Oya wahusika, sikieni.'
Nikiwa mfanyakazi wenu mtiifu hapa mjengoni, ninawataarifu kuwa kuanzia wiki ijayo nataka kuchukua likizo isiyo na malipo na sitaki mtu aniulize kwanini sitaki kulipwa, nimechoka mie. Ninataka nikirudi nikute nafasi yangu bado ipo, sitaki utani na mtu yeyote yule. Msela nawasilisha, adios.
 
Utapata taabu sana! Mwendazake aliweka sheria kwamba ukiomba likizo ya bila malipo unakuwa umejifuta kazi ili wachukuliwe watu wenye shida na kazi!
 
Habari za usiku waungwana?

Ninataka kupumzika kazi kwa muda wa angalau mwaka mmoja au miwili.

Kuna jambo nataka kulifanya la kibinafsi.

Mimi ni mtumishi wa serikali.

Aliyewahi kuomba likizo isiyo na malipo au anayefahamu kwa undani hili jambo anipe mwanga.

Thanks

Yaani huwezi hata kuandika barua hadi udese. Rudi Shule
 
Unamwandikia katibu mkuu kiongozi Ikulu unaipitisha barua hiyo kwa mwajiri wako Kama ni halmashauri ni DED, mkoani RAS,wizarani karibu mkuu, mashirika DG or CEO
Umeambiwa huyu kibaka, ni mteule wa Rais? Kwa Kuandika kwa chief secretary ni kuwa yeye ni katibu mkuu wa wizara. Mwelekeze asome standard order. Leave without pay ina kanuni za kuombwa na anatoa kibali katibu mkuu Utumishi
 
Andika hicho unachotaka kupewa. Hakuna cha fomati, muhimu ueleze sababu ya likizo hiyo ni nini. Haitoki bila sababu maalum, ni aidha unaenda masomoni nje ya mpango wa mwajiri, unaenda kutumikia ajira taasisi za kimataifa n.k
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom