Msaada: Mnafanyaje mambo yenu yaende poa?

Msaada: Mnafanyaje mambo yenu yaende poa?

Kazi na biashara..Kiuchumi kwa ujumla

Nitakupa a generic answer sababu mada yako ipo hivyo pia.

Biz haina mambo ya imani either uchawi au Mungu ndo maana kuna watu wapagani wanatoboa na wengine waumini nao wanatoboa au kufeli equally.

Haya mambo ni kujua your strengths and weaknesses and work on them. Kila mtu anajua hali yake so mtu wa kukutoa hapo ulipo ni wewe mwenyewe.

Aidha just working hard won't cut it you ought to work smart as well.

Fuata principles/basics za biashara, soma soko lako vilivyo fanyia kazi.

Mwisho, one needs to know when to call it quits. Kuna mambo mengine yanadinda mwanzo mwisho haina sababu ya kuendelea kung'ang'ania na kupoteza rasilimali hapo, tafuta shughuli nyingine move on. Such is life.
 
Nitakupa a generic answer sababu mada yako ipo hivyo pia.

Biz haina mambo ya imani either uchawi au Mungu ndo maana kuna watu wapagani wanatoboa na wengine waumini nao wanatoboa au kufeli.

Haya mambo ni kujua your strengths and weaknesses and work on them. Kila mtu anajua hali yake so mtu wa kukutoa hapo ulipo ni wewe mwenyewe.

Aidha just working hard won't cut it you ought to work smart as well.

Fuata principles/basics za biashara, soma soko lako vilivyo fanyia kazi.

Mwisho, one needs to know when to call it quits. Kuna mambo mengine yanadinda mwanzo mwisho haina sababu ya kuendelea kung'ang'ania na kupoteza rasilimali hapo, tafuta shughuli nyingine move on. Such is life.
Thank you
 
Keep on praying, wakati wako waja...

Hujasema mambo gani Ila? Stress kila kona how?

Mfanowe me siku hizi Nina vihasira vya hapa na pale, kuna muda naona Kama sijielewi 😁 Ila najua 7bu. Kichupa kimejaa sana... Hebu check na huko kwanza u boost akili.
For sure! Ukipigwa pipe stress zinapungua hapo sasa unaweza kufanya mambo yako kiufanisi zaidi
 
Ndugu yangu nasali lakini wapi...

Watu wako mtaani huku wanashinda kwa Mwamposa na bado hawatoboi tunawapa buku buku kila siku wengine tunshinda juu ya viti virefu ila maisha si haba, my point is yaangalie maisha face to face achana na wanaokwambia sijui uwe msafi rohoni na blah blah kibao.
 
Habari zenu,

Ndugu zangu, mnaombaje kwa Mungu mpaka mnapata baraka tele. Mimi binafsi kila ninachogusa mambo hayaendi, stress kila corner mpaka kuna wakati unatamani ujiwaishe tu mbinguni.

I am working really hard and sitamani kukataa tamaa zaidi.Naombeni ushauri huwa mnafanyaje fanyaje mambo yenu yaende poa.

Asante.

futa vitu hivi
-watu walio karibu ambao ni mzigo na sio support kuanzia michongo,kazi,dili na muongozo.
-nenda na wakati na mazingira unachokifanya kuna watu wanang’ang’ania sehemu moja au biashara hiyo hiyo wakati imeshampita wakati au mungu kakwambia jaribu kingine.
-toka sehemu ambayo miaka nenda rudi hupo nayo
 
Habari zenu,

Ndugu zangu, mnaombaje kwa Mungu mpaka mnapata baraka tele. Mimi binafsi kila ninachogusa mambo hayaendi, stress kila corner mpaka kuna wakati unatamani ujiwaishe tu mbinguni.

I am working really hard and sitamani kukataa tamaa zaidi.Naombeni ushauri huwa mnafanyaje fanyaje mambo yenu yaende poa.

Asante.
Kwa Mungu ndio penyewe.

Naweza kujua dini/dhehebu lako ili watu watakapokushauri namna ya kumuendea Mungu wasiende nje ya misingi ya imani yako.

Ila msingi Mkuu ni IMANI KAMILIFU KWA MUNGU.
 
Kwa kiasi chake yes .
Katika maisha ya kiroho na kimwili wapoje? Tafakari mwenyewe!
Kama upo mule mule basi shughuli ya kujichomoa ni pevu, kama ni vice versa shughuli ya kujichomoa ni simple! Karibu!
 
Wala siyo kwamba wengine wanapendelewa ila kwa neema tu
1. Jiepushe kuwa na marafiki wa kupiga soga. Kuwa na marafiki wa kwenye kutafuta kazi, kuangalia fursa. Mnapigiana simu, kuna kazi fulani twende tukafanye
2. Penda kuchangamana na watu ila wenye malengo hasa angalia waliokuzidi umri au umri sawa ila malengo ya kutoboa
3. Usipende kubagua kazi. Mfano mm huwa sichagui kazi ili mradi iwe halali. Anza hata kukaanga chapati uza
Kadri unavyozidi kupambana ndiyo Mungu anakufungulia baraka
4. Siri ambayo ni ngumu na rahisi kutoboa. Kuishi mbali na ndugu, huko hakuna msaada wowote zaidi ya kujipigania. Lazima upambane utoboe
5. Kupunguza matumizi yasiyo ya msingi
6. Nyumba hizi tunazokaa huwa zina neema au mikosi. Unaweza kuwa kwenye lkn kila unachofanya hakifanikiwi ila nyumba nyingine ukafanikiwa
7. Usichoke kumuomba Mungu siku zote.
ushauri safi Sana Huuu.
 
Kwanza pole sana, pole sana kwa kuwa wewe unadhani wewe ndiye unayepitia changamoto ili hali binafsi nadhani si kweli!
Kuna watu wanapitia nyakati ngumu wala hawawezi kupata bando wakapost ulichofanikisha kupost hapa! Wewe unasmart na unaweza kuwa na bando, mshukuru Mungu!
Naomba nikwambie jambo, kuna usemi kuwa "makipo ni hapahapa duniani" au "apandacho mtu ndicho avunacho"!
Sasa, kuna watu wanapitia nyakati ngumu kwa kulipa matendo yao wenyewe ya nyuma, au ya wazazi ama wazee wake ambao walitenda yasiyofaa na wenyewe binafsi hawakukamilisha kulipa matendo hayo! Yaani kama utasadiki usemi wa malipo ni hapa hapa duniani, maana yake matendo yetu yote hulipwa hapahapa na matendo ya wema humlipa mtu wema vilevile, na ukitenda wema na hulipwi sawa sawa na wema wako, tambua upo katika orodha ya kulipa nakosa yaliyofanywa kwa generation yako hasa wazee wako hapo zamani na siku deni litakapoisha, taa ya kijani unakuwa upande wako!
Wengi tunapitia nyakati ngumu kwa matendo yetu ama ya wazee wetu magumu ya nyakati za nyuma! Tafakari na ubaini ukweli ktk hili nazungumza maana kanuni ni ile ile ukipanda uovu utavuna uovu pia, kama si wewe basi uzao wako! Na huo ndo msemo wa akipandacho mtu ndicho avunacho!
Endelea kutenda wema ipo siku utanufaika na wema huo lakini ikitokea hujanufaika wewe, basi uzao wako utanufaika na wema wako wa leo!
Tena niseme, hata uchukulie mambo kimasihara nisemayo haiondoi maana ya misemo hiyo niliyoitaja! Jiepushe na maisha ya kuigiza, ishi maisha yako halisi wala usidhani kufanya mambo kwa kujifika machoni pa watu kutakuepusha na matokeo ya matendo yako!
Samahani usinielewe vibaya, natamani uelewe binafsi kwa nini unapitia nyakati ngumu na uanze safari ya kusafisha mapito yako na ya uzao wako!
Pia yapo matendo yaliyokosewa na wazee wako ambayo deni lake kulipika ni ngumu sana, tunaita laana! Kuichomoa laana ni mtihani ila zipo njia za kuifuta na usipoifuta leo, itawaandama pia uzao wako! Ipo mimea ukielekezwa namna ya kuitumia huondoa na kufuta laana! Lakini kwanza tafakari, unadhani kwa nini unapitia nyakati ngumu!
Niyo mengi ya kukueleza lakini naomba nitoe rai kuwa, ukiguswa na haya nisemayo, uliza swali lolote nitakuelekeza cha kufanya ili twende pamoja!
Mimi hii ndio naikataaga. Yaani kosa afanye babu yangu huko nyuma kabla sijazaliwa afu me mtu mwingine nibebe msalaba hapana kwa kweli. Huucni uonevu wa hali ya juu. Imagine me nifanye kosa afu mwanangu aje apate shida kisa eti mimi kuwa ni baba ake yeye ndo iwe shida na mahangaiko kwake. Sijui hii imekaaje
 
Kwa Mungu ndio penyewe.

Naweza kujua dini/dhehebu lako ili watu watakapokushauri namna ya kumuendea Mungu wasiende nje ya misingi ya imani yako.

Ila msingi Mkuu ni IMANI KAMILIFU KWA MUNGU.
Mimi mkristo.Ila msaada hauangalii dini
 
Katika maisha ya kiroho na kimwili wapoje? Tafakari mwenyewe!
Kama upo mule mule basi shughuli ya kujichomoa ni pevu, kama ni vice versa shughuli ya kujichomoa ni simple! Karibu!
Wapo kawaida tu..Mimi nimejitenga kiukweli cuz napitia wakati mgumu kidogo..
 
Mimi hii ndio naikataaga. Yaani kosa afanye babu yangu huko nyuma kabla sijazaliwa afu me mtu mwingine nibebe msalaba hapana kwa kweli. Huucni uonevu wa hali ya juu. Imagine me nifanye kosa afu mwanangu aje apate shida kisa eti mimi kuwa ni baba ake yeye ndo iwe shida na mahangaiko kwake. Sijui hii imekaaje
Kama unaarithi genetic Sasa utashindeaje kubeba mzigo wa roho za kale
 
Mimi hii ndio naikataaga. Yaani kosa afanye babu yangu huko nyuma kabla sijazaliwa afu me mtu mwingine nibebe msalaba hapana kwa kweli. Huucni uonevu wa hali ya juu. Imagine me nifanye kosa afu mwanangu aje apate shida kisa eti mimi kuwa ni baba ake yeye ndo iwe shida na mahangaiko kwake. Sijui hii imekaaje

Mambo ya imani kama hizi za wafia dini sijui makosa ya babu alipe mjukuu ni NONSENSE. Mleta uzi akitaka akate ringi kabisa aendeleze hayo.
 
Mimi mkristo.Ila msaada hauangalii dini
Ukitaka msaada usiwe na KIHEREHERE AU KIMDOMO KASUKU.. Wewe ni mkristo, bila shaka unafahamu Umuhimu wa Jina na Damu ya Yesu Kristo.

Je, mtu tofauti na imani yako ya kikristo anaweza kukushauri hayo?

Au, mtu ambaye si mkristo unaweza kumshauri namna ya kumuendea Mungu kwenye Maombi kwa kutumia Jina la Yesu Kristo?
 
Back
Top Bottom