Msaada:mwenye uelewa juu ya solar

Msaada:mwenye uelewa juu ya solar

Brbm

Member
Joined
Apr 16, 2014
Posts
71
Reaction score
6
Katika harakati za kupangiwa vituo vipya vya kazi nilijikuta nimepangiwa sehemu isiyo na umeme imenibidi kununua solar panel wat 50,betri N70 na invetor SI 150 sasa hapa nataka kuchukua tv flat screen inch 18 ila nina wasiwasi kama itaweza kuumudu moto huu.Naomba kwa mtu mwenye uelewa juu ya hili anijuze
 
itafaa maana flat screen inakula moto kidogo sana. ila kwa vile solar zimeshuka sana bei ungechukua panel ya wats 100 ndo ungefurahia maisha ya solar.kwa mwanza kuna duka linaitwa zara solar wanaiuza tsh240000 tu
 
Hiyo solar itasukuma hiyo tv lakini itakua kwa masaa machache ungechukua betry N 100 solar watt 100 na tv iwe na watt ndogo my b 40 up to 50 utaifurahia sola
 
Da vp kama nitaongeza sola pekee ikawa wat 150 ila betri likabaki lilelile tu
 
Da vp kama nitaongeza sola pekee ikawa wat 150 ila betri likabaki lilelile tu

Itakusaidia tu kujaza betri mapema,yaani saa 4 Asubuhi betri itakuwa tayari full na masaa yanayobaki moto utakuwa unapotea bure.Ongeza na betri kama mdau alivyoshauri hapo juu ili upate storage kubwa ya usiku.
 
hiyo inveta ni ndogo najua utakuwa na sabufa na tv na king'amuzi hivyo ni mzigo mkubwa ni bora upat ya watt 250,330 na kuendelea au hiyo 150 mpe fundi asuke upya kuiongeza nguvu.ni mtazamo tu.
 
Natumia kwe sabufa ila mchana tu mara nyingine hata usiku ila kwa muda mfupi na simu nachaji zaidi ya mbili hiyo ndo imenifanya niamini tv itamudu vizuri?
 
Ukubwa wa invetor ie 300 ni nzuri shida yake itamaliza umeme haraka,ila kwa wewe unachotakiwa ni kuwa na panel ya watt 100 control ya 10A na battery N100 utaifurahia
 
Wakuu miye nahitaji solar ambayo inaweza kuwasha TV yenye kisogo ya inchi 32, taa 16, pasi ya solar na redio kubwa. Sijajua nahitajika ninunue panel ya ukubwa gani, inverta na betri ya ukubwa gani? Charge control pia zinatofautiana ukubwa? Tafadhali mwenye ujuzi katika hili
 
Katika harakati za kupangiwa vituo vipya vya kazi nilijikuta nimepangiwa sehemu isiyo na umeme imenibidi kununua solar panel wat 50,betri N70 na invetor SI 150 sasa hapa nataka kuchukua tv flat screen inch 18 ila nina wasiwasi kama itaweza kuumudu moto huu.Naomba kwa mtu mwenye uelewa juu ya hili anijuze

sola panel uliyonayo ni ndogo ukilinganisha na betri ulio nunua, inveter sawa , tatizo betri itakua haijai coz panel ndogo hivyo utakua unaangalia mda mdogo, ongeza panel ya 40w , na chage control ya 10A, hakikisha unatumia waya za 4mm kutoka kwenye panel , control , betri, invertet
 
unataka kueasha taa 18 na tv ya 32 inch redio na feni, fafanua kuhusu taa za dc au ac, km za dc utahitaji panel ya 100w , betri 140N, controler 30A, inverter 300w, cable za main supply 6mm, km taa za dc fanya wiring kwa cable ya 2.5. pasi haiwezekani kwa mfumo huu
 
muhimu kuzingatia katika mfumo wa sola pamoja na uwezo wa panel, betri na low consuption ya appliance umbali na size ya waya ni muhimu ku calculate sababu ya tabia ya umeme wa dc ili kupata matokeo mazuri
 
Muda wote ktk matumizi ya umeme jua unashauriwa kutumia vitu vinavyotumia umeme mdogo.sasa unaposema pasi,kwanza hakuna pasi ya solar.unaweza kuitumia ila ikawahi sana kumaliza moto wako ktk betri
 
unataka kueasha taa 18 na tv ya 32 inch redio na feni, fafanua kuhusu taa za dc au ac, km za dc utahitaji panel ya 100w , betri 140N, controler 30A, inverter 300w, cable za main supply 6mm, km taa za dc fanya wiring kwa cable ya 2.5. pasi haiwezekani kwa mfumo huu

Mkuu wiring imeshafanyika ya kawaida sasa sijajua kama itaendana na mfumo wa DC. Kwahiyo nilikuwa nafikiri itabakia AC.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Muda wote ktk matumizi ya umeme jua unashauriwa kutumia vitu vinavyotumia umeme mdogo.sasa unaposema pasi,kwanza hakuna pasi ya solar.unaweza kuitumia ila ikawahi sana kumaliza moto wako ktk betri

Asante mkuu,
Hivi mfumo mzuri ni upi kati ya AC na DC kwa maana ya kuwasha taa kwa muda mrefu. Watumiaji wa solar wanaweza tuambia hili kwa uhakika zaidi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Muda wote ktk matumizi ya umeme jua unashauriwa kutumia vitu vinavyotumia umeme mdogo.sasa unaposema pasi,kwanza hakuna pasi ya solar.unaweza kuitumia ila ikawahi sana kumaliza moto wako ktk betri

Pasi za solar zipo mkuu!
 
Ninazo Tv za solar 4w
pasi za Solar 6w
Bulb za solar 1w,2w,3w
na vifaa vyote vya solar kwa anaetaka tuwasiliane
 
Ninazo Tv za solar 4w
pasi za Solar 6w
Bulb za solar 1w,2w,3w
na vifaa vyote vya solar kwa anaetaka tuwasiliane

Mkuu hizo pasi unauzaje?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom