Msaada: Naomba kujua shule ya secondary nzuri kwa o-level (boarding)

Wasomba

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
323
475
Habarini wanajanvi,

Mwanangu amechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya secondary Morogoro. Natamani nimuhamishe kumpeleka shule ya secondary ya boarding ya serikali yenye ufaulu mzuri ambayo wanaweza kumconsider kulingana na ufaulu wake wa Std 7. Kuhusu Ufaulu wake ni kama ufuatavyo. Hisabati A, Maarifa B, Science, A Kiswahili A na English A. Wastani wa A.
 
Kiswahili ngapi? Alafu ujue mwaka huu wastani wa A walikuwa kibao tena wengi masomo yoote A. Alafu ujue A inaanzia 81 hadi 100. Jumla ya marks katika ufaulu zinaangaliwa katika kupambanisha. Kuna mwingine kapata A lakini alikuwa anacheza na 81 na mwingine kapata A alikuwa anacheza 95 hadi 100. Kama unahela mpeleke private lakini kwenda kulalamika kwanini kapelekwa alipopelekwa unapoteza muda! Kubali sehemu alikopangiwa
 
Kiswahili A. Sina tatizo na hilo. Wala Sijasema wamemuonea. Ninachotaka kumuamisha mwanangu.
 
Changamoto Ni Kubwa Sana
Nadhani Unahitaji Shule Ambayo Ni Nzuri Na Gharama Nafuu. Mpeleke Afrigems Ingawa Wao Hawaangalii Huo Ufaulu Alionao.
Wanampa Mtihani Upya Anatakiwa Apate Kuanzia Marks 40 Kwenda Juu Katika Maswali 50 Yenye Mchanganyiko Wa Masomo Yote.
 
Habarini wanajanvi,

Mwanangu amechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya secondary Morogoro. Natamani nimuhamishe kumpeleka shule ya secondary ya boarding ya serikali yenye ufaulu mzuri ambayo wanaweza kumconsider kulingana na ufaulu wake wa Std 7. Kuhusu Ufaulu wake ni kama ufuatavyo. Hisabati A, Maarifa B, Science, A Kiswahili A na English A. Wastani wa A.
morogoro kunashule inaitwa MGUGU SEC. ipo gairo karibu na ile hospital ya mission
 
Huyo kumuhamishia shule za bweni kawaida.wanafunzi waliochaguliwa waligawanywa katika makundi yafuatayo kulingana na ufaulu wao. 1 Shule za bweni Ufaulu mzuri,hizo shule ni kama Kibaha,Ilboru,Mzumbe, Kilakala na zile za technical.Hawa walipata A zote total marks zilikuwa 230 had I 250(matokeo niliyoona hapa kwetu)Kundi la Pili ni shule za bweni kawaida,hapa wengi walikua Na A nne Na B moja (nafikiri mwanao anafit hapa) Kundi la tatu ni shule za Bweni mahitaji maalumu mf Pugu sec,hapa ni walemavu wamechaguliwa ili mradi awe amefaulu.Kundi la mwisho ni shule za kutwa,hapa nimeona wengi wanawastani wa A B na C.
I

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom