Msaada: Namna ya kuripoti uhalifu wa kutumia silaha za moto bila kwenda Polisi

Restless Hustler

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
4,741
17,995
Niliwahi kuleta Uzi kwa nia ya ku whistle blow taarifa nyeti ya mtu ninayemshuku kuwa ni gaidi wilayani Bwagamoyo.

Nilimshuku mtu huyo baada ya ishara kuu Tatu.
1. Tulianza mijadala ya kawaida ya kidini lakini baadaye akwa nanaishawishi nibadili dini.

2. Alipoona sielekekei kukubaliana naye ndipo akaanza kunitumia SMS za vitisho kuwa yeye ni mujahideen na ana uhakiaka miaka ijayo wataishika dola kwa mtutu wa bunduki na Watu wote ambao siyo Waislam watachinjwa kwa hiyo Ni vyema nihamie dini salama mapema.

3. Alienda mbali na kunieleza kuwa matarajio ya Vita vya Tatu vya dunia vitakuwa Kati ya Waislam na makafiri na wao ndiyo watashinda. Akasema vita hivyo vitaanza hivi karibuni pindi tu hekalu la Sulemani litakapobomolewa.

Nikaingia Google nikajua kumbe mujahideen ni neno linalohusisha wapignaji wa dini Kama Al shabaab, Islamic State nk.

Pia kupitia Google, nilijua kuwa Wayahudi wameanza maandalizi ya kubomoa Hilo hekalu.

Kupitia JamiiForums nilifahamu kuwa Kafiri Ni mtu yeyote ambaye siyo muislam.

Nilipoona habari za mtu huyu zinaweza kuwa kweli na huku nikiamini kuwa JamiiForums Kuna watu wa kila kada, nikaleta taarifa na namba yake ya simu ili wahusika wa ulinzi na usalama wamfuatilie wajiridhishe Kama Ni mtu wa Amani au Ni hatari.

Kwanini niliamua kuleta Habari humu badala ya kwenda Polisi?
1. Yule mtu kwa kinywa chake aliniambia wana mtandao mkubwa serikalini na kwenye majeshi mbalimbali hapa nchini. Nikawaza endapo nikitoa taarifa Polisi na kwa bahati mabaya nitakaowakuta Ni watu wao.

Au nikipiga Simu na baadae nikajikuta kwenye cheni ya upelelezi ambao utanipotezea Muda.

Au Polisi na Wana usalama wengine wakapokea taarifa kwa mihemko na kunishikilia jambo litakalohatarisha kibarua changu.

Leo naomba Wana JamiiForums tufahamishane njia nzuri ya kuripoti matukio ya kiusalama bila kujulikana au kuhatarisha usalama wa mtoa taarifa.
 
Kwa maelezo haya ni wazi ni lazima vyombo vya usalama vikushikilie kwa mahojiano zaidi maana inakuwaje mtu from no where tu mmekutana eti aanze kukulazimisha ubadili dini? Haimake sense hii labda muwe mnafahamiana kiundani na huyo muhusika ndipo inawezekana na nadhani ndio mana vyombo vya usalama vitakutaka uwape ushirikiano zaidi na kitu hicho hutaki, kwanini??
 
Unayo yasema kama ni kweli hapo ulipo si kuna mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa mkuu wa polisi wilaya mkoa nenda kawape habari hizo na namba zake za simu hao nilio wataja hawazi kuhatarisha maisha yako vinginevyo ni mihemko tu
 
Kwa maelezo haya ni wazi ni lazima vyombo vya usalama vikushikilie kwa mahojiano zaidi maana inakuwaje mtu from no where tu mmekutana eti aanze kukulazimisha ubadili dini? Haimake sense hii labda muwe mnafahamiana kiundani na huyo muhusika ndipo inawezekana na nadhani ndio mana vyombo vya usalama vitakutaka uwape ushirikiano zaidi na kitu hicho hutaki, kwanini??
Huyo dogo alishawahi kuweka privacy ya mtu humu na hiyo tabia yake ni wazi kabisa anachuki na watu wa dini Fulani. Vyombo vya ulinzi na usalama SI aende akaripoti! Ukweli huyu dogo angeonja kukaa sero walau masaa matatu angeacha tabia yake ya upashkuna..

Angejua uchungu wa mateso wanayopitia watu walioachwa na ndugu zao Kwa makosa ya kusingiziwa angeacha tabia za kipumbavu..
 
Kama kweli anania njema why aogope kuripoti kwa vyombo vilivyopo jirani nae? Haraka tu inaonesha ana chuki na wote manake kwa maelezo yake ni kama hawaamini hata Polisi ambao watakuwa ni waislam.. Hili ni Tatizo jingine pia.
 
Huyo dogo alishawahi kuweka privacy ya mtu humu na hiyo tabia yake ni wazi kabisa anachuki na watu wa dini Fulani. Vyombo vya ulinzi na usalama SI aende akaripoti! Ukweli huyu dogo angeonja kukaa sero walau masaa matatu angeacha tabia yake ya upashkuna..

Angejua uchungu wa mateso wanayopitia watu walioachwa na ndugu zao Kwa makosa ya kusingiziwa angeacha tabia za kipumbavu..
Ameuliza akareport wapi. Mpe jibu
 
Mhhh hili swala lako litakua vzuri kama tutapata muongozo.
Kipindi kile cha Magufuli hawa watu walishughulikiwa haswa mwingine alikua jirani yetu tu walikuja askari wakamkata usiku kumbe alikua kafuatiliwa muda mrefu.
 
Kwa maelezo haya ni wazi ni lazima vyombo vya usalama vikushikilie kwa mahojiano zaidi maana inakuwaje mtu from no where tu mmekutana eti aanze kukulazimisha ubadili dini? Haimake sense hii labda muwe mnafahamiana kiundani na huyo muhusika ndipo inawezekana na nadhani ndio mana vyombo vya usalama vitakutaka uwape ushirikiano zaidi na kitu hicho hutaki, kwanini??
Vimshikilie kwasababu zipi??
Ameshajieleza kuwa anaogopa mana huyo muhusika amemtaarifu kuwa Kuna watu wao huko kwahiyo hata akienda ni bure mana ni kama kesi ya ngedere umpelekee nyani.
Nyie ndo huwa mnasababisha watu wanakuwa na taarifa sensitive lakini wanashindwa kuripoti wakihofia usalama wao mana ukiripoti unageuka mtuhumiwa na usumbufu mwingi.
Badala wachukue taarifa kuifanyia kazi na kumtumia mtoa taarifa kuwapa taarifa wanamgeuza mtuhumiwa na usumbufu mwingi ndio mana watu wanaangalia tu mpaka yawe makubwa.
 
Shida ukiwa whistle blower police wanakukamata na hamna Sheria inayokulinda na vile watataka uwe shahidi wao kitendo ambacho ni hatari. Inatakiwa wakipata taarifa waifanyie uchunguzi na kulinda ma whistle blower wao
 
Back
Top Bottom